Pre GE2025 Mchungaji Peter Msigwa abainisha kuwa hakuna mpango wa kugombea uongozi ngazi ya taifa

Pre GE2025 Mchungaji Peter Msigwa abainisha kuwa hakuna mpango wa kugombea uongozi ngazi ya taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
17 April 2024

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa abainisha kuwa hakuna mpango wa kugombea uongozi ngazi ya taifa....

Mch. Msigwa asisitiza viongozi wa CHADEMA Taifa wasichafuliwe kuwa wana wagombea wa kanda na mikoa mfukoni, bali wagombea ngazi za kanda na mkoa wajitokeze kwa kuuza sera ...
 
Bahati mbaya sana kwetu sote, kwamba hizi ndizo habari muhimu kutoka ndani ya chama hiki wakati kama huu!

Acha CCM iendelee kutufanya mateka.
 
Achukue fomu ya uenyekiti, it's about time Mbowe awe challenged. Same to Lissu na Heche wote wafocus kwenye uenyekiti ndio itakua referendum nzuri ya kupima uongozi wa Mbowe.

Cc Tindo
 
Chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema ni lazima Mwenyekiti wake awe ni mtu ambaye pamoja na exposure atakayokuwa nayo katika mambo mengi yanayohusu uongozi lakini ni muhimu pia awe na uwezo au awe amezungukwa na watu wenye uwezo kiuchumi !!
Ni sawasawa na klabu za mpira bila kuongozwa au kudhaminiwa na watu wenye Fuweza kweri kweri hizo timu hata ziwe na wachezaji mahiri kama Mbappe au Halland ni kazi bure haziwezi kufua dafu kamwe !!

Huo ndio ukweli usiokuwa na mashaka ndani yake !! 🙏🙏
 
Bahati mbaya sana kwetu sote, kwamba hizi ndizo habari muhimu kutoka ndani ya chama hiki wakati kama huu!

Acha CCM iendelee kutufanya mateka.
Matarajio yako ulitaka yawe..."MSIGWA ALETA MEGAWATI LAKI SABA ZA UMEME KUTOKA IRINGA"...(?)
NB;Kila habari huenda kwa muda na muktadha wake.Usiyavute masikio juu kusikiliza harufu badala ya sauti.
 
Ndani ya Ccm pia ni marufuku mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kushindana na Mwenyekiti wa Chama ! 😅😅
 
Matarajio yako ulitaka yawe..."MSIGWA ALETA MEGAWATI LAKI SABA ZA UMEME KUTOKA IRINGA"...(?)
NB;Kila habari huenda kwa muda na muktadha wake.Usiyavute masikio juu kusikiliza harufu badala ya sauti.
Mbona hayo ya "MEGAWATI" umeyawaza wewe!
Habari ya muda wote kama hutambui ni "CCM kuwaweka mateka waTanzania"
Yaani hata 'hint' hiyo niliyoiweka haikuweza kukustua akili kidogo! Hakika "masikio huko husikiliza harufu."
 
Hakika dawa ya mtu muongo huwa ni fupi sana.

Kumekuwepo na propaganda chafu zikienezwa kwa makusudi na watu kutoka CCM kwa makusudi ili kuleta mpasuko ndani ya CHADEMA.

Wanasema eti Msigwa anataka kumpindua mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA MH Mbowe.

Hizi ni propaganda za majitaka njia za hovyo na nikuonyesha kuwa CCM hawajiamini wakati wapo kwenye uongozi kwa zaidi ya miaka 60.

CCM kamwe hawawezi kuichagulia CHADEMA viongozi hata siku moja.

Kama wanataka kuwachagulia viongozi waendelee na vyama vyao vya mfukoni maana vipo vingi.

Hakika dawa ya mtu muongo huwa ni fupi sana.

Kumekuwepo na propaganda chafu zikienezwa kwa makusudi na watu kutoka ccm kwa makusudi ili kuleta mpasuko ndani ya CDM.

Wanasema eti Msigwa anataka kumpindua mwenyekiti wa taifa wa CDM MH Mbowe.

Hizi ni propaganda za majitaka njia za hovyo na nikuonyesha kuwa CCM hawajiamini wakati wapo kwenye uongozi kwa zaidi ya miaka 60.

CCM kamwe hawawezi kuichagulia CDM viongozi hata siku moja.
Kama wanataka kuwachagulia viongozi waendelee na vyama vyao vya mfukoni maana vipo vingi.View attachment 2967396
Sasa km walijua ni propaganda wanajibu nn. Si wafanye vitendo
 
Back
Top Bottom