Mchungaji huyu nitampataje?

Mchungaji huyu nitampataje?

Wahubiri wengi wanajua yawapasayo kufanya ila utendaji sasa ndo mtihani.

Ukisikiliza mahubiri ya Kakobe yalivyojaa makaripio utasema yes huyu ndiye malaika wa mwisho aliyetumwa na Mungu kuionya dunia .

Sasa uje kwenye maisha halisi, utakuta account ina bilioni 5 na kuna muumini anakwenda kupita mbele(madhabahuni) aombewe apate elfu 50 ya mtaji wa matunda. Naye bila aibu anaweka mikono kumbariki apate hitaji lake huku anashindwa kuchota laki 2 ambariki.

Wahubiri wengi ndio watakaotangulia jehanamu, maana wanajua yawapasayo kutenda ila hawatendi.
Dhambi wanayoikemea ni don't do only.

Huku dhambi ziko za aina 2.

Usifanye na fanya.

Mtu ana lijumba likubwa la mabilioni ndani yuko yeye na mke na watoto wake tu anashindwa hata kukaa na mtoto wa dada yake
 
Ila kweli
Utumishi wa mtu yeyote haupimwi kwa miujiza, kiasi cha waumini au mahubiri yake.

Pima matendo ya upendo.

Haiwezekani mchungaji unamiliki private jet ya mabilioni huku kanisa lako kuna watu wanatoa sadaka sh. Elfu 10 ya kujimaliza ili wavute muujiza wa kupata kazi.

Love.

Upendo.

Hiki ndicho kipimo mujarabu.

Kuna watu kanisani kwako wanaishi kwa mlo mmoja na wewe unanena kwa lugha huku benki una bilioni moja.

No.no.no
 
Unadhan maamrisho yanavyosema toeni katika aliyowaruzuku Mola wenu yanamaanisha nini? Maamrisho ya kulisha masikini, kutoa zaka , na kulisha yatima ni kwa ajili gani?

Kwa ulichokiandika ina maana kila ukipatacho utumie peke yako, huo ni ubinafsi na sio Mungu anavyotaka tuishi.

Naimani hata hyo kazi uliyonayo unamtegemea mtu mwingine, acha kukimbilia maneno ya ovyo kwa nini dada azae ikiwa hana uwezo
Kwani huyo mtoto wa dada yake hana mama na baba au wao kazi zao ni kunyanduana na kuzaa na kutupia wengine walee na kusomesha?
 
Andiko lako limeuchoma moyo wangu sana sana.

Ninamfahamu Kakobe nafahamu maisha yake lakini andiko lako limenigusa mimi kuliko unavyodhani.

namuomba Mungu anipe unyenyekevu
Wahubiri wengi wanajua yawapasayo kufanya ila utendaji sasa ndo mtihani.
Ukisikiliza mahubiri ya Kakobe yalivyojaa makaripio utasema yes huyu ndiye malaika wa mwisho aliyetumwa na Mungu kuionya dunia...
 
Wahubiri wengi wanajua yawapasayo kufanya ila utendaji sasa ndo mtihani...
Kwa kweli Kakobe sijui alikengeuka wapi, jamaa ni bonge la mhubiri, anapiga gombo balaa ila sasa matendo yake ndio yana walakini wa kumtoa kwenye utumishi.

Kama ulivyoeleza, wakati mwingine ni kama anawaibia waumini wake maskini, amekataza kutoa sadaka za coin kanisani (Tshs. 200/=) kwamba watu watoe kuanzia jero, unaona kabisa hapo focus ni pesa. Ile ishu ya Gwajima na mkono wa Baunsa nae akaitwa kwenda kumsafisha Bwana Rashid, aisee nilisikitika sana, Kakobe.
 
Unadhan maamrisho yanavyosema toeni katika aliyowaruzuku Mola wenu yanamaanisha nini? Maamrisho ya kulisha masikini, kutoa zaka , na kulisha yatima ni kwa ajili gani?

Kwa ulichokiandika ina maana kila ukipatacho utumie peke yako, huo ni ubinafsi na sio Mungu anavyotaka tuishi.

Naimani hata hyo kazi uliyonayo unamtegemea mtu mwingine, acha kukimbilia maneno ya ovyo kwa nini dada azae ikiwa hana uwezo
Kila mtu ashinde mechi zake.
Kusaidia kupo lakini sio kwa kubweteka kwa kuwa fulani yupo.
 
Nisamehe kama nimekukwaza
Mkuu
Hapana ni kwamba nimeangalia umesema ukweli mchungu sana.

Kinachoendelea kwenye madhabahu leo ndicho Yesu alichokikataa. Ukisoma maandiko utaona ninachokiongea. Wewe umeandika, mimi nimefunuliwa

Mathayo 24:3
Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?

