Nilishawahi kusema hapa wakati fulani kwamba wanawake wengi wanaumia kwenye ndoa kwa sababu ya kuwasifu waume zao kwa mashoga kupita kiasi, si vibaya kumsifia mumeo kwa mashoga lakini pale yanapotokea mabadiliko kama haya usione aibu kusema umeshindwa na kuangalia mustakabali wako upya, kila mtu ameoa au kuolewa kwa utashi wake na hamna sababu ya mahusiano yenu au ndoa yenu kushikiliwa na majirani, marafiki au ndugu, kama yamekushinda bwaga manyanga anza maisha mapya, mambo ya kuanza kuwaza eti,...... "hivi majirani, ndugu au marafiki watanionaje?" yamepitwa na wakati, ndoa ni yako na sio ya kwao, anayeumia ni wewe na wala sio wao, na kama wakikuzodoa kwa kukusimanga wakikwambia ........ "kiko wapi ulichokuwa ukiringia...." Wao haiwahusu kwani wao wana maisha yao na wewe una maisha yako, kama alikuwa na tabia nzuri ni wakati ule,.......... Sasa kama amebadilika na kuwa na tabia za kiasherati wewe ufanye nini.......? Mtu hukuzaliwa naye tumbo moja, amelelewa kwao na