Mkuu
Hapana ni kwamba nimeangalia umesema ukweli mchungu sana.
Kinachoendelea kwenye madhabahu leo ndicho Yesu alichokikataa. Ukisoma maandiko utaona ninachokiongea. Wewe umeandika, mimi nimefunuliwa
Mathayo 24:3
Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?
Mathayo 24:4
Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.
Mathayo 24:5
Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.
Mathayo 24:6
Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.
Mathayo 24:10
Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
Mathayo 24:11
Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.
Mathayo 24:12
Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
Mathayo 24:15
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),