Mathayo 24:4
Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

Mathayo 24:5
Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

Mathayo 24:6
Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

Mathayo 24:10
Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.

Mathayo 24:11
Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.

Mathayo 24:12
Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.

Mathayo 24:15
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
 
Haya maandiko uliyowaatacch ni mazito
Mwenye masikio na asikie
 
Nimejisikia vibaya sana kwakweli. Ndo maana shetani anaimani kubwa atavuna wengi na tusipoangalia watu tutakua kuni humu hatari. Wengi wetu tunahubiri A tunafanya B. Kuna akina sie kutwa kuhubiri kumbe ndo tutakaobaki masihi akirudi. Ooh God forgive us.
 
Naona mmeuvamia uzi wangu na kutoka nje ya kile nilichoandika. Sijui kwa nini mmekuja kumalizia hasira zenu hapa.

Niliyeandika huu uzi sijawauliza kuhusu maisha ya wachungaji. Naomba kuhusu maisha ya watumishi anzisha uzi wako. Mimi nahitaji kumpata huyu hayo mengine sio sehemu yake hapa
 
Utumishi wa mtu yeyote haupimwi kwa miujiza, kiasi cha waumini au mahubiri yake.

Pima matendo ya upendo.

Haiwezekani mchungaji unamiliki private jet ya mabilioni huku kanisa lako kuna watu wanatoa sadaka sh. Elfu 10 ya kujimaliza ili wavute muujiza wa kupata kazi.

Love.

Upendo.

Hiki ndicho kipimo mujarabu.

Kuna watu kanisani kwako wanaishi kwa mlo mmoja na wewe unanena kwa lugha huku benki una bilioni moja.

No.no.no
Kwa nini mnakerwa na watumishi kuwa na Mali? Nini maono yenu mnataka wawe maskini? Ayubu alikuwa tajiri na suleman alikuwa tajiri mchungaji hajakuzuia wewe kuwa na Mali tafuta utapata wakiwa maskini bado hamtasaidia kitu ,unaenda kanisani ukiwa maskini Ili ukasaidiwe au unaenda kukua kiroho ? Acheni mijadala ya kipumbavu
 
Kwenye kutoa sadaka ukiifahamu hizi kanuni basi utafanikiwa sana

Toa kwa Mungu si kwa mwanadamu, namaanisha uconnect moyo wako na sadaka kwa Mungu, na usijali sana inaenda kutumikaje sababu kama mtu ataitumia ndivyo sivyo ni yeye na Mungu wake ila wewe kama wewe unakuwa umetimiza wajibu wako kwa Mungu

Hakuna madhabahu bila sadaka, ibada kamili inakamilishwa na sadaka na hivyo basi sadaka ni kwa ajili ya utimilifu wa ibada yako na sio kwa ajili ya mtumishi japo biblia inasema watakula madhabahuni. Kumbuka wale wa upande wa giza wanatoa sadaka ngumu sana ili wapate utajiri wa kipepo na the higher the sacrifice the higher the outcome hata huku kwetu nuruni kanuni huwa ni moja. Sadaka kubwa haina maana ya fedha nyingi inaweza kuwa muda wako, huduma, fedha au chochote ambacho kitaugusa moyo wa Mungu.Mfano wewe ni fundi ujenzi unaweza kujitolea kujenga nyumba ya Mungu kwa kutoa sadaka ya ujuzi wako, huna fedha unaweza kujitolea kudeki kanisa au kudeki choo cha kanisa etc.

Kingine toa sadaka kwa kadri Roho wa Mungu anavyokuongoza sio wale wa laki pita mbele ili upewe mafuta au maombi maalumu na wewe unapita, kama umeongozwa na Roho wa Mungu kufanya hilo sawa ila tusitoe sadaka kwa mihemko. Maandalizi ya sadaka yanapaswa kuanzwa mapema na ikifika jmosi au jpili unajua kabisa nimeandaa sadaka yangu kumtolea Mungu na kwa heshima zaidi unaweza kuwa na bahasha yako kama kanisa halina utaratibu ya bahasha maalumu. SADAKA NI IBADA HIVYO TUIPE HADHI YAKE INAYOSTAHILI.

Lkn muhimu zaidi ni kumuomba Mungu atuongoze kwenye madhabahu sahihi za kumtolea Mungu sababu si kila.madhabahu ni ya KiMungu na kujua hilo unapaswa kuwa Rohoni na hata sehemu ya kuabudu ukimwomba Mungu akuongoze atakuongoza sababu siku hizi huduma zipo nyingi na sio wote wanamtaja Mungu ni wa Mungu wa kweli.

MUNGU AWABARIKI
 
Back
Top Bottom