Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kwenda CCM ni moja kati ya 'usajili' mbaya kuwahi kufanywa na vyama vya siasa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa kwenda CCM ni moja kati ya 'usajili' mbaya kuwahi kufanywa na vyama vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nehemia Kilave ninakuita Ndugu yangu
Nadhani kuna namna fulani dhana ya Siasa kidogo huijui.

Kwanza kabisa Chama cha Siasa huwa kinajenga Ideology ambayo huwa inaaminiwa na wafuasi wake. Kama zilivyo dini, siasa nazo ni mfumo wa namna hiyo.

Mchungaji Msigwa siyo lengo pekee la kuongeza wafuasi ndani ya CCM bali pia kuongeza wigo wa watu wanaosikiliza sera za CCM.

Kumbuka mpaka sasa kunahoja ambazo Msigwa amezitoa ambazo zimezalisha attention kwenye Taifa. Hata wale waliokuwa hawamfuatilii MSigwa kila mkutano akienda watataka wasikie anaongea nini..

CCM haihitaji watu wote ndani ya CHADEMA bali inahiaji baadhi ya waliomo ndani ya Chama hicho wanaomuunga mkono Msingwa.

CCM tayari ipo na wanachama Hai zaidi ya 15,000,000.
Peter Msigwa 😂😂😂😂😂
 
Kwa sasa Tundu Lissu ndiye mwanasiasa pekee ambae kuhama kwake sehemu kunaweza hama na watu , sababu nyuma kuna watu wengi sana ambao ni wafuasi wake na wana imani na yeye.

CCM wamemchukua Msigwa kama mtaji ndio maana anapewa airtime kwenye mikutano.

Kiuhalisia sasa ni kwamba Mchungaji imani na mvuto kwa wana CDM ulishapotea hata ushindani uliotokea kwenye uchaguzi wa kanda ni kwa wajumbe wanakosa mtu mwingine sahihi katika hiyo nafasi ila wote ni wabovu.

Lakini pia ni bad timing sababu 1. Unapokea mtu tayari ameshindwa uchaguzi kwanini hakuhamia kabla ya Uchaguzi wa kanda?

2. Msigwa ilibidi apokelewe CCM kama mwanachama wa kawaida halafu aanze kupewa time jukwaani taaratibu hasa kuelekea 2025 - sasa watu wanamchulia kama msaliti fulani na mroho wa Madaraka.

Kwangu mimi huu ni usajili mbovu kuwahi kufanywa na vyama.

Soma Pia:

- Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM


- Kuelekea 2025 - Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Chief Odemba na Peter Msigwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa
Jamaa alifikiri ni maarufu. Kumbe hakuna aliye na umaarufu. Chadema ndio inawapa umaarufu. Nje ya chadema wote ni wananchi tu
 
Back
Top Bottom