Mchungaji Lusekelo: Kwa mujibu wa Biblia mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa, hao wanaohoji baadae ni wavuta bangi

Mchungaji Lusekelo: Kwa mujibu wa Biblia mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa, hao wanaohoji baadae ni wavuta bangi

Watakao mpinga na kumtukana Mzee wa Upako ni Mapaganitu. Wasiojua maandiko. Alichosema Mzee wa Upako ndio ukweli wa Neno LA Mungu.

Tena neno LA Mungu limesema Amelaaniwa MTU Anae Mlaani kiongozi wake.
Hapa ndipo mkristo ulipopewa mtihani mkubwa sana..

Wanafunzi wakamuuliza Yesu, Je Mwalimu tutawajuaje hao manabii wa uongo.???

Sasa ewe mkristo rudi tena kwenye biblia yako soma soma soma.... kwa msaada wa roho mtakatifu nina hakika utapewa mwangozo.. , nyakati hizi ni za hatari..tunaelekea si kuzuri...tusipokuwa makini tutapotea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kuskeko huwa mropokaji alafu nikama anaroho mbaya na hasira za kimkizimkizi. Maranyingi namhisi anatumia mavitu yakulefya sana itakuwa alianza kipindi ile anakula msoto mwendekeza hela mkubwa
 
Alinunuliwa kwa kuhongwa kipande cha lami so hawezi kwenda against la sivyo usajili utafutwa,Hawa Wala dezo hawana alternative ya maisha Hadi wanaondoka duniani so no lzm wawe makada tu
 
Huwa nashangaa sana, sijui wanadamu tumeumbwa namna gani, Lusekelo na Gwajima nao wana wafuasi wa imani ya kikristo. Wana haki ya kuwa na wafuasi kwenye mambo mengine lakini siyo kwenye imani ya kikristo. Sidhani hawa wawili kama kuna wakati wowote wamewahi kuwa wakristo, achiliambali uchungaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiwa mfanyabiashara ya dini,mwanamuziki, kibiashara si vizuri kujionyesha uko upande gani hii ibakie tu moyoni mwako
 
Mchungaji Lusekelo amesema yeye ni miongoni mwa wachungaji bora 10 barani Afrika hivyo anapoongea jambo wananchi ni lazima wamuelewe.

Lusekelo anasema Rais Magufuli ameitikisa dunia kwa namna alivyoweza kudhibiti Corona, kadhalika wale walioongea baada tu ya Rais kuongea na wananchi ni wavuta bangi.

Lusekelo anasisitiza kuwa mkuu wa nchi akishaongea mjadala unafungwa kinachofuatia ni utekelezaji na yule mtu anayesubiri Rais aongee ili yeye amjibu huyo ni mvuta bangi. Mkuu wa nchi anaheshimiwa na kuenziwa kwa mujibu wa Biblia.

Mchungaji Lusekelo alikuwa akichangia mada kuhusu kudhibitiwa kwa Corona nchini na yeye alielezea kwa upande wa Wakristo na upande wa waislamu alikuwepo shehe wa mkoa wa Dsm Alhad Mussa Salum.

Mjadala huo uliendeshwa na Channel Ten tv.

Maendeleo hayana vyama!
Bora mvuta bangi anapiga nyungu kuliko mlevi wa konyagi anaunguza maini na utumbo.
 
Hapa ndipo mkristo ulipopewa mtihani mkubwa sana..

Wanafunzi wakamuuliza Yesu, Je Mwalimu tutawajuaje hao manabii wa uongo.???

Sasa ewe mkristo rudi tena kwenye biblia yako soma soma soma.... kwa msaada wa roho mtakatifu nina hakika utapewa mwangozo.. , nyakati hizi ni za hatari..tunaelekea si kuzuri...tusipokuwa makini tutapotea.
Asante mkuu hili ni tapeli la dini
 
Back
Top Bottom