Unajua Mimi nalaumu nini? Hawa wapigania Uhuru wa nchi za Africa Kwa kuingia mkenge wa demokrasia ya vyama vingi ni Bora tungebaki na chama kimoja tu halafu tuendeshwe Kwa mkono wa chuma.
Kwa sababu hii ngozi nyeusi hatuna uvumilivu tukishindwa kwenye box la kura hatukubali matokeo. Hakuna uchaguzi wapinzani walikubali matokeo wao kila mwaka wameibiwa,
Wenzenu Wana watu mpaka kwenye shina huko, nyie mmeconcentrate vimiji kadhaaa tu halafu mnadhani mtaishinda CCM? Mfano uchaguzi uliopita asilimia kubwa mikoani walipiga kura kasoro Dar, Mbeya ( tena mijini tu wilaya za ndani ndani walipiga kura) Mwanza mjini na Arusha. Sasa unataka uchaguzi urudiwe Kwa kigezo kipi? Mtu WA Sumbawanga, tabora , Katavi, njombe, Iringa Dodoma Simiyu nk. Haki Yake itakuwa wapi? Acheni kuwa selfish. Tena Mimi naona Bora tumpate magufuli mwingine twende Kwa mkono wa chuma