Mchungaji Msigwa umetukosea heshima wanandugu kwa kushindwa kutambua mchango wa fedha za familia

Kama kweli wewe ni ndugu wa damu wa Mch. Peter Msigwa basi nampa pole kuwa na ndugu juha kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka DNA test tuone kama wewe kweli ni ndugu. Wapo wengi wanajiita ndugu lakini ni aliens
 
Msigwa kasema mambo ya kifamilia yanaongelewa nyumbani kifamilia siyo kwenye kadamnasi na si hapa jamvini. Kaongeeni hayo nyumbani kuwa kawakosea kutotambua mchango wenu.
 
Hili litakuwa lijitu la ccm limetumwa kuja kuleta porojo huku ili kuhadaa umma wa wapigania haki, Mh Msigwa ni wa kwetu nyie nendeni huko mkaangaike na Polepole
 
  • mngepeleka chadema waunganishe nguvu.
  • kama mliona za maana si mngeenda benki kimya kuzilipa na kumtoa?
  • matangazo yalikuwa ya nini?
  • kwanini muanze michango baada ya wanawake wa chadema kutolewa rumande?
  • kama vipi andamaneni mkadai hela zenu pale KRA
Tenda wema nenda zako
 
Kwani aliwaomba mumchangie au kiherehere chenu ili mjiinue baada ya kujua rais ni ndg yenu.
Nyambafu na msirudie tena, msigwa syo wa kulamba miguu inayonuka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msigwa ni mchungaji wa kanisa la vine yard kama sijasahau. alikuwa anatumia ukumbi kwa kufanya ibada karibu na makitaba iringa. Nimeabudu kanisani kwake. Ni mtumishi wa Mungu! Nimewahi kum translate kwa kiswahili wakati yy akihubiri kwa english. Mahubiri ya mchungaji yako very powerful.

Anapenda sana kutunza mazingira na akiwa anauza pia miche ya miti, maua, nk.

Lakini Najiuliza kama huyu mtumishi wa Mungu anao muda tena wa kuchunga kondoo wa Bwana maana asilimia 100 yuko kwenye siasa. siasa za kushinda mahakamani, polisi, nk.
 
Huyu atakuwa ni mpuuzi mwingine. Hakustahili kuchanganya undugu na ushabiki wake kwa CCM.

Hakukuwa na ndugu yeyote yule mpaka akatafutwe Polepole?
 
Mkuu upako anao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeanza vizuri kwa kumsifia Mchungaji Msigwa, kwa nini tena unamalizia kwa kumzodoa ?.
 
Mambo Yakifamilia yana taratibu zake,msigwa ni simba Wa yuda nitaendelea kumuheshimu sana
 
Sijawahi kuona Wahehe wanafiki kiasi hiki.
Wakati "mwanafamilia" mwenzenu anampeleka Mhe. Peter Msigwa mahabusu 'bila kosa' na kumpitisha Kisutu wakati anampeleka jela, Wanafamilia mlikuwa mmeziba masikio na kufumba macho?
Masononeko na mateso ya watoto wa Msigwa, na mama yao hamkuyaona?
Masononeko yenu yamejitokeza tu, baada ya Watanzania kumtoa jela?
Luvanda Ngurusavangi Msigwa, unajua kuwa kulipa faini maana yake ni kwamba Mhe. Peter Msigwa ametumikia kifungo?
Unajua kuwa kumbukumbu za kifungo ni doa chafu katika maisha yake?
Je, wanafamilia mnaandaa utaratibu gani kufuta hilo doa chafu?
Luvanda, wanafamilia mmejipangaje kuhakikisha kuwa mwamafamilia mwenzenu Mhe. Peter Msigwa anaendelea kupata haki yake ya kuongea na Watanzania waliompigia kura kuwa Mbunge ambazo zimenyakuliwa a "mwanafamilia mwenzenu aliyechangia milioni 38"?
Kinyume cha hapo, wewe Luvanga Ngurusavangi Msigwa utakuwa ni mshiriki wa utesaji wa Mhe. Peter Msigwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…