Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kahamia CCM katika kipindi kibaya

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kahamia CCM katika kipindi kibaya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Jul 6, 2016
Posts
14
Reaction score
15
Nathubutu kusema Msigwa ameshindwa kusoma nyakati, hatukatai kwamba CHADEMA hakuna mapungufu lakini sioni kama Matatizo anayoyasema ndio chanzo cha yeye kuhama. Watu wenye macho matatu wanajua ni uchu wa madaraka tu, kwa sababu shida ilianza baada ya kushindwa na Sugu kwenye Uchaguzi Kanda ya kusini.

Kwanini nasema kahimia CCM kipindi kibaya. CCM sasa hivi inaongozwa na Mwenyekiti ambaye anaamini kwenye misingi ya Demokrasia ya kweli, ni kiongozi anayependa Vyama vya upinzani viwe imara ili kuweka upinzani wa kweli kwenye chama chake na hana mpango wa kuvibomoa Vyama vya upinzani, pia ni Kiongozi ambaye anaamini katika misingi yake, anaweza akasemwa vibaya lakini yeye anasonga mbele, pia ni Kiongozi ambaye hana visasi na mtu.

Ndio maana Msigwa kama amehamia CCM kwa ajili ya kupata Teuzi hapa kafeli labda ingekuwa kipindi hicho.

Pia soma Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
 
CCM saizi inaongozwa na Mwenyekiti ambaye anaamini kwenye misingi ya Demokrasia ya kweli,ni kiongozi anayependa Vyama vya upinzani viwe imara ili kuweka upinzani wa kweli kwenye chama chake na hana mpango wa kuvibomoa Vyama vya upinzani,
a very very shallow analysis. chawa wa ajabu kweli kweli wewe
 
Kule ataishi kama mtumwa!! Juzi press imemshinda hadi akawa anapenyezewa ki karatasi cha maneno wanayotaka ayaseme!!

Maisha magumu sana huyu bingwa kayachagua.
 
Alikosea wakati wa Jiwe! Bahati aliyoipata kwa Jiwe hawezi kuipata tena.
Anyway wanaweza kumwonjesha udc au u RAS then mwakani baada ya uchaguzi 2025 wakamumwaga!
 
upinzani maisha magumu. inataka roho ngumu huko
 
Alikosea wakati wa Jiwe! Bahati aliyoipata kwa Jiwe hawezi kuipata tena.
Anyway wanaweza kumwonjesha udc au u RAS then mwakani baada ya uchaguzi 2025 wakamumwaga!
si atapewa kuwa RC
 
CHADEMA ni genge la waharakati na waropokaji, ni watu wenye "uchu wa madaraka" tu.

Hawana sera zinaozoleweka, yani kiukweli, hawana sera.

Karbu Msigwa.
 
Tatizo kubwa ni kwamba wanasiasa wa kiafrika wanaichukulia siasa kama njia ya mkato ya kujitafutia maisha badala ya lengo la awali ambayo ni utumishi kwa umma.

Fikra hiyo ya wanasiasa wa kiafrika ndio chanzo cha waafrika kutokuamini katika kuwajibika kwa kujiuzulu pale wanapotakiwa kufanya hivyo.

Hii hulka ya waafrika kuchukulia siasa kama njia ya mkato ya kujitafutia maisha ndio chanzo cha watu wa bara hili kuwa maskini wa kutupwa pamoja na kwamba bara lenyewe lina rasilimali lukuki.
 
Back
Top Bottom