Me and me
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 226
- 496
Jamii nyingi zimepiga hatua katika maendeleo ya kiteknolojia na Ustaarabu (civilization) japo bado kuna jamii chache zimebaki na Ustaarabu wa zamani ambao jamii nyingi tayari wamepiga hatua kutokea huko. Mfano hiyo jamii uliyoitaja.Mabinti wa ki Hadzabe huwa wanatembea matiti yakiwa nje bila kufunikwa na nguo na hawabakwi huko kwao mapolini...
Hiyo hoja ya kufunika mwili haina mashiko kabisa, ni heri useme mporomoko wa maadili ndio unawafanya Me hasa wale waishio mjini kuwaingilia Ke kwa tamaa zao za kimjini mjini
Sasa kwa jamii kama hiyo bado norms zao na morals zinawaruhusu kuvaa hivyo na wala kwao haina shida na mindset yao katika kutamani haipo hapo.
Ila kwa jamii zetu ambazo kwa tafsiri ya ujumla zimepiga hatua katika Ustaarabu tayari tumekubaliana Mwanamke asioneshe maumbile yake na maungo yake yatakiwa yafichwe hii mindset ndio inatufanya tukiyaona yale yaliyotakiwa kufichwa tuhisi hisia za matamanio.
Kwaiyo usilinganishe jamii zenye Level tofauti tofauti za Ustaarabu (civilization). Kwani hata Mindset zao ni tofauti tofauti.