The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ameibua mjadala mkali kuhusu hali ya CHADEMA, akidai kuwa chama hicho kimepoteza imani kwa wananchi na kinakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa ndani.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio cha Ebony FM mjini Iringa leo Jumamosi Machi 08, 2025, Msigwa amesema kuwa uongozi uliopita wa CHADEMA ulifanya makosa makubwa yaliyochangia kudhoofika kwa chama.
Amesisitiza kuwa chama hicho kinahitaji kuimarisha miundombinu yake kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi wowote.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Katika siasa kuna political science na applied politics, political science ni nadharia lakini applied politics ni vitendo. Ukiangalia kwenye vitendo, uongozi uliopita wa CHADEMA ulishindwa na umekiharibu chama," alisema Msigwa.
Akitilia mkazo haja ya mshikamano ndani ya chama, Msigwa alidai kuwa CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni.
Amesema, chama hakiwezi kuandaa umma kwa ajili ya uchaguzi ikiwa viongozi wake wenyewe bado hawajafikia maridhiano.
Msigwa pia amekosoa mkakati wa "No Reforms, No Election" akidai kuwa ni mbinu dhaifu isiyoweza kuleta matokeo chanya kwa chama.
Ameendelea kwa kusema kuwa badala ya kususia uchaguzi, CHADEMA ilipaswa kwanza kuimarisha miundombinu yake na kuunganisha wanachama wake kabla ya kufikiria kushindana katika uchaguzi.
"Kazi ya kwanza sio kulipeleka Jeshi barabarani kwenye vita wakati bado hujaliandaa kwenye kambi yako," alifafanua.
Kauli hii ya Msigwa inakuja wakati ambapo mijadala kuhusu mwelekeo wa CHADEMA inaendelea kushika kasi, huku chama hicho kikijaribu kujipanga kwa chaguzi zijazo. Kauli yake inazua maswali makubwa juu ya umoja wa chama na mbinu zake za kisiasa katika kipindi hiki cha mpito.