Mchungaji wa KKKT mbaroni kwa kumbaka binti wa miaka 15 mbele ya mdogo wake

Mchungaji wa KKKT mbaroni kwa kumbaka binti wa miaka 15 mbele ya mdogo wake

Mission was incomplete......watu wawili ambao usije ukajidanganya wataficha siri ni Mtoto na Mzee.
Binti alikuwa ameficha siri hiyo kama kawaida yake, ila mchungaji Lauwo alimkomalia sana kumdadisi kwa vitisho ikabidi afunguke..... Lauwo naye alikuwa anataka kujipigia hapo kaamua kumchafua mtumishi mwenzie tu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria – Busweru, Samweli Lunzebe kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda unyama huo mbele ya mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne ambaye ni mdogo wake binti huyo.

Akizungumza na waandishi Alhamis, Mei 30, Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi la polisi linamshikilia mchungaji huyo katika kituo cha Polisi Nyamagana mkoani Mwanza kwa mahojiano zaidi.

“Ni kweli jeshi linamshikilia na kumuhoji kuhusiana na hilo tukio hilo na uchunguzi unaendelea hivyo ukikamilika atafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Mutafungwa

Aidha, Kamanda Mutafungwa amebainisha kuwa Mchungaji Samweli Lunzebe alikamatwa tarehe 27 Mei mwaka huu kwa tuhuma za kumuingilia kimwili binti huyo mwenye umri wa miaka 15 jambo ambalo linatafsirika kuwa ni ubakaji.

Aidha, akizungumzia tukio hilo ambalo taarifa zake zimesambazwa kwenye mitandao, Kamanda Mutafungwa amesema bado hajapata taarifa hizo.

Mwanahalisi ilipotaka kujua kuhusu Mchungaji Moses Lauwo anayedaiwa kusambaza mahojiano yake na binti huyo pamoja na taarifa za Hospitali Kamanda Mutafungwa alisema “Mimi sijaisikia hiyo sauti na kama unayo ningependa unirushie niifuatilie.

“Lakini niseme kama ipo, si maadili mema ya kumu-‘expose’ shahidi kiasi hicho kwa sababu shahidi baadaye anatakiwa kutoa ushahidi mahakamani katika utaratibu ulioruhusiwa kisheria kimahakama na utaratibu unaolinda faragha za watu”

Tukio hilo liliripotiwa baada ya kusambaa kwa sauti ya mahojiano baina ya Mchungaji Moses Lauwo na Binti huyo ambapo Mchungaji alitaka kujua ilikuwaje akafanyiwa kitendo hicho na Mchungaji Lezebe.

Sauti ya mahojiano ya Mchungaji Lauwo na binti huyo inaendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii ya makundi sogozi sambamba na ripoti ya daktari jambo ambalo pia linatafsiriwa kuwa ni udhalilishaji kwa mtoto huyo.

Akizungumza na binti huyo, Mchungaji Lauwo kupitia sauti hiyo alitaka kujua ni nini kilimtokea binti huyo mpaka akawa na uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji Luzebe.

Binti huyo kupitia sauti hiyo alisema kuwa anamfahamu Mchungaji Luzebe kuwa ni baba wa rafiki yake (jina linahifadhiwa).

''Mimi nilifahamiana na mchungaji huyo siku nilipoenda nyumbani kwa rafiki yangu ambaye alinipa namba za simu ya baba yake ambayo huitumia kuwasiliana na marafiki zake. Sasa nilipoipata namba hiyo yeye ndio alianza kunipenda,”

Aliendelea kusimulia kwa kusema kuwa “Baada ya Lunzebe kupata namba yake siku moja nilimpigia ili niongee na rafiki yangu ndipo mchungaji huyo akaanza kunitumia meseji kwenye yangu ya kunitaka niende nyumbani kwake. Sikuenda akanipigia simu akauliza kwanini sikuenda nikamwambia nilibanwa na kazi.

“Simu yangu iliharibika nikamwambia, akaniambia niende atanipa simu,” anasema.

Anasema siku moja alimwambia wakutane eneo linaloitwa National huko mkoani Mwanza ili akamnunulie simu lakini alipoenda na kuonana naye Mchungaji huyo hakwenda kumnunulia simu na kudai amesahau kadi za benki kwenye begi hivyo watakwenda siku nyingine.

