Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Hiyo sio kweli ya Mungu, kweli pekee ina Mungu wetu.
Pesa/ Mali/Wenye mali, haya mambo ndo yanalitesa kanisa la sasa.... ndomana walifukuzana kila mmoja akaanza kudai miradi ni yake..... warudi enzi za kina Elisha hawakufagilia hayo mambo...
 
Exactly. Tusaidiane kuwaelimisha hawa mambumbumbu wasiendelee kuwapotosha watu kuhusu madini anayotema Dr Kimaro.
Hawa waabudu "MAJINI" toka huyu mchungaji wao awasifie bado kdg watamlamba matako....
 
Ashaanza kulewa sifa, mapinduzi makubwa katika kitabu cha matendo na uzihirisho wa roho Mtakatifu walifanya matajiri? Shida ni jina Kimaro.
Wakatishia kumhamisha "kati kati" ya mji wampeleke shamba akangua kilio, amshukuru sana Shoo, angetupwa Ruvuma....
 
Nimeipenda hii!.
Umasikini ni laana!.
Ila Yesu alitueleza jinsi ilivyo rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia peponi

P.
 
Nini kazi ya Kanisa ? Tuanze kwanza hapo; nadhani majibu ya hayo ndio tutajua kama anachosema ni kweli sio kweli; After all haya ni Mambo ya Imani na ukiamua kuamini kitu - who are we to say otherwise...

By the way kwahio Yesu did not know better yaani angejua yatakayotokea huenda angefanya kina Petro wakawa matajiri (Kama aliweza kubadilisha maji yakawa wine asingebadilisha mchanga kuwa marumaru...) Au ya Kaisari alimuachia Kaisari ?
 
Endeleeni kukaa kwenye Comfort Zone. Ukifanya deep analysis kwa alichosema Mchungaji sidhani kama ni issue ya kuichikulia in negative perspective. Kusudi la uumbaji halikuwa mwanadamu kuishi hali ya umaskini. Kanisa linahitaji matajiri, umaskini ni uovu, shame on us tunaotetea umaskini
 
Ndio maana sisali tena. Pale.

Jamaa anapotosha mandiiko.

Petro ndio msiingi wa kanisa. Na hakua tajiri.

Hiyo ya Arimathaya ni sadaka kama nyingine tu.

Hapo kijito washarika wana pesa na wanamhudumia hivyo lazima awapaishe.
Kila mtu ana nafasi yake kanisani na hapa duniani kwa ujumla.
Awe masikini au tajiri, wote wana umuhimu na wajibu kwa kadiri wanavyoweza.
Hata hivyo, kumekuwa na tabia ya masikini (walio wengi) kujifariji kuwa wao ndiyo wa Mungu zaidi (wakitumia neno la ngamia na tajiri) kitu ambacho siyo kweli.
Ukifanyika utafiti rasmi, masikini wanaweza kuwa na roho mbaya kuliko matajiri, hivyo ikawa vigumu zaidi kwa masikini kuingia mbinguni.
 
Ni ngumu sana kuwa tajiri bila kuua, kudhulumu na kuiba.

Yote hayo yanamfanya tajiri awe na chances ndogo Sanaa kiimani.

Kwa macho ya kibinadamu tajiri anaonekana kama mtu muhimu Sanaa ila kwa Mungu wote ni sawa tu.

Ila huyo Mchungaji anapenda pesa na kuna msharika hapo kaanisaani anapesa na ni mtu wake wa karibu anamsaafisha.
 
Umeongea vema sana mkuu. Nilichogundua ni kwamba watu wengi wanaotoa maoni hasi humu wana umbumbumbu wa kutosha kuhusu neno la Mungu. Wangekuwa na uelewa wala wasingehoji madini aliyotema Mch Dr Kimaro bali wangemshukuru kwa kuwa na karama ya kufundisha neno la Mungu kwa mifano halisi ya kipindi tulichopo kama alivyofanya Bwana wetu Yesu Kristo wakati akihubiri injili kule Galilaya na maeneo mengine ya nchi.

Tuwasaemehe bure wale wote walioshindwa kumuelewa Dr kimaro kwani sio wao bali ni uelewa wao mdogo uliochanganyika na nguvu za giza ndio unawafanya wasimuelewe moja kwa moja kuhusu mafundisho yake.
 

Acha kutetea makosa. Mchungaji kachemka Mara ya pili, nadhani hajajufunza.
 
Pesa/ Mali/Wenye mali, haya mambo ndo yanalitesa kanisa la sasa.... ndomana walifukuzana kila mmoja akaanza kudai miradi ni yake..... warudi enzi za kina Elisha hawakufagilia hayo mambo...
Hatasijakuelewa, unazungumzia Kanisa lipi? Nani waliofukuzana wakadai mali? Mimi nazungumzia Kanisa la Kristo.
 
Ukiwa na akili ndogo kama mbegu ya hardali huwezi kumuelewa Mch Dr Kimaro. Muombe Mungu akupe hekima uelewe madini anayotema Dr Kimaro.
Kama kumuelewa ni kugumu hivyo, basi hafai. Mchungaji mzuri ni yule anayeeleweka vizuri na kila mtu, na hasababishi taharuki kwa mahubiri yake.
 
Siyo kweli kwamba ili uwe tajiri kuna ugumu bila kuua, kuiba au kudhulumu.
Haya ni mawazo mabaya yanayotaka utajiri wa haraka haraka.
Ni muhimu watu wajifunze kufanya kazi kwa bidii yenye akili, kwa muda unaotosha na utajiri utapatikana vivyo hivyo. Msingi wa utajiri unaweza kuanzisha wewe lakini wakaja kuonekana matajiri wanao au wajukuu.
Watu wajue kweli ili wawe huru kuhusu hali zao kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…