Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Maranja anaishi kwa kutegemea kuzururazurura kwenye korido za CHADEMA na kulamba viatu vya Mbowe

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Maranja anaishi kwa kutegemea kuzururazurura kwenye korido za CHADEMA na kulamba viatu vya Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama swala la kutokuwa na ukomo ingekuwa ni tatizo basi chama kisingesajiriwa. Demokrasia ni pamoja na kufata katiba
Unaweza kufuata katiba lakini hiyo katiba Ikawa na mapungufu Moja kati ya pungufu katika katiba ya CHADEMA ni kutoweka ukomo katika cheo Cha Mwenyekiti
Mfano tu sisi tunaolilia katiba mpya kwani Nchi haina katiba? Katiba ipo ila tunaona baadhi ya maneno Yana mapungufu na kwa hili lazima Chadema wajirekebishe waludishe kipengere Cha ukomo kama ilivyokuwa mwanzo

Na kwa utaratibu huu atatokea mwingine atarekebisha katiba na kujiita Mwenyekiti wa milele
 
Msigwa athibitiwe kabla hajaharibu taswira ya chama zaidi. Akubali kushindwa na si kuanza kurusha shombo kwa wenzake
Kamati ya nidhamu Chadema imuite athibitishe hayo madai kuwa Maranja anaishi Kwa kulamba miguu ya Mbowe tuhuma nzito hizo Kwa Mbowe na Maranja

Hiyo ni defamation case mawili Mbowe au Maranja waamfungukie kesi Msigwa au hatua za kichama zichukuliwe dhidi ya Msigwa

Lakini napendekeza achukuliwe hatua za kichama
 
Safi, sasa kama katiba yao ambayo inasema hivyo na iko wazi,kwanini unaumia ili hali wanafuata katiba yao? Katiba haina uko na ilikuwa hivyo toka mwanzo,sasa shida ni nini hapo?
Haikuwa hovyo toka mwanzo ila baada ya Mbowe kumaliza vipindi viwili ndipo katiba ilipobadilishwa kinyemela
Pia Chadema sio chama chao ni chama Cha Umma(ndio maana wanapokea ruzuku) na tunaimani kinaweza kuwa mbadala wa CCM siku Moja Sasa yale mabaya tunayolalamika yanafanywa na chama tawala tukiyaona yanafanywa na kikubwa Cha Upinzani sisi Wananchi tunashindwa kutofautisha yupi Bora na ndipo ule usemi wa kiswahili zimwi likujualo...,.....unapotamali
 
Kujenga chama unadhani ni kazi rahisi? Muulize Zitto Kabwe atakwambia.

Walafi wanataka ready made, Mbowe ameshasurubika amewekwa jela amepewa kesi za ugaidi leo kirahisi tu awaachie uongozi mchwa waje kula pesa hata mimi siwezi kufanya ujinga huo.

Mbowe kamatia hapohapo wewe ndio Putin wetu endelea kuwanyoosha.
Hata mimi simwachii yeyote, ila kama wanachama wakinichoka basi nasepa
 
down,Chawa wa Mwenyekiti kila chama wapo,Mbona Ndugai Uvccm walimtukana kwa kuongea ukweli kuhusu mwenyekiti mpk akajiuzulu usipka
Chadema inapaswa kujinasibu kwa mazuri na siyo kujilingangdnisha na mabaya ya ccm.
 
Ni mtifuano mkali Ukurasani X Kati ya Mchungaji Msigwa na Chawa wa Mbowe Martin Maranja.

Mashambuliano hayo, kebehi, kejeli na kudharauliana kunaonyesha jinsi CHADEMA ilivyosheheni wahuni.

Chonde chonde Katibu mkuu Mnyika hebu ingilia kati nidhamu na kuheshimiwa a kurejee ndani ya chama

Ni wazi kuna ugomvi mkubwa sana Kati ya Mchungaji Msigwa na Mwenyekiti Mbowe.

Mchungaji Msigwa asikilizwe kabla hajaanza kutoa siri za michango ya Nairobi hospital.

Mungu wa mbinguni inusuru CHADEMA.

Kwako Lucas 😂🔥
Msigwa banana na Mbowe mpaka kieleweke. Ni zamu ya Mbowe kungoka mwaka huu. Jeshi lipo vizuri. Ni lazima kuisambaratisha ngome ya kaskazini ili CHADEMA ipumue.

Wamegusa pabaya! Msigwa komaaaa, tupo nyuma yako mpaka kieleweke.
 
Ni mtifuano mkali Ukurasani X Kati ya Mchungaji Msigwa na Chawa wa Mbowe Martin Maranja.

Mashambuliano hayo, kebehi, kejeli na kudharauliana kunaonyesha jinsi CHADEMA ilivyosheheni wahuni.