“Akaniambia twende huku tukawa tunaenda tu mimi sikujua kuwa tunaenda wapi… kwa sababu hakuniambia kuwa tunaenda nyumba ya wageni tukawa tunaenda tu… kumbe tunaenda guest. Nilikuwa na mdogo wangu, tukaingia mimi na mdogo wangu tukakaa kwenye stuli.

“Akanilazimisha niende kukaa kitandani, nikamuacha mdogo wangu amekaa kwenye stuli mara akaanza kunishikashika kisha akaniingilia kimwili huku mdogo wangu mwenye umri wa miaka minne akiwa amekaa pembeni,” anaeleza binti huyo.

Akizungumza na MwanaHALISI hivi karibuni, Mchungaji Lauwo alisema taarifa za binti huyo kuingiliwa kimwili na mchungaji Lunzebe alizipata kutoka kwa wazazi wa binti huyo.

Mchungaji Lauwo amefafanua kuwa hajasambaza mahojino hayo kwenye mitandao ya kijamii, bali baada ya kumhoji binti huyo ali’share’ na watu ambao wangeweza kumsaidia binti huyo kupata msaada wa kisheria.

Alisema alituma sauti ya mahojiano hayo kwa Mkuu wa Jimbo Kanisa la KKKT Mkoani Mwanza, Obadia Ruhalile ambaye Mchungaji huyo Lunzebe yupo chini yake.

Mchungaji Lauwo aliendelea kueleza kwamba aliamua kumripoti Mchungaji Lunzebe ili mamlaka zinazomsimamia zimchukulie hatua za kisheria.

MwanaHALISI Online lilizungumza na Mchungaji Obadia ambaye alithibitisha kutumiwa sauti hiyo.

“Yeye (Lauwo) alinitumia sauti hiyo lakini bahati mbaya pia alikuwa ameiweka kwenye Group la Wakristo… nikamwambia asiisambaze popote tena kwa sababu nilitaka niisikilize nijue nitachukua hatua gani kama kiongozi, hivyo sijaisambaza popote” alifafanua Mchungaji Obadia

Hata hivyo, alisema kwa kuwa group hilo la whatsap lenye watu wengi, inawezekana wao ndio waliosambaza sauti na ripoti hiyo ya daktari aliyemfanyia uchunguzi binti huyo.
Mungu tuepushe na vitendo vya kikatili kwa watoto
 
Hii dayosis ina shida nyingi sana ikiwemo masuala ya
ukirtimba, ukabila, undugu na kujuana
Zingatia pia kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi kwahiyo kichabya kwamba hii tuhuma ya huyu bwana ni ya kweli, ila ni katika harakat za kuchafuana na kuharibiana ugali.

Huyu bwna aliyevujisha hizo sauti za mahojiani, Mchungaji Moses Lauwo ,kwa mujibu wa chanzo changu cha ndani kabisa hapo Ndani ya dayosisi, ni mchungaji ambaye ana kisasi na anawatafuta wenzake maana yeye mwenyewe tayar alishafukuzwa baada ya kukamatwa live live akimtomba mke wa mtu. Alikamatwa red handed muda sasa umepita na akafukuzwa. Hivyo hik amefanya ni katika kudhirisha kuwa sio yeye peke yake aliye mchafu katika viongozi wa kanisa.

Wapo wengi na yapo mengi machafu yanayofanyika.

Back to huyu mtoto aliyebakwa ni kwamba kwa mujibu wa mahojiano, hayupo shulen almost zaidbya miez mi 3 na baada ya kikao cha board ya shule kukaa ,akafukuzwa shule. Hivyo unaona kabusa kuwa binti naye si haba anajua jua anachofanya.

