Mchuzi wa nyanya ya kibati

Mchuzi wa nyanya ya kibati

Hiki kitu Uzile ulosagwa ni kitu gani mbona kiswahili kimepita kando
Mahitaji

  • Kuku wa kienyeji 1
  • Nyanya mbili zilizomenywa na kukatwakatwa
  • Kitunguu maji kikubwa kimoja kilichomenywa na kukatwa
  • Nyanya ya kibati vijiko viwili vya supu
  • Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
  • Juisi ya limau/ndimu kiasii
  • Uzile ulosagwa

Jinsi ya kutayarisha
  1. Mtayarishe kuku na umkate vipande kama kawaida,mtie kitunguu swaumu,pilipili manga,chumvi na uzile ulosagwa kijiko kimoja. Muinjike jikoni na Mfunike viungo vikolee muache atokote mpaka maji ya kauke,muongezee maji kiasi cha kumfunika kuku,mfunike na muache achemke.
  2. Akikaribia kuvia half way through mtie kitunguu maji na nyanya pamoja na nyanya ya kibati,ongezea uzile kijiko kimoja kingine cha chai na muache aendelee kuiva taratibu.Unaweza kuingezea maji ukipenda ili uwe na mchuzi mwingi.
  3. Mkamulie limau na adjust chumvi.
  4. Mchuzi huu mtam sana ukiula na wali wa nazi.
Cc farkhina, Mrs Kharusy, FirstLady, Angel Nylon, Revocatus Kashaga HP1, Honey Faith, xiexie, rasai, ICHANA, tama, Mwananchi, ladyfurahia
View attachment 163579
View attachment 163578
 
uzile ni sawa kama binzari ya pilau dia
uzile.jpg
 
aisee asante kwa pishi best ila mwenzangu yeye ni wa kijiji hajazoea nyanya paste labda nimtengenezee kwa nyanya za kawaida
 
Jamani nimechelewaaaa...hivi kuna kilichobaki lkn?? Au farkhina na Angel Nylon wamemaliza kila kituu...
Doh nasinzia ati nimeona NYAMA ya kibati halaf na kuku wa kienyeji nikawa najiambia two in one vitanogaje! sie wazee wa minofu!....lol
huyo alieulza hajui nyanya ya kibati ndio amenishtua...lol
 
Last edited by a moderator:

Tumebakisha Shoga.

Pishi hilo, hasara yako Wali ulokolea nazi tu.
 
Last edited by a moderator:
Jamani wana JF hivi ili pishi likipikwa na Gorgeousmimi na likapakuliwa na Fixed Point halafu Ladyfurahi akakukaribisha mezani mlaji unaweza kujisikiaje? halafu hicho chakula ukile na Evelyn Salt au Ichana au Masai dada, au au Tina Cute
litakuwa pishi la jioni ya leo.....
nitaongeza na pilipili mbuzi na rosemary.........
Asante kwa pishi hili
 
Jamani wana JF hivi ili pishi likipikwa na Gorgeousmimi na likapakuliwa na Fixed Point halafu Ladyfurahi akakukaribisha mezani mlaji unaweza kujisikiaje? halafu hicho chakula ukile na Evelyn Salt au Ichana au Masai dada, au au Tina Cute
waweza vimbiwa.........
 
tutakula huku nikisigua gaga
 
Mahitaji

  • Kuku wa kienyeji 1
  • Nyanya mbili zilizomenywa na kukatwakatwa
  • Kitunguu maji kikubwa kimoja kilichomenywa na kukatwa
  • Nyanya ya kibati vijiko viwili vya supu
  • Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
  • Juisi ya limau/ndimu kiasii
  • Uzile ulosagwa

Jinsi ya kutayarisha
  1. Mtayarishe kuku na umkate vipande kama kawaida,mtie kitunguu swaumu,pilipili manga,chumvi na uzile ulosagwa kijiko kimoja. Muinjike jikoni na Mfunike viungo vikolee muache atokote mpaka maji ya kauke,muongezee maji kiasi cha kumfunika kuku,mfunike na muache achemke.
  2. Akikaribia kuvia half way through mtie kitunguu maji na nyanya pamoja na nyanya ya kibati,ongezea uzile kijiko kimoja kingine cha chai na muache aendelee kuiva taratibu.Unaweza kuingezea maji ukipenda ili uwe na mchuzi mwingi.
  3. Mkamulie limau na adjust chumvi.
  4. Mchuzi huu mtam sana ukiula na wali wa nazi.
Cc farkhina, Mrs Kharusy, FirstLady, Angel Nylon, Revocatus Kashaga HP1, Honey Faith, xiexie, rasai, ICHANA, tama, Mwananchi, ladyfurahia
View attachment 163579
View attachment 163578

Shoga mchuzi mtamu sina la kukwambia nimeshiba apa kitumbo mbwiiiiiii

Sasa basi kuku nlompika ni wa kizungu maana wa kienyeji angenichelewesha nkamueka unga wa chicken soup weeeee harufu nzuriiii majirani sijui kama hawajaskia na wangekuja nsingemgaia mtu lol. Sasa hapo sikueka chumvi hata kidogo ule unga si una chumvu.....

Nkala ba pancakes zangu
 
Back
Top Bottom