Chonde chonde Katibu mkuu Mnyika hebu ingilia kati nidhamu na kuheshimiwa a kurejee ndani ya chama

Ni wazi kuna ugomvi mkubwa sana Kati ya Mchungaji Msigwa na Mwenyekiti Mbowe.

Mchungaji Msigwa asikilizwe kabla hajaanza kutoa siri za michango ya Nairobi hospital.

Mungu wa mbinguni inusuru CHADEMA.

Kwako Lucas 😂🔥
Hapa kuna kitu hakiko sawa ndani ya CHADEMA ingawa makamanda hawataki kukubali.
 
Leo ma mangi wako kazini...

Ni hawa tu ndio hawaonagi makosa ya Mbowe...

Ngoja tusubiri hadi mwisho.
 
Unaweza kufuata katiba lakini hiyo katiba Ikawa na mapungufu Moja kati ya pungufu katika katiba ya CHADEMA ni kutoweka ukomo katika cheo Cha Mwenyekiti
Mfano tu sisi tunaolilia katiba mpya kwani Nchi haina katiba? Katiba ipo ila tunaona baadhi ya maneno Yana mapungufu na kwa hili lazima Chadema wajirekebishe waludishe kipengere Cha ukomo kama ilivyokuwa mwanzo

Na kwa utaratibu huu atatokea mwingine atarekebisha katiba na kujiita Mwenyekiti wa milele
Mwishoni umenichekesha sana mkuu, lakini je Chadema ilisajiriwa bila kuwa na katiba? Wasajiri hawakuona hicho kipengere au Chadema walikibadilisha baada ya usajiri? Jiulize shida hapo ni Chadema au serikali kwa ujumla. Ishu ndogo sana hapo wewe gombea ukionekana utaleta maendeleo na kukisimamia chama utachaguliwa. Achana na wale wanaochapisha fomu moja tu,hapa unasemaje?
 
Msigwa ashapoteza sifa ndani ya chadema, Teknolojia imemummbua, sifa zilimjaa anajiona yeye ndio chadema na chadema ndio yeye. arudi kanisani akadanganye upande huo tena siasa zishamshinda, unakaa miaka 10 nafasi hutosheki?
Mwenyewekiti amekaa miaka mingapi au umeiona miaka kumi ya Msigwa tu?
 
Ndugu zetu wa Iringa huwa hawapendi kuonewa rejea Chifu Mkwawa alivyowanyoosha Wajerumani na ukawaonea Wanajinyonga.

Maranja anachezea Moto.
 
😂 So demokrasia ni ile ya kumuweka mtu kama Jiwe madarakani au siyo
Kwenye kuchagua kina kupatia na kukosea na ndio maana Kuna ukomo kama umepatia atakae kuja ataendeleza mazuri yako na kama umekosea atakaekuja atarekebisha makosa yako lakini hili la kuongoza wewe tu mpaka Mungu atakapokuchukua ni dalili za Udikteta
😂 So demokrasia ni ile ya kumuweka mtu kama Jiwe madarakani au siyo
Chedema kwenye uongozi wa juu haina tofauti na Museveni,Kagame nk wewe unaona hiyo ndio Demokrasia tuitakayo?

Unaonaje Leo bunge likakaa na kuondoa ukomo wa vipindi viwili na wakaja na style Rais achaguliwe tu mpaka watu watakapochoka?
 
Ni aibu sana kutupiana maneno ya khanga mitandaoni.....Msigwa umejijengea heshima kubwa sana ndani ya CDM ,sidhani kwamba nafasi ya uenyekiti ni kubwa kuliko ubunge.....Kubali matokeo.....Ni ngumu kumshinda Sugu.
 
Ndugu zetu wa Iringa huwa hawapendi kuonewa rejea Chifu Mkwawa alivyowanyoosha Wajerumani na ukawaonea Wanajinyonga.

Maranja anachezea Moto.
Maskini hawezi shindana na Tajiri

Msigwa na Lisu malofa Hela hawana washukuru hata hiyo tunafasi walitupata Kwa huruma tu za matajiri wa Chadema
 
Kwenye kuchagua kina kupatia na kukosea na ndio maana Kuna ukomo kama umepatia atakae kuja ataendeleza mazuri yako na kama umekosea atakaekuja atarekebisha makosa yako lakini hili la kuongoza wewe tu mpaka Mungu atakapokuchukua ni dalili za Udikteta

Chedema kwenye uongozi wa juu haina tofauti na Museveni,Kagame nk wewe unaona hiyo ndio Demokrasia tuitakayo?

Unaonaje Leo bunge likakaa na kuondoa ukomo wa vipindi viwili na wakaja na style Rais achaguliwe tu mpaka watu watakapochoka?
Mkuu sijasema achaguliwe, namaanisha kugombea, kama kuna bora zaidi yake basi atachuguliwa huyo. Kikubwa uchaguzi uwe huru bila magumashi
 
Back
Top Bottom