Mchungaji Mashimo ahukumiwa kwenda jela miaka 2 na miezi 6

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
​

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Hakimu Rugemalila imemhukumu Daudi Mashimo kifungo cha miaka miwili na miezi sita jela baada ya kumkuta na hatia katika mashtaka mawili kati ya matatu yaliyokuwa yakimkabili.

Mashimo alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kuvamia na kuishi kwenye eneo la mlalamikaji, Flora Jonasi, kuharibu mali kwa makusudi, na kufanya vurugu dhidi ya Ramsoni. Mahakama ilimkuta na hatia katika mashtaka ya mawili, huku ikimuondolea shtaka la moja ambalo wamekuta hana hatia.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtuhumiwa ameshauri ndugu,jamaa na marafiki kukata rufaa ikiwa hawajaridhika na uamuzi huo.

=====

================

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mchungaji Daud Nkuba, maarufu kama Komando Mashimo au Nabii Mikaya, baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu ujenzi wa nyumba mali ya Frola Mwashaa katika eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam.

Aidha, Mahakama imemtia hatiani kwa kuingia kwa jinai katika ardhi ya Frola Mwashaa, lakini imemuachia huru katika shtaka la kutishia kwa vurugu, kwa kuwa upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha shtaka hilo bila shaka yoyote.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira, ambaye amesema upande wa mashtaka umethibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa kupitia mashahidi watano na vielelezo mbalimbali.

"Kwa shtaka la kuingia kwa jinai, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi sita, na kwa kosa la kuharibu mali, atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani," alisema Hakimu Rugemalira.
Hata hivyo, Mahakama imeamua vifungo hivyo viende kwa pamoja, hivyo Komando Mashimo atatumikia kifungo cha miaka miwili pekee.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu, aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Komando Mashimo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu, akidai ana familia inayomtegemea.

Komando Mashimo alishtakiwa kwa makosa matatu:
  1. Kuingia kwa jinai katika ardhi ya Frola Mwashaa mnamo Novemba 22, 2023, eneo la Mbezi Luis, Wilaya ya Ubungo.
  2. Kuharibu ujenzi wa nyumba ya Frola Mwashaa kinyume cha sheria.
  3. Kutishia kwa vurugu dhidi ya Ramson Vicent – shtaka hili lilikosa ushahidi wa kutosha, hivyo Mahakama ikamuachia huru.
ITV
 
Ningekua raisi mpaka sasa hao wachungaji na manabii wote wangekua gerezani kwa kosa la utapeli kwa jina la kiroho.
Hao wachungaji na mitume ni mapandikizi ya ccm...ndiyo maana unashangaa kwanini wanafanya uanithi na serikali ya samia inawachekea ....kama huyu muhuni mwampooosa huenda tayari kapachikwa usalama wa taifa
 
Wakristo ni magaidi kuna sababu gan ya kuharibu mali ya raia na kudhulumu afungwe tu wamezid ugaidi
Nimeeleewa wazi lako but huoni ukijumuisha WOTE unawakosea na wale wasiofanya matendo hayo let say mtu akaja akasema wahindu WOTE wachafu kwa sababu mmoja wao alifanya tukio chafu haiwezi KUWA Sawa kwenye jamii. Tukemee ubaya tusiwatwike WOTE ubaya isipokuwa WOTE wamebainika na kuthibitika wanafanya hivyo.
 
Hao wachungaji na mitume ni mapandikizi ya ccm...ndiyo maana unashangaa kwanini wanafanya uanithi na serikali ya samia inawachekea ....kama huyu muhuni mwampooosa huenda tayari kapachikwa usalama wa taifa
Kumbe kuna namna wana wa manipulate watu kisiasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…