LGE2024 Mchungaji Peter Msigwa aichachafya CHADEMA mchana kweupe, afunguka Ugomvi uliopo kati ya Mbowe na Lissu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Bado ana mahaba ya dhati na mtalaka
 
Inawezekana ni kweli... Hapa anaonyesha kuwa naye ni mnafiki. Kayajua hayo kwa miaka 20 kaendelea kukaa hadi pale walipomnyima uongozi ndipo katoka. Ila kama angepewa angeendelea kukaa humo humo na kuendelea kudanganya. Huyu ina maana hata ccm akikuta kuna mabaya as long as anapata uongozi hatosema ataendelea kukaa hata miaka 50.
 
Anasoma scripts
Anasoma scripts katika waliokosea kuchanga karata zao ni huyu mwehu.yeye alifuatwa mpaka gerezani kwa amri ya Magufuli akakataa leo upepo umebqdilika ati ndo anahama?
 
Msigwa ni mtu mkweli. Mtu alikuwa kamati kuu ya CHADEMA hawezi danganya.
 
Msigwa ni mtu mkweli. Mtu alikuwa kamati kuu ya CHADEMA hawezi danganya.
Kinana alikuwa kamati kuu ccm mbona alidanganya akasafirisha twiga wakiwa hai?
Majaliwa yupo kamati kuu mbona alidanganya kwamba Magufuli yu mzima kumbe keshakufa?
Samia yupo cc mbona alidanganya kwamba ajali ya kariakoonilipotokea hakuwepo nchini wakati alikuwepo?
Jifunze kufikiri acha UCHAWA
 
Yaani zaidi ya miaka 20 unaona madudu huko CHADEMA upo tu?...sema ukweli Mtumishi,sio ile kuukosa MKATE wa hiyo kanda??
 
Hayo yoote hakuwahi kuyasema hafi pale alipopigwa chini kwenye uchaguzi wa kanda?
 
Kwani Msigwa hajui kuwa watu wanachagua upande wa pili kwa kuwa CCM wameshindwa kufanya kile ambacho wanapaswa kuwafanyia wananchi?.
 
Wabongo bana! Mtu mmoja anachachafyaje taasisi? Aliondoka Slaa na Kabourou kabla hujazaliwa na hajachachafya atakuwa huyu jamaa? Inasikitisha sana, akiichachafya basi itakua na udhaifu mkubwa. Alikuwepo kwenye huo ugomvi akawaamua? Au anapiga ramli na maombi naye pia? Ila wabongo kwa kuwa ni watu wa kiroho sana watamuamini natarajia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…