Makanisa haya siku hiz ni vichaka vya wahuni tu
 
Ugalatia ni dini ya kabaka vitoto
Mtaacha lini huu ushenzi
20240601_153759.jpg
 
. Hizi dini ikiwezekana zifutwe tu.. 🤒🤒
. Maana sijaona umuhimu wake
sasa kama kungekuwa na dhambi nafuu hiyo si nafuu, amemuingilia kwenye uke, yule shehk wa rufiji ambaye MKuu wa wilaya kasema amewaingilia watoto wa madrasa 15 kinyume na maumbile je?

kwa wachungaji, mara nyingi ukiona hivi jua ni mnyukano wa madaraka, ametafutiwa kosa, ameingia king. akapambane na hali yake huko wakati mwenzake anachukua jimbo. siku zote shetani huwa anakutafutia kinyongeo na kukumaliza bila huruma, huyo aende akapambane huko, though ni ngumu kuamini kwamba binti ana miaka 15, aingie guest house na mtoto wa miaka 4 pamoja na libaba hilo, hao watu wa guest house wasingemzuia? wasingemripoti akutwe red handed? kama mtu wa guest alinyamaza, naye akamatwe, alikula njama hiyo pamoja na huyo mchungaji.

walutherani tulishawaambia muokoke hamtaki, haya sasa ona yanawakuta.
 
Yawezekana pengine ni kweli, lakini taarifa za namna hii unatakiwa kuwa nazo makini Sana kwa sababu siku hizi watu wamekuwa wakitengeneza Sana Visa vya matukio ya namna hii kwa lengo la kuchafuana na kuharibiana CV.

Matukio ya kufanyiana visasi ili kukomoana.
Hata mi ninihisi hivyo na nilitaka kuandika comment kama hii. Kwanini isambazwe kwenye mitandao na kwenye magroup? Hapa kuna jungu limeandaliwa.
 
Kosa kwa mchungaji kosa kwa mbakwaji
Tokea mwanzo alisha ona dalili za kutakwa kimapenzi tena na baba wa rafiki yake inakuaje baada ya hapo akaendeleza mazoea mpka kupelekana guest
Miaka 15 bado ni mtoto usimpe lawama katika hili, yeye hakuona hatari yoyote ndio maana akaenda na mdogo wake wa miaka 4!
 
sasa kama kungekuwa na dhambi nafuu hiyo si nafuu, amemuingilia kwenye uke, yule shehk wa rufiji ambaye MKuu wa wilaya kasema amewaingilia watoto wa madrasa 15 kinyume na maumbile je?

kwa wachungaji, mara nyingi ukiona hivi jua ni mnyukano wa madaraka, ametafutiwa kosa, ameingia king. akapambane na hali yake huko wakati mwenzake anachukua jimbo. siku zote shetani huwa anakutafutia kinyongeo na kukumaliza bila huruma, huyo aende akapambane huko, though ni ngumu kuamini kwamba binti ana miaka 15, aingie guest house na mtoto wa miaka 4 pamoja na libaba hilo, hao watu wa guest house wasingemzuia? wasingemripoti akutwe red handed? kama mtu wa guest alinyamaza, naye akamatwe, alikula njama hiyo pamoja na huyo mchungaji.

walutherani tulishawaambia muokoke hamtaki, haya sasa ona yanawakuta.
Ripoti ya daktari inasemaje kwenye hiyo taarifa iliyovuja?
 
Ripoti ya daktari inasemaje kwenye hiyo taarifa iliyovuja?
being a lawyer, hiyo ni statutory rape, huyo binti lazima haikuwa mara ya kwanza, kalikuwa kazoefu na hata kanapohusiana na mchungaji kalikuwa kanajua kinachoendelea ila akikamatwa ndio anatoa maelezo meeengi ati sijui simu sijui nini. kwenye kubaka, kinachohitajika ni mpenyo tu (penetration) ndio huwa inaangaliwa, hivyo hata ukienda kwa daktari, kinachotakiwa kuangaliwa ni kama iliwezekana kupenya, yaani kama hamna bikra. kama bikra ipo sio lazima kuwepo shahawa au michubuko kama wengi tulivyokuwa tunaamini, kwasababu penetration however slight, yaani hata ukiingiza nusu ya kichwa tu, umeshabaka. na kwa hao wanaokubali wenyewe, hiyo ni statutory rape, kufanya ngono na binti ya miaka chini ya 18 asiye mkeo. kwa miaka hii, kweli binti afike miaka 15, umwambie njoo ukae hapa kitandani na mimi, asijue kinachoendelea? asipige kelele, asiwe na consent? ndo maana inaitwa statutory na ni ngumu kupangua, inatusumbua sana kupangua mahakamani hiyo, mawakili wa serikali wakitupania inakuwa ngumu kwasababu wanasema ushahidi wa victim ndio unaoaminika, kabinti kakisema ni huyu umeisha.
 
Back
Top Bottom