Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: CHADEMA imepoteza imani na wananchi, No Reforms, No Election ni mkakati butu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizi ndio tabia za kibongo na zinakatisha tamaa sana huyu kama bado angekuwa CHADEMA angekuwa mstari wa mbele kuiuza Strategy ya NO REFORMS NO ELECTION tena kwa jazba kubwa sasa baada ya kuondoka kwa "hasira" kageuka 360° utasema alikuwepo huko CCM tokea Uhuru.
 
Yaani huyu ndio hajitambui kabisa, hivi yeye ndio msemaji wa Chadema. Badala liongelee chama chake kutwa chadema, kweli njaa mbaya sana
 
Hili ndio zuzu la kutupwa,
Kwa watu kuuliwa kwake ni shere,
Watu kutekwa kwake ni sherehe,
watu kuenguliwa kwake ni sherehe,
Mawakala kutopewa barua za uteuzi kwake ni sherehe,
Matokeo kupinduliwa kwake ni sherehe,
Mawakala kutolewa nje ya vyumba vya kupigia kura kwake ni sherehe,
Washindi kutotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi kwake ni sherehe,
Uchaguzi kusimamiwa na makada wa ccm kwake ni sherehe

Mtu kama huyo ni kumuogopa kama ukoma japo tunajua yote hii ni njaa na uroho wa madaraka.

WATANZANIA NCHI HII NI YETU SOTE, TUPUNGUZE UNAFIKI TUWEZE KUSONGA MBELE KAMA TAIFA, HUU UNAFIKI MNAOUENDEKEZA UNAPELEKEA KUPATA VIONGOZI WA HOVYO.
upuuzi mwingine huu hapa kaandika mpuuzi mmoja
 
Hizi ndio tabia za kibongo na zinakatisha tamaa sana huyu kama bado angekuwa CHADEMA angekuwa mstari wa mbele kuiuza Strategy ya NO REFORMS NO ELECTION tena kwa jazba kubwa sasa baada ya kuondoka kwa "hasira" kageuka 360° utasema alikuwepo huko CCM tokea Uhuru.
siasa ni sayansi
 
Hili ndio zuzu la kutupwa,
Kwa watu kuuliwa kwake ni shere,
Watu kutekwa kwake ni sherehe,
watu kuenguliwa kwake ni sherehe,
Mawakala kutopewa barua za uteuzi kwake ni sherehe,
Matokeo kupinduliwa kwake ni sherehe,
Mawakala kutolewa nje ya vyumba vya kupigia kura kwake ni sherehe,
Washindi kutotangazwa na wasimamizi wa uchaguzi kwake ni sherehe,
Uchaguzi kusimamiwa na makada wa ccm kwake ni sherehe

Mtu kama huyo ni kumuogopa kama ukoma japo tunajua yote hii ni njaa na uroho wa madaraka.

WATANZANIA NCHI HII NI YETU SOTE, TUPUNGUZE UNAFIKI TUWEZE KUSONGA MBELE KAMA TAIFA, HUU UNAFIKI MNAOUENDEKEZA UNAPELEKEA KUPATA VIONGOZI WA HOVYO.
Hizo ni hoja ambazo ziinarekebishwa kwa kukaa meza moja na wenye nguvu ili kuzijadili.sasa chadema wamekuja na utoto wakususia uchaguzi hapo wanakua wanamkomoa nani?.Kwasababu usidanganyike kwamba Ccm na serikali inaogopa hayo matamko.Ukipunguza mihemko utamwelewa msigwa.
 
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM ameibua mjadala mkali kuhusu hali ya CHADEMA, akidai kuwa chama hicho kimepoteza imani kwa wananchi na kinakabiliwa na mgawanyiko mkubwa wa ndani.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio cha Ebony FM mjini Iringa leo Jumamosi Machi 08, 2025, Msigwa amesema kuwa uongozi uliopita wa CHADEMA ulifanya makosa makubwa yaliyochangia kudhoofika kwa chama.

Amesisitiza kuwa chama hicho kinahitaji kuimarisha miundombinu yake kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi wowote.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Katika siasa kuna political science na applied politics, political science ni nadharia lakini applied politics ni vitendo. Ukiangalia kwenye vitendo, uongozi uliopita wa CHADEMA ulishindwa na umekiharibu chama," alisema Msigwa.

Akitilia mkazo haja ya mshikamano ndani ya chama, Msigwa alidai kuwa CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni.

Amesema, chama hakiwezi kuandaa umma kwa ajili ya uchaguzi ikiwa viongozi wake wenyewe bado hawajafikia maridhiano.

Msigwa pia amekosoa mkakati wa "No Reforms, No Election" akidai kuwa ni mbinu dhaifu isiyoweza kuleta matokeo chanya kwa chama.

Ameendelea kwa kusema kuwa badala ya kususia uchaguzi, CHADEMA ilipaswa kwanza kuimarisha miundombinu yake na kuunganisha wanachama wake kabla ya kufikiria kushindana katika uchaguzi.

"Kazi ya kwanza sio kulipeleka Jeshi barabarani kwenye vita wakati bado hujaliandaa kwenye kambi yako," alifafanua.

Kauli hii ya Msigwa inakuja wakati ambapo mijadala kuhusu mwelekeo wa CHADEMA inaendelea kushika kasi, huku chama hicho kikijaribu kujipanga kwa chaguzi zijazo. Kauli yake inazua maswali makubwa juu ya umoja wa chama na mbinu zake za kisiasa katika kipindi hiki cha mpito.

View attachment 3263432
chadema kasahau nini mla umbwa huyu
 
Huyu Mbena amekonda, kawa mweusi na sura haina nuru kabisa kama alivyokuwa CDM. Hana uhuru wa mawazo hata mawasiliano yake yameshikiliwa na jabali la utapeli wa kisiasa kutoka Kiegea.

Narudia hana uhuru wa kupanga mipango yake binafsi wala kuwasiliana na rafiki wa upande wa pili na huenda akaishia kuchanganyikiwa muda sio mrefu
 
Back
Top Bottom