Mchungaji Lusekelo: Kwa mujibu wa Biblia mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa, hao wanaohoji baadae ni wavuta bangi

Huyu ni Mchugaji au dalali wa dini?
Hapa ndipo mkristo ulipopewa mtihani mkubwa sana..

Wanafunzi wakamuuliza Yesu, Je Mwalimu tutawajuaje hao manabii wa uongo.???

Sasa ewe mkristo rudi tena kwenye biblia yako soma soma soma.... kwa msaada wa roho mtakatifu nina hakika utapewa mwangozo.. , nyakati hizi ni za hatari..tunaelekea si kuzuri...tusipokuwa makini tutapotea.
 
Hana akili sawa sawa huyo dingi.
Anasahau kabisa kuwa Yesu Kristo alipingana na mkuu wa nchi ya Israeli (Pilato na Herode) ndio maana hukumu ya kusubiriwa ikatolewa.

Pia anasahau kabisa harakati zote za kuhubiri ukombozi zilizofanywa na Musa, Joshua, Eliya, Elisha, Petro, Paulo nk zilikuwa kinyume na amri na kauli za wakuu wa nchi zile walizokuwepo.
 
Mchungaji Lusekelo amesema yeye ni miongoni mwa wachungaji bora 10 barani Afrika hivyo anapoongea jambo wananchi ni lazima wamuelewe.

Lusekelo anasema Rais Magufuli ameitikisa dunia kwa namna alivyoweza kudhibiti Corona, kadhalika wale walioongea baada tu ya Rais kuongea na wananchi ni wavuta bangi.

Lusekelo anasisitiza kuwa mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa kinachofuatia ni utekelezaji na yule mtu anayesubiri Rais aongee ili yeye amjibu huyo ni mvuta bangi. Mkuu wa nchi anaheshimiwa na kuenziwa kwa mujibu wa Biblia.

Mchungaji Lusekelo alikuwa akichangia mada kuhusu kudhibitiwa kwa Corona nchini na yeye alielezea kwa upande wa Wakristo na upande wa waislamu alikuwepo shehe wa mkoa wa Dsm Alhad Mussa Salum.

Mjadala huo uliendeshwa na Channel Ten tv.

Maendeleo hayana vyama!

Mchungaji Lusekelo ndio mvuta bangi wala Hana sifa za kuwa Kiongozi wa kiroho.....Nonsense!
 
Mzee wa upako asilaumiwe kwa lolote.

Hapo anaesema sio yeye ni pombe.

Hapo alipo anaongea huku chini hapo kaweka glass ya smonof vodka au konyagi kubwa anapiga taratibu.

Mzee wa upako muda wote amelewa hivyo huna sababu ya kumlaumu.
 
Lakini havuti bangi kama yule anayehoji bila utaratibu!
 
Alikuwa amepiga bapa ngapi kabla ya kuongea huyu mlevi
 
Kama ni top ten LA wanywa BAPA sawa nadhani yupo sahihi vinginevyo atakuwa amepiga cha Jamaica.
 
Mchungaji Lusekelo amesema yeye ni miongoni mwa wachungaji bora 10 barani Afrika hivyo anapoongea jambo wananchi ni lazima wamuelewe.

Lusekelo anasema Rais Magufuli ameitikisa dunia kwa namna alivyoweza kudhibiti Corona, kadhalika wale walioongea baada tu ya Rais kuongea na wananchi ni wavuta bangi.

Lusekelo anasisitiza kuwa mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa kinachofuatia ni utekelezaji na yule mtu anayesubiri Rais aongee ili yeye amjibu huyo ni mvuta bangi. Mkuu wa nchi anaheshimiwa na kuenziwa kwa mujibu wa Biblia.

Mchungaji Lusekelo alikuwa akichangia mada kuhusu kudhibitiwa kwa Corona nchini na yeye alielezea kwa upande wa Wakristo na upande wa waislamu alikuwepo shehe wa mkoa wa Dsm Alhad Mussa Salum.

Mjadala huo uliendeshwa na Channel Ten tv.

Maendeleo hayana vyama!
Lusekelo ni mchungaji au anajiita mchungaji? Tukumbuke kuwa tapeli ana uwezo wa kujiita jina lolote analoona linaweza kusaidia kutimiza azma yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchungaji Lusekelo amesema yeye ni miongoni mwa wachungaji bora 10 barani Afrika hivyo anapoongea jambo wananchi ni lazima wamuelewe.

Lusekelo anasema Rais Magufuli ameitikisa dunia kwa namna alivyoweza kudhibiti Corona, kadhalika wale walioongea baada tu ya Rais kuongea na wananchi ni wavuta bangi.

Lusekelo anasisitiza kuwa mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa kinachofuatia ni utekelezaji na yule mtu anayesubiri Rais aongee ili yeye amjibu huyo ni mvuta bangi. Mkuu wa nchi anaheshimiwa na kuenziwa kwa mujibu wa Biblia.

Mchungaji Lusekelo alikuwa akichangia mada kuhusu kudhibitiwa kwa Corona nchini na yeye alielezea kwa upande wa Wakristo na upande wa waislamu alikuwepo shehe wa mkoa wa Dsm Alhad Mussa Salum.

Mjadala huo uliendeshwa na Channel Ten tv.

Maendeleo hayana vyama!
Lazima chadema watapinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mashaka na uelewa wake kuhusu Biblia

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa nashangaa sana, sijui wanadamu tumeumbwa namna gani, Lusekelo na Gwajima nao wana wafuasi wa imani ya kikristo. Wana haki ya kuwa na wafuasi kwenye mambo mengine lakini siyo kwenye imani ya kikristo. Sidhani hawa wawili kama kuna wakati wowote wamewahi kuwa wakristo, achiliambali uchungaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom