Pre GE2025 Mchungaji Peter Msigwa abainisha kuwa hakuna mpango wa kugombea uongozi ngazi ya taifa

Pre GE2025 Mchungaji Peter Msigwa abainisha kuwa hakuna mpango wa kugombea uongozi ngazi ya taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kang'oe kwanza magego yako ndiyo uwapangie CDM nini cha kufanya

Miaka ni ishirini sasa, magego ya kuyang'oa ni ya Mwenyekiti wa CHADEMA.

Madeni yake ayadai akiwa nje ya chama. Vyama vingine vishaonyesha ukomavu, CHADEMA inangoja nini? Haijalishi.

Mmelia Kulikuwa na Udikteta Nchi hii wakati Dikteta namba moja yupo CHADEMA.

Ni hivi sasa, ninakuhakikishia, ukianzisha poll hapa Jamiiforums ya kuchagua nani anayefaa kukivukisha chama katika wanja hili jipya la Siasa na Demokrasia, Mwenyekiti wa CHADEMA ataangukia pua.

Itoshe, akiingia tu kwenye Kinyanga'anyiro cha kuwania Urais uchaguzi mkuu 2025, CHADEMA ndio 'itapotezwa' mazima.
 
Asee d.j mbowe hiyo nafasi atakufa nayo
Hebu fikiria akipata Uraisi itakuaje??
Ujue huko CHADEMA anatumia manguvu, kubakia madarakani, akiwa Rais wa Nchi je?

Ndio maana wanataka Kubadilisha Katiba, ili aweze kuwania nafasi hiyo bila ya ukomo kama ilivyo CHADEMA.
 
Hakika dawa ya mtu muongo huwa ni fupi sana.

Kumekuwepo na propaganda chafu zikienezwa kwa makusudi na watu kutoka CCM kwa makusudi ili kuleta mpasuko ndani ya CHADEMA.

Wanasema eti Msigwa anataka kumpindua mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA MH Mbowe.

Hizi ni propaganda za majitaka njia za hovyo na nikuonyesha kuwa CCM hawajiamini wakati wapo kwenye uongozi kwa zaidi ya miaka 60.

CCM kamwe hawawezi kuichagulia CHADEMA viongozi hata siku moja.

Kama wanataka kuwachagulia viongozi waendelee na vyama vyao vya mfukoni maana vipo vingi.

asate Mh Msigwa
 
Wanoko wa CCM umewagalagaza kikweli kweli leo!

johnthebaptist msikilize Mchungaji Msigwa na wapelekee ujumbe wenzako, maana umelikomalia la Uenyekiti wa Mbowe as if bila kumtaja Mbowe kwako ugali haupatikani

 
Back
Top Bottom