Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mtumishi wa Mungu Mchungaji peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada mtiifu na Mzalendo kwa chama cha Mapinduzi na ambaye anajutia uamuzi wake wa kupoteza nguvu zake na muda wake wa miaka takriban 20 kuwa ndani ya CHADEMA.
Amsema kuwa CHADEMA ni Sacco's ya mtu ,ambapo hata maamuzi yanafanywa na kumtegemea mtu mmoja.akiendelea kuichana chana CHADEMA ameendelea kusema ya kuwa ni chama kilichojaa utapeli kwa kuwahadaa wananchi kuwa kimejaa na kupigania demokrasia,haki na uhuru ,jambo ambalo siyo la kweli na mambo hayo hayapo wala kufanyika ndani ya CHADEMA.
Soma Pia Mchungaji Msigwa: Nitazunguka Nchi nzima kuelezea Uongo wa CHADEMA
Mtumishi huyo Wa Mungu ameendelea kusema Kuwa CHADEMA haina uhalali wa kuikosoa wala kuishambulia CCM kwa jambo lolote lile .akasema yeye kama mtumishi wa Mungu Biblia inaeleza kuwa unapaswa kutoa kibanzi katika jicho lako kabla ya kumnyooshea kidole mtu Mwingine.
Mtumishi huyo wa Mungu akiwa na sura ya tabasamu na furaha na kupendeza vizuri ndani ya sare za CCM amesema ya kuwa anawasihi sana wananchi kuacha kabisa habari za kuambiwa na CHADEMA kukunja ngumi mpaka migongo yao inapinda.
Mtumishi huyo Wa Mungu akaendelea kusema kuwa kazi ya upinzani hasa CHADEMA ilikuwa ni kupinga pinga tu kila kitu.akatolea mfano kuwa Hayati Daktari Mwalimu John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa anaanzisha ujenzi wa miradi mikubwa kama vile Bwawa la Mwalimu Nyerere,SGR pamoja na Daraja la Busisi. Wao CHADEMA na wabunge wao walikuwa wanafanya kazi ya kupinga pinga tu miradi hiyo yenye manufaa makubwa Kwa Taifa letu.
Mtumishi huyu wa Mungu ambaye anaendelea kuisambaratisha CHADEMA kanda ya Ziwa kwa kuusema ukweli mchungu juu ya ulaghai na utapeli wa CHADEMA,amewasihi sana wananchi kuiunga mkono CCM na kuunga juhudi za Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan katika ujenzi wa Taifa letu.
Ikumbukwe ya kuwa mtumishi huyu wa Mungu anaifahamu sana CHADEMA.na ndio maana anaongea vitu vya ukweli na uhalisia kabisa juu ya utapeli uliopo na kujaa ndani ya CHADEMA.ikumbukwe na kufahamika ya kuwa huyu ni Mtumishi wa Mungu ambaye hawezi kudanganya wala kusema uongo juu ya kile kilichopo ndani CHADEMA,maana Mtumishi wa Mungu ni Mwenye hofu ya Mungu na ndio maana ameona asiendelee na dhambi ya kuwadanganya na kuwapoteza watu kuwa waiamini CHADEMA.ndio maana ameona aepuke dhambi hiyo kwa kuondoka CHADEMA na kujiunga na CCM chama kilichobeba matumaini ya mamilioni ya watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.