Mchungaji Lusekelo: Libya na Iraq zinajuta kuwasaliti viongozi wao Gaddafi na Sadam Hussein, watanzania msifanye makosa mtajuta!

Mchungaji Lusekelo: Libya na Iraq zinajuta kuwasaliti viongozi wao Gaddafi na Sadam Hussein, watanzania msifanye makosa mtajuta!

Magu kafika kusali kanisani kwake kutoa sadaka,tayari Lusekelo anataka na watanzania tumfanye Magu na CCM yake kuwa rais wa maisha wakati kuna nchi wamefanya zaidi ya anachokifanya Magu na bado wanaondolewa kwenye utawala na mambo yanaendelea vizuri tu.
 
Mchungaji Anthony Lusekelo amewataka watanzania kutoiga iga mambo kwani demokrasia ina maana pana.

Mzee wa Upako amesema hata Marekani demokrasia wanayoihubiri hawaiishi kwa mfano Hilarry Clinton ndiye aliyeshinda kwa wingi wa kura lakini aliyeteuliwa kuwa Rais ni Donald Trump.

Kadhalika Uingereza Waziri mkuu anapigiwa kura lakini mfalme ndiye anayempitisha.

Lusekelo amewataka watanzania wajifunze Libya na Iraq waliotupa " mbachao" kwa msala upitao na sasa wanajuta.

Source Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Yaani haoni kuwa wale viongozi ndio walisaliti wananchi wao, mfano Chemical Ali.
 
usipowaunganisha watu wako watashirikiana na adui zako kukumaliza.
Kweli kabisa..
Idi Amin Dada hakutambua hili, aliwagawa na kuwatesa wananchi wake, matokeo yake wakashirikiana na sisi Watanzania kumfurusha!
 
Wewe ya malawi hayakuhusu angalia nchi yako, amani ikipotea ndo wakwanza kufoka.
Amani inapoteaje?,kwani si unafanyika uchaguzi wananchi wanapiga kura kumchagua wampendae.
Au nyie ccm ndo mtaanzisha machafuko baada ya kupigwa chini?.
Afu unayo CV ya Mzee Wa upako kweli,ndio atushauri kweli?.
 
Mpaka hapo nyinyi mnao lalama mnaamini vipi kama tundu lissu atawaletea auheni katika maisha yenu,, fikirini kwanza kabla ya kuchukua maamuzi na katika siasa kuna maneno ya kukushawishi mwananchi a.k.a kukutongoza ili ujuwe huyo ndo mkweli kumbe akishika dolla mnaanza kusema bora na Mweshimiwa magufuli,,

Kuweni makini hii ni siasa ndugu zanguni musiamini kila anachosema huyu tundu lissu maana kwa upande wangu naona nikama mahasimu kwa hiyo hawawezi kuombeana au kusemana vizuri,,


Na huyu tundu lissu akiingia madarakani mtajuta naamini maana atafanya kama kulipiza kisasi kwa yote yaliyo fanyika katika utawala wa mweshimiwa.
HAPO NDO MTAJUA KWANINI SHUKA HALINA MFUKO?

Mwenye masikio na asikie,
Nawatakia uchaguzi mwema.
 
Amani inapoteaje?,kwani si unafanyika uchaguzi wananchi wanapiga kura kumchagua wampendae.
Au nyie ccm ndo mtaanzisha machafuko baada ya kupigwa chini?.
Afu unayo CV ya Mzee Wa upako kweli,ndio atushauri kweli?.

Maono ya mzee hayo mkuu
 
Alikuwa akibwabwaja tu
Muulize huyo mtu wako

Anajua mfumo wa kura za Marekani ukoje?

Muulize pia ni Uingereza gani Waziri mkuu anapitishwa na Mfalme?

Mwisho muulize tutajuta nini??? Kwa hiyo yeye anamfananisha Magufuli na Saddam Hussein??? Anazijua sifa za Saddam Hussein??? Je anamfananisha Magufuli na Gaddafi? Anazijua sifa za Gaddafi??? Ametumia vigezo gani kumfananisha Magufuli na hawa? Au amekaririshwa tu??[emoji23][emoji23]
 
Mchungaji Anthony Lusekelo amewataka Watanzania kutoiga iga mambo kwani demokrasia ina maana pana.

Mzee wa Upako amesema hata Marekani demokrasia wanayoihubiri hawaiishi kwa mfano Hilarry Clinton ndiye aliyeshinda kwa wingi wa kura lakini aliyeteuliwa kuwa Rais ni Donald Trump.

Kadhalika Uingereza Waziri Mkuu anapigiwa kura lakini mfalme ndiye anayempitisha.

Lusekelo amewataka Watanzania wajifunze Libya na Iraq waliotupa " mbachao" kwa msala upitao na sasa wanajuta.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Haya ni mavi ya kale
 
Back
Top Bottom