Mchuzi wa nyanya ya kibati

Mchuzi wa nyanya ya kibati

huyo ndo anafaa haswa wallahi we muwekee moto mdogo tu aive taratibu....mchuzi huu mtamu,haukinaishi maana hauna mafuta waweza ule mpaka basii....

Mambo hayo......
 
Attachments

  • 20140610_221533.jpg
    20140610_221533.jpg
    426.3 KB · Views: 192
Shoga mchuzi mtamu sina la kukwambia nimeshiba apa kitumbo mbwiiiiiii

Sasa basi kuku nlompika ni wa kizungu maana wa kienyeji angenichelewesha nkamueka unga wa chicken soup weeeee harufu nzuriiii majirani sijui kama hawajaskia na wangekuja nsingemgaia mtu lol. Sasa hapo sikueka chumvi hata kidogo ule unga si una chumvu.....

Nkala ba pancakes zangu
wangekuja majirani ungewapa receipe nao wakajipikie…nimefurahi kusikia umeufurahia mchuzi….wakati mwengine hata mimi namuwekaga huo unga wa soup ya kuku kuongeza ladha na soup…inakuwa nzuri kwa kweli...🙂
 
Yeah nkaweka na curry powder kidogo...mtamuuuu
 
Shoga kuku huyu wa kienyeji nlionae mie anawivaa masaa 2 naimba nyimbo zote jikoni ndio awive lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

hahah na imani aliiva vizuri kuku wetu
 
Afadhali hapa hujatia aibu.
ila mie sili michuzi kabisaaa. Ningeacha iive hadi ikauke iwe rosti rosti. Na nyanya ya kibati siipendi. Ila naambiwa ina ladha tafauti kama smoked tomatoes
hili pishi nililipenda, my fav.
 
nyanya ya kibati ni kwa ajili ya rangi, lazima.ya tunda iwepo.

Hehehe, hivi vya hivi umenifikisha, tatizo ni ngano.

Afadhali hapa hujatia aibu.
ila mie sili michuzi kabisaaa. Ningeacha iive hadi ikauke iwe rosti rosti. Na nyanya ya kibati siipendi. Ila naambiwa ina ladha tafauti kama smoked tomatoes
 
Uzile ni nini jamani? Yani naona kila pishi wanaweka uzille afu ata sijui ni nini
 
Dada gorgeousmimi haya mapishi nayapenda maana kwanza huweki mafuta maana mimi si mpenzi wa mafuta, pili ukiongezea juice ya limau hapo umenimaliza kabisa ila ungeweka pia pili pili mbuzi hapo chuzi lingekuwa la mama Mpigi. Ila jamani lini nakaribishwa kula huo mlo wako?
Mahitaji

  • Kuku wa kienyeji 1
  • Nyanya mbili zilizomenywa na kukatwakatwa
  • Kitunguu maji kikubwa kimoja kilichomenywa na kukatwa
  • Nyanya ya kibati vijiko viwili vya supu
  • Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
  • Juisi ya limau/ndimu kiasii
  • Uzile ulosagwa

Jinsi ya kutayarisha

  1. Mtayarishe kuku na umkate vipande kama kawaida,mtie kitunguu swaumu,pilipili manga,chumvi na uzile ulosagwa kijiko kimoja. Muinjike jikoni na Mfunike viungo vikolee muache atokote mpaka maji ya kauke,muongezee maji kiasi cha kumfunika kuku,mfunike na muache achemke.
  2. Akikaribia kuvia half way through mtie kitunguu maji na nyanya pamoja na nyanya ya kibati,ongezea uzile kijiko kimoja kingine cha chai na muache aendelee kuiva taratibu.Unaweza kuingezea maji ukipenda ili uwe na mchuzi mwingi.
  3. Mkamulie limau na adjust chumvi.
  4. Mchuzi huu mtam sana ukiula na wali wa nazi.
Cc farkhina, Mrs Kharusy, FirstLady, Angel Nylon, Revocatus Kashaga HP1, Honey Faith, xiexie, rasai, ICHANA, tama, Mwananchi, ladyfurahia
View attachment 163579
 
Dada gorgeousmimi haya mapishi nayapenda maana kwanza huweki mafuta maana mimi si mpenzi wa mafuta, pili ukiongezea juice ya limau hapo umenimaliza kabisa ila ungeweka pia pili pili mbuzi hapo chuzi lingekuwa la mama Mpigi. Ila jamani lini nakaribishwa kula huo mlo wako?
Karibu 🙂
 
Back
Top Bottom