Palikuwa na habari humu kumhusu mchungaji wa kanisa la wasabato na ofisa wa Takukuru kahama:
www.jamiiforums.com
Habari mpya ni kwamba lengo la mtakukuru hatimaye limetimia na mtumishi wa Mungu kafukuzwa kazi.
Pole mchungaji lakini hukumu za haki ni za mola peke yake.
Kufukuzwa kwake mchungaji huyu kumefanikishwa na kuongezwa kwa tuhuma kuwa yeye alilIfikIsha suala lake kwenye vyombo vya habari jambo ambalo si kweli.
Kwa bahati mbaya sana wasichokijua kanisa, uongozi wa kanisa (conference), waumini na hata mchungaji mhanga na mke wake ni kuwa mtakukuru kajipenyeza ndani yao kweli kweli. Itawachukua muda sana kukitambua kiwalacho.
Kiwalacho ki nguoni mwao.
Huyu bwana yumo hadi kwenye vikao vyenye kupendekeza maamuzi magumu kufanyika ngazi za juu (conference). Ambapo ngazi za juu kwa kawaida huthibitisha tu mapendekezo hayo.
Hakuishia hapo, bali kajipenyeza hadi kwenye baadhi ya ofisi ambazo waumini wengi wa kanisa hilo huzitumia kwa ushauri wa kisheria wakiamini damu ni nzito kuliko maji.
Matokeo yake bila kujua mchungaji na mkewe wamekuwa wanashauriwa kisheria na mtakukuru yule yule kupitia vipandikizi huku yeye akiwasubiri kuwashughlikia kwa Pilato na kwenye kamati za maadili kanisani pia.
Anatoboa vipi mchungaji mwaminifu wa Mungu hapo?
Ushauri wa bure kwake, kimlacho ki nguoni mwake:
1. haraka sana aende ikiwezekana mkoani kuonana na mawakili wengine kwa ushauri.
2. Kwa vile anajua hajatendewa haki, akae mbali kabisa na conference kwa sasa.
3. Asikubali ushauri wowote wa conference, washauri wao au wenye kumshauri kuhusiana na lolote kwenye jambo hili, ila mawakili wapya Shinyanga.
Akumbuke si nadra kufanyika makosa ya kimaamuzi panapo kukurupuka, fitna au hila.
Mabilioni ya shilingi ya fidia yanaweza yakamhusu akijipanga sawa sawa.
Mungu hajawahi kumtupa mja wake (Zab 23).
Pole mchungaji, jipe moyo. Mwana wa Mungu atatenda.
Mchungaji wa kanisa la Wasabato Kahama na familia yake wasoteshwa rumande kwa kesi ya dawa za kulevya
Imekuwa dhuluma hadi kwa watumushi wa Mungu. Raia wema wakimbilie wapi? Katika hali ya kushangaza Mchungaji mmoja wa kanisa la wasabato wilayani Kahama na familia yake wamejikuta wakinyanyasika pasipokuwa na uhalali wowote kufikia kuswekwa ndani na kulala rumande. Kadhia hii imemkuta mchunga...