Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Hiyo sio kweli ya Mungu, kweli pekee ina Mungu wetu.
Pesa/ Mali/Wenye mali, haya mambo ndo yanalitesa kanisa la sasa.... ndomana walifukuzana kila mmoja akaanza kudai miradi ni yake..... warudi enzi za kina Elisha hawakufagilia hayo mambo...
 
Exactly. Tusaidiane kuwaelimisha hawa mambumbumbu wasiendelee kuwapotosha watu kuhusu madini anayotema Dr Kimaro.
Hawa waabudu "MAJINI" toka huyu mchungaji wao awasifie bado kdg watamlamba matako....
 
Ashaanza kulewa sifa, mapinduzi makubwa katika kitabu cha matendo na uzihirisho wa roho Mtakatifu walifanya matajiri? Shida ni jina Kimaro.
Wakatishia kumhamisha "kati kati" ya mji wampeleke shamba akangua kilio, amshukuru sana Shoo, angetupwa Ruvuma....
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama amesema Tajiri Yusuf wa Almathaya ndio aliyemzika Yesu katika kaburi lake la kifahari

Kimaro amesema Kanisa linawahitaji Matajiri kwa sababu ndio wanaoliondolea Kanisa aibu Wakati wa uhitaji

Hivyo tusiwape majina mabaya Matajiri kwa kuwaita Mafisadi, Wahujumu Uchumi au Freemason Kwani utajiri ni baraka hata katika level ya familia Kwani ndio wanaofuta aibu za familia, amesisitiza mchungaji Kimaro

Kimaro amesema Watu wengi ni walinzi tu wa makaburi kama wale Walinzi wa Pilato waliotumwa kulinda kaburi la Yesu, hivyo wewe kama mkristo usikubali kuwa Mlinda makaburi

Nawatakia Pasaka Njema!
Nimeipenda hii!.
Umasikini ni laana!.
Ila Yesu alitueleza jinsi ilivyo rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia peponi

P.
 
Nini kazi ya Kanisa ? Tuanze kwanza hapo; nadhani majibu ya hayo ndio tutajua kama anachosema ni kweli sio kweli; After all haya ni Mambo ya Imani na ukiamua kuamini kitu - who are we to say otherwise...

By the way kwahio Yesu did not know better yaani angejua yatakayotokea huenda angefanya kina Petro wakawa matajiri (Kama aliweza kubadilisha maji yakawa wine asingebadilisha mchanga kuwa marumaru...) Au ya Kaisari alimuachia Kaisari ?
 
Endeleeni kukaa kwenye Comfort Zone. Ukifanya deep analysis kwa alichosema Mchungaji sidhani kama ni issue ya kuichikulia in negative perspective. Kusudi la uumbaji halikuwa mwanadamu kuishi hali ya umaskini. Kanisa linahitaji matajiri, umaskini ni uovu, shame on us tunaotetea umaskini
 
Ndio maana sisali tena. Pale.

Jamaa anapotosha mandiiko.

Petro ndio msiingi wa kanisa. Na hakua tajiri.

Hiyo ya Arimathaya ni sadaka kama nyingine tu.

Hapo kijito washarika wana pesa na wanamhudumia hivyo lazima awapaishe.
Kila mtu ana nafasi yake kanisani na hapa duniani kwa ujumla.
Awe masikini au tajiri, wote wana umuhimu na wajibu kwa kadiri wanavyoweza.
Hata hivyo, kumekuwa na tabia ya masikini (walio wengi) kujifariji kuwa wao ndiyo wa Mungu zaidi (wakitumia neno la ngamia na tajiri) kitu ambacho siyo kweli.
Ukifanyika utafiti rasmi, masikini wanaweza kuwa na roho mbaya kuliko matajiri, hivyo ikawa vigumu zaidi kwa masikini kuingia mbinguni.
 
Kila mtu ana nafasi yake kanisani na hapa duniani kwa ujumla.
Awe masikini au tajiri, wote wana umuhimu na wajibu kwa kadiri wanavyoweza.
Hata hivyo, kumekuwa na tabia ya masikini (walio wengi) kujifariji kuwa wao ndiyo wa Mungu zaidi (wakitumia neno la ngamia na tajiri) kitu ambacho siyo kweli.
Ukifanyika utafiti rasmi, masikini wanaweza kuwa na roho mbaya kuliko matajiri, hivyo ikawa vigumu zaidi kwa masikini kuingia mbinguni.
Ni ngumu sana kuwa tajiri bila kuua, kudhulumu na kuiba.

Yote hayo yanamfanya tajiri awe na chances ndogo Sanaa kiimani.

Kwa macho ya kibinadamu tajiri anaonekana kama mtu muhimu Sanaa ila kwa Mungu wote ni sawa tu.

