Dah Mkuu umetisha sana!
Ila ukiwa na mrembo ambaye moyo wako umemndondokea, unamwamini, unampenda na unamjari siyo mbaya mara moja moja kumtoa out za maana au kumnunulia zawadi. Ndio uanaume na mapenzi yalivyo.
Ingawa inategemea na uwezo wako, usifanye kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako. Kuna wengine kumnunulia mrembo zawadi ya TZS 20, 000 tu ni mtihani kutokana na kipato kuwa duni.
Lakini kuna watu wanamudu na ni kawaida kwao kila baada ya 3 months kumpeleka ampendaye katika maduka ghali kama Gucci & Louis Vuitton. Ukimnunulia mrembo Perfume, hereni, pochi, miwani na kiatu kwa mkupuo katika maduka ya Gucci & Louis Vuitton siyo ajabu zikakutoka 15, 000 USD au zaidi. Lakini kuna watu wanafanya na hawashtuki wala hawaachi. Ukitembelea hayo maduka pale Champs-Élysées Ave Paris, au 5 Ave NY, au Beverly Center LA utashangaa maduka yanavyojaa wanaume wakiwanunulia vitu vya gharama wanawake zao.
Vijana siyo mbaya siku moja moja uka copy style ya staring wa movie ya Pretty Woman, chamsingi usiidhurumu nafsi yako wala usiibe bali uzingatie urefu wa kamba yako. Ukimfanyia hivyo mwananmke huwa anakujari na kukupa umaalumu usio wa kawaida hata kama ni mpalestina.
Tuwatunze, tuwalinde, tuwajari na tuwafurahishe warembo tuliopewa na mungu kwani ni wajibu wetu.