PostGE2025 Mchungaji Mashimo ahoji, Jaji Warioba amepata wapi takwimu za waliofariki?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakuu baada ya Jaji Warioba kueleza kuwa watu waliofariki Oktoba wakati wa maandamano ni wengi kuliko waliofariki kwenye vita ya Kagera Mchungaji Daudi Mashimo ameibuka na kohoji ni wapi Jaji Warioba alipozipata takwimu hizo?

"Watu waliokufa mpaka sasa Tanzania hakuna mwenye takwimu kamili tunasubiri mamlaka ambazo tayari zimepewa jukumu la kuchunguza ili kubaini.

Hata mzee wangu Warioba sijui sensa amefanyia wapi? Lakini siwezi kuunga mkono maneno yake aliyoyasema mara ya mwisho" - Mch. Mashimo

Your browser is not able to display this video.
 
Sawa sawa na jina lake,ametoboka mashimo.ni wakati sasa wa kumnyima sadaka pale kituo cha mabasi mbezi mwisho,arudi achunge kanisa lake.
 
Mchungaji yuko sahihi. Warioba utu uzima unamsumbua.
 

Mtu anaitwa mashimo!! Naye ni wa kumshangaa akitoa maswali yanayoashiria mashimo akilini mwake?
 
mzee Warioba ni kama babu wa Loliondo tu sasa hivi,

eti nae kaoteshwa takwimu dah
 
Mchungaji Mashimo ahoji, Jaji Warioba amepata wapi takwimu za waliofariki?
Ni wa wapi huyo chawa?

Anamchukulia poa mzee aliyewahi kuwa jaji, waziri mkuu, makamo wa rais, nk, tena sio wa mchongo kama hawa wa sasa!

Ungetuwekea hapa clip yake
 
Uganda walikufa askari kati ya 500 na 1000.

Warioba kaongelea kuhusu namba zinazoongelewa waliokufa 25/10 ambazo ni zaidi ya vijana elfu 10.

Hata kwa kuangalia misiba tu kwa vyovyote ni zaidi ya vijana elfu 10 wameuawa.
 
Huyo mashimo anamfahamu kwanza Mzee Warioba ni nani nchi hii?
 
Mbona jibu ni jepesi tu kama siyo wengi kwanini imefichwa miili na idadi ya waliokufa....kama walio uliwa ni mia kadhaa mbona miili imepotezwa .. serikali isingekuwa na kigugumizi kama walio uliwa ni wachache ....kigugumizi na kufichwa kwa maiti ni ushahidi tosha kuwa wamekufa maelfu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…