Ila huyo Mchungaji anapenda pesa na kuna msharika hapo kaanisaani anapesa na ni mtu wake wa karibu anamsaafisha.
 
Huu ndio ufanatic usio na maana.
Ulihudhuria mahubiri au mdio unajibu kutokana na masimulizi ya jf?

Msiwe wahukumu wasiokuwa na maana yoyote.
Mahubiri mtu aweza kutoa mfano tu kama Yesu alivyotoa mifano ili aeleqeke.
Katika kutoa mfano wewe unajenga hoja hapo hapo.

Unaukumbuka ule mfano akioutoa Yesu kumwelezea yule mtu aliajiriwa katika kuposha kwa riba?
Yesu akasema alipopata habari za kufukuzwa kwake kazi akawaendea wadaiwa na kuwaambia wqpunguze kiwango cha pesa wanazodaiwa? Yaani wamdanganye mwenye kampuni ya ukopeahaji?
Unakumbuka Yesu alimsifia kwa kutumia akili kujipatanisha na wqtu ili arudipo mtaqni akubalike?

Na akasifia kuwa wana giza wana akili kuliko wana wanuru?
Hivi Kimaro angetoa mfano ule si ungemlaqni kabisa?

Mkuu huna hoja na una ulokole flani wa mapokeo..
Pole
Umeongea vema sana mkuu. Nilichogundua ni kwamba watu wengi wanaotoa maoni hasi humu wana umbumbumbu wa kutosha kuhusu neno la Mungu. Wangekuwa na uelewa wala wasingehoji madini aliyotema Mch Dr Kimaro bali wangemshukuru kwa kuwa na karama ya kufundisha neno la Mungu kwa mifano halisi ya kipindi tulichopo kama alivyofanya Bwana wetu Yesu Kristo wakati akihubiri injili kule Galilaya na maeneo mengine ya nchi.

Tuwasaemehe bure wale wote walioshindwa kumuelewa Dr kimaro kwani sio wao bali ni uelewa wao mdogo uliochanganyika na nguvu za giza ndio unawafanya wasimuelewe moja kwa moja kuhusu mafundisho yake.
 
Kama Petro hatakiwi kudhalilishwa kama unavyodai ambacho ni ujinga basi isingeelezewa kwenye biblia tunazosoma. Wapi imesema kuwa Mchungaji kamuhukumu petro? Au una maujinga yako tu kichwani?

Ni ukweli pia tajiri ndo aliyeenda kuomba kuuhifadhi mwili wa Yesu na sio kina Petro. Hivyo mchungaji Kimaro yuko sahihi kama una jambo nae litafute kwenye hoja nyingine sio hapo

Acha kutetea makosa. Mchungaji kachemka Mara ya pili, nadhani hajajufunza.
 
Pesa/ Mali/Wenye mali, haya mambo ndo yanalitesa kanisa la sasa.... ndomana walifukuzana kila mmoja akaanza kudai miradi ni yake..... warudi enzi za kina Elisha hawakufagilia hayo mambo...
Hatasijakuelewa, unazungumzia Kanisa lipi? Nani waliofukuzana wakadai mali? Mimi nazungumzia Kanisa la Kristo.
 
Ukiwa na akili ndogo kama mbegu ya hardali huwezi kumuelewa Mch Dr Kimaro. Muombe Mungu akupe hekima uelewe madini anayotema Dr Kimaro.
Kama kumuelewa ni kugumu hivyo, basi hafai. Mchungaji mzuri ni yule anayeeleweka vizuri na kila mtu, na hasababishi taharuki kwa mahubiri yake.
 
Ni ngumu sana kuwa tajiri bila kuua, kudhulumu na kuiba.

Yote hayo yanamfanya tajiri awe na chances ndogo Sanaa kiimani.

Kwa macho ya kibinadamu tajiri anaonekana kama mtu muhimu Sanaa ila kwa Mungu wote ni sawa tu.

Ila huyo Mchungaji anapenda pesa na kuna msharika hapo kaanisaani anapesa na ni mtu wake wa karibu anamsaafisha.
Siyo kweli kwamba ili uwe tajiri kuna ugumu bila kuua, kuiba au kudhulumu.
Haya ni mawazo mabaya yanayotaka utajiri wa haraka haraka.
Ni muhimu watu wajifunze kufanya kazi kwa bidii yenye akili, kwa muda unaotosha na utajiri utapatikana vivyo hivyo. Msingi wa utajiri unaweza kuanzisha wewe lakini wakaja kuonekana matajiri wanao au wajukuu.
Watu wajue kweli ili wawe huru kuhusu hali zao kiuchumi.
 
Back
Top Bottom