PostGE2025 Mchungaji Msigwa: Msajili wa vyama vya siasa ana matatizo, hayupo kwa maslahi ya Taifa

PostGE2025 Mchungaji Msigwa: Msajili wa vyama vya siasa ana matatizo, hayupo kwa maslahi ya Taifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mchungaji Peter Msigwa akihojiwa na Wasafi FM, Juni 2, 2026 amesema;

"Mvutano kati ya Msajili na Chadema haujanza leo. Lakini tukiwa wakweli ambao, hatupepesi macho, na tunalipenda taifa kuliko vyama vyetu vya kisiasa itikadi; nadhani Msajili hayuko sawa, mizani haija—balance. Kwa sababu maneno hayo hayo, au vitendo hivyo hivyo vinaweza vikafanywa na chama tawala, Msajili anakaa kimya. Lakini neno hilo hilo likifanywa na upinzani, miaka yote, anapiga kelele.

Mfano mwepesi kabisa, mimi nimekaa na Richard Kasesela; Alivyokuwa mkuu wa wilaya, alilitumia lile neno ambalo sio vizuri kulitaja hapa. Lakini na mwingine wa Chadema amelitumia hilo hilo. Alivyo litumia huyo wa Chadema amepewa barua, yule wakati alilitumia hakulipewa barua. Sasa nadhani ili tuwe na utengamano na utulivu, mizani inatakiwa i-balance.

Kwa hiyo mimi nadhani Msajili wa vyama vya siasa ana matatizo. Yaani hayupo kwa maslahi ya taifa, yupo kwa interest ya kikundi kimoja katika nchi, ambayo hiyo ni ni jambo baya sana.
 
Hujamalizia Tena huyo alitamka neno Hilo akiwa kiongozi wa chama tawala! Ambaye alipaswa kuwa mfano Bora,Hawa CHADEMA hawajawahi tawala!
 
Back
Top Bottom