Mdada katendwa kabakia haamini kama ni yeye ...

Mdada katendwa kabakia haamini kama ni yeye ...

Nilishawahi kusema hapa wakati fulani kwamba wanawake wengi wanaumia kwenye ndoa kwa sababu ya kuwasifu waume zao kwa mashoga kupita kiasi, si vibaya kumsifia mumeo kwa mashoga lakini pale yanapotokea mabadiliko kama haya usione aibu kusema umeshindwa na kuangalia mustakabali wako upya, kila mtu ameoa au kuolewa kwa utashi wake na hamna sababu ya mahusiano yenu au ndoa yenu kushikiliwa na majirani, marafiki au ndugu, kama yamekushinda bwaga manyanga anza maisha mapya, mambo ya kuanza kuwaza eti,...... "hivi majirani, ndugu au marafiki watanionaje?" yamepitwa na wakati, ndoa ni yako na sio ya kwao, anayeumia ni wewe na wala sio wao, na kama wakikuzodoa kwa kukusimanga wakikwambia ........ "kiko wapi ulichokuwa ukiringia...." Wao haiwahusu kwani wao wana maisha yao na wewe una maisha yako, kama alikuwa na tabia nzuri ni wakati ule,.......... Sasa kama amebadilika na kuwa na tabia za kiasherati wewe ufanye nini.......? Mtu hukuzaliwa naye tumbo moja, amelelewa kwao na wewe umelelewa kwenu, mmekutana ukubwani, kisa cha kutoana roho kwa sononi na msongo wa mawazo ni nini....!?
Kila mtu anaweza kuchukua ustaarabu wake kwani huo sio mwisho wa maisha.... na maisha ni popote, hata kama ukisemwa au kusengenywa na mashoga thamani yako iko pale pale wala haiondoki, ni wewe tu unayeweza kuiondoa kwa kujishusha na kujiona dhalili mbele ya binadamu wenzio..............
Kama ulioa au ulioelewa kwa malengo ya muda mfupi, kubwaga manyanga ni rahisi sana. Lakini kama ndo ile ya kufa na kuzikana, kazi kweli kiakili na kimwili kufanya hivyo. Na siyo suluhisho hilo.
 
Huyu mdada ni jirani yangu..

Alikuwa na ka mtindo fulani kila siku anamsifia husband wake ooh ndoa yangu ni imara na ni kama paradise ndogo
Mme wangu hawezi kurudi saa mbili usiku kama waume zenu wanavyofanya nashangaa mie.!
Akitoka kazini moja kwa moja home
Nawahurumia nyie waume zenu kurudi home saa tano..sita ,akiwahi sana saa nne mnawezaje haya maisha ..?
Sifa nyingi zilimiminika kwa huyu dear husband
..Mama mmoja wa makamo alikuwa mara nyingi akimwambia temea mate chini mdogo wangu,
Haya mambo omba mungu aendelee kumtunza mmeo
LOL sasa limezuka la kuzuka
Ghafla mme kaanza kurudi saa mbili eti ooh nilikuwa na washikaji
Ikaenda saa sita kulikuwa na vikao vya dharula kazini nisamehe my wife
Ikafikia sasa anarudi asubuhi ooh nilikuwa night shift siku hizi nimekuwa potential sana kazini wife
Ghafla picha ya mrembo mmoja kwenye screen ya simu..oops
Simu inakumbatiwa wakati zamani ilikuwa inakaa popote pale
Mara trip za hapa na pale zikaendelea

Vunja kazi mzee kamtakia wife Mie bila kumuoa huyo dada wa kwenye screen ya simu nitajiua ..makubwa ……
***Based on true story ****
Jamani tuendelee kuwaweka kwenue maombi wenza wetu
Tuziombeee ndoa na familia zetu
Amani itawale daima

Nawakilisha

FL1- Mama Mwenye Nyumba
huyo mama aliyetendwa angepewa ile namba ya hule mlokole aliyeonyeshwa mchumba ahangaike nae
 
wanaume kitu gani bwana...upuuuzi mtupu..
smile nakuelewa we na wanawake wenzako mnapowachukia wanaume....haswa pale mnapokuwa mmetendwa kwa njia moja au nyingine.....Ebu soma hapa chini ushuhuda wa mwenzako (mdada kama wewe) wa humu humu JF ambae naye alifanywa vibaya na wanaume...tena mdada mwenyewe msomi tu..graduate wa udsm.....ebu msome hapa chini ujumbe wake kwangu (nime quote)....ukisoma hii maneno waweza kweli kuwachukia sana wanaume....

Soma hii "habari yako bwana,
samahani naomba tu nikuibie kitu, hapa nilipo nina nina mimba ya miezi minne na mwanaume aliyenipa mimba kanikataa na bad enough kumbe ameoa na akuniambia kama kaoa na nimekuja kujua baada ya kumwambia nina mimba akanikatalia na akaniambia nikatoe mana ameoa na awezi kuwa na mtoto nje ya ndoa.
nimekataa kutoa na mpaka sasa hivi nina mimba na yule mwanaume haniudumii kwa lolote amekata mawasiliano kabisa.
kwetu mimi ni 1st born na ni msichana peke yangu nina wadogo zangu but wote ni wavulana, nimemaliza chuo but ndo naangaika kutafuta kazi ili niweze kumlea my baby vizuri zaidi.
so ninavyosema i real mean it , namaanisha kweli from my heart. hope umenielewa.
jioni njema buddy."
 
Dah Kaunga kumbe una shemeji hapa JF tetetetet congrats madame

Nimembahatisha leo, yaani full shangwe! Mwanaume faithful, mwanaume decent, mwanaume full maconfidence. Yaani kupendwa raha, hasa unapojitambua uko peke yako! LOL

Kongosho kimemuuma mpaka basi!
 
Last edited by a moderator:
FL1,am here,yaani we acha tu!I realy love her!Sijui nilichelewa wapi!

hata hujachelewa ulipoanzia ndo hapo ulipotakiwa kuanzia Eiyer all the best
 
Last edited by a moderator:
hata hujachelewa ulipoanzia ndo hapo ulipotakiwa kuanzia Eiyer all the best

Una akili wewe; ni kweli this is the right time; maana nilihitaji kupitia magumegume ili nimiappreciate my sweet Eiyer.

Eiyer dearest, yaani leo nitakuota kwa jinsi ulivyo kwenye mawazo yangu na mtima wange!

Mwaaah!
 
Last edited by a moderator:
hata hujachelewa ulipoanzia ndo hapo ulipotakiwa kuanzia Eiyer all the best

Asante FL1,Kaunga my love i realy love u!Achana na akina The Boss na Aprini,hapa unafunua mwenye raha na unajipimia peke yako!Only u!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom