Mchungaji kusafisha nyota, hii imekaaje wadau?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
KUOSHWA KWA NYOTA ILIYOCHAFUKA..!

Ayubu 25:5-6
Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Andiko hili linatuonesha nyota ya Mtu inaweza Ikachafuliwa na kuonekana si safi machoni Pake katika Ulimwengu wa roho!! Hapa biblia Inatuambia thamani ya mtu huyu hushuka na kuwa kama mdudu, au mwanadamu huyu huibeba thamani ya buu.

👉 Nyota ni kitu cha Ajabu na ni siri kubwa katika ulimwengu wa Roho, Nyota hubeba hatima ya mtu na utukufu wa Mtu tangu siku anazaliwa, Nyota inauwezo wa kuvuta waliobeba baraka zako;

Ndio maana wakati Yesu amezaliwa (Mathayo 2) Ilionekana nyota yake, Ile nyota ya Bethlehem Ikiwaongoza mamajusi kupeleka fedha, manemane, dhahabu n.k kwa mtoto Yesu, Hivyo kwa kifupi nyota yako Inatakiwa Iwavute waliobeba baraka zako ukutane nao. Lakini nyota ikiwa imechafuliwa haiwezi onekana na waliobeba mibaraka yako.

Nyota silaha, Biblia Inasema
Waamuzi 5:20
Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.

Andiko hili linaonesha Iko vita nyota zinapigana katika ulimwengu wa roho, kama nyota yako ni dhaifu...basi huwezi ona matokeo kwa chochote Kile unafanya: Hivyo basi chukua hatua ya Imani ufike KWENYE IBADA JUMATANO YA KESHO, Kwa Msaada wa Roho Tutaosha nyota yako Kwa Damu ya Yesu. Prophet Martin na Prophet Malisa katika madhabahu Moja....! WOTE MNAKARIBISHWA.
 
Bora Kazi ikiwa ni kusafisha tu,
Na Kama imechukuliwa kabisa, hapo napo nini kifanyike kuirudisha?
Na ipi ni Ishara Wazi kwamba sasa inawezekana nyota yangu ni Chafu/Imechafuliwa au Imechukuliwa.
 
KUOSHWA KWA NYOTA ILIYOCHAFUKA..!

Ayubu 25:5-6
Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Andiko hili linatuonesha nyota ya Mtu inaweza Ikachafuliwa na kuonekana si safi machoni Pake katika Ulimwengu wa roho!! Hapa biblia Inatuambia thamani ya mtu huyu hushuka na kuwa kama mdudu, au mwanadamu huyu huibeba thamani ya buu.
Mkuu unataka kuingia ulimwengu wa roho kwa gia isiyo.
Katika ulimwengu wa roho pande ziko mbili tu.
Upande mwema na upande mbaya.

Na pande zote zina mapandikizi duniani.
Ndiyo maana ukimwamini Kristo umetawala upande ule mbaya pamoja na maajenti wao.
Ati nyota, maajenti wabaya wa yule mwovu ni wajanja sana, wanataka kukuingiza katika unajimu wa yafuatayo ilhali wao wenyewe hawajui hatma yao.
Na hao maajenti mbele ya Kristo hupotea kama vile hawapo kwa kuogopa yanayowasibu.

Kaa upande mwema, wa Kristo, na uwe na imani.
Hakuna cha nyota wala nini.
Kuwa na uhakika kwa yajayo.

Waebrania 11:1​

Imani​

11 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona.
 
NAmshangaa anayetofautisha dini na mizimu/ imani za the so called za kichawi.

Kuna makanisa yanaanzishwa baada ya kuzika mifupa ya viongozi wao, kuna makanisa wana maji, mafuta etc, bila kusahau na mashehe. Hapo kilichobadilika ni kwamba dini imehalalishwa psychologically against huo uchawi.

Fikiria unakataa kumuita mwanao koku unamuita wolfgang tofauti yake ni nini🙄😅😅😅

Nashauri katiba pendekezwa iunganiahe dini na uchawi ziwe na kurugenzi pale MoHA😂😂
 
KUOSHWA KWA NYOTA ILIYOCHAFUKA..!

Ayubu 25:5-6
Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Andiko hili linatuonesha nyota ya Mtu inaweza Ikachafuliwa na kuonekana si safi machoni Pake katika Ulimwengu wa roho!! Hapa biblia Inatuambia thamani ya mtu huyu hushuka na kuwa kama mdudu, au mwanadamu huyu huibeba thamani ya buu.
UNAPOTOSHA,UMECHOMOKA NA KAANDIKO KAMOJA TU UNAANZA KUBWABWAJA.SOMA SURA NZIMA ELEWA KILICHOLUWA KINAZUNGUMZIWA NI NINI.TUMECHOKA KUDANGANYWA NA MAGUNDISHO YA MTU KUJITUNGIA VITU KICHWANI
 
E! Umekuwa mhubiri tangu lini? Kumbe unaamini juu ya nyota
 
NAmshangaa anayetofautisha dini na mizimu/ imani za the so called za kichawi.
Kuna makanisa yanaanzishwa baada ya kuzika mifupa ya viongozi wao, kuna makanisa wana maji, mafuta etc, bila kusahau na mashehe. Hapo kilichobadilika ni kwamba dini imehalalishwa psychologically against huo uchawi. Fikiria unakataa kumuita mwanao koku unamuita wolfgang tofauti yake ni nini🙄😅😅😅

Nashauri katiba pendekezwa iunganiahe dini na uchawi ziwe na kurugenzi pale MoHA😂😂
Imetisha aisee... hajambo MCHAWI Karaba lakini?
 
Ndio maana wakati Yesu amezaliwa (Mathayo 2) Ilionekana nyota yake, Ile nyota ya Bethlehem Ikiwaongoza mamajusi kupeleka fedha, manemane, dhahabu n.k kwa mtoto Yesu, Hivyo kwa kifupi nyota yako Inatakiwa Iwavute waliobeba baraka zako ukutane nao. Lakini nyota ikiwa imechafuliwa haiwezi onekana na waliobeba mibaraka yako.
Herode akaitamani
 
Mchungaji kanisani kwetu akiwa kwenye ibada mwezi uliopita👇😁😁😁
XgAEiV7K.jpeg
 
KUOSHWA KWA NYOTA ILIYOCHAFUKA..!

Ayubu 25:5-6
Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Andiko hili linatuonesha nyota ya Mtu inaweza Ikachafuliwa na kuonekana si safi machoni Pake katika Ulimwengu wa roho!! Hapa biblia Inatuambia thamani ya mtu huyu hushuka na kuwa kama mdudu, au mwanadamu huyu huibeba thamani ya buu.

👉 Nyota ni kitu cha Ajabu na ni siri kubwa katika ulimwengu wa Roho, Nyota hubeba hatima ya mtu na utukufu wa Mtu tangu siku anazaliwa, Nyota inauwezo wa kuvuta waliobeba baraka zako;

Ndio maana wakati Yesu amezaliwa (Mathayo 2) Ilionekana nyota yake, Ile nyota ya Bethlehem Ikiwaongoza mamajusi kupeleka fedha, manemane, dhahabu n.k kwa mtoto Yesu, Hivyo kwa kifupi nyota yako Inatakiwa Iwavute waliobeba baraka zako ukutane nao. Lakini nyota ikiwa imechafuliwa haiwezi onekana na waliobeba mibaraka yako.

Nyota silaha, Biblia Inasema
Waamuzi 5:20
Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.

Andiko hili linaonesha Iko vita nyota zinapigana katika ulimwengu wa roho, kama nyota yako ni dhaifu...basi huwezi ona matokeo kwa chochote Kile unafanya: Hivyo basi chukua hatua ya Imani ufike KWENYE IBADA JUMATANO YA KESHO, Kwa Msaada wa Roho Tutaosha nyota yako Kwa Damu ya Yesu. Prophet Martin na Prophet Malisa katika madhabahu Moja....! WOTE MNAKARIBISHWA.
Tafsiri ya uongo hivyo hayo mafundisho ni batili na potofu
 
Back
Top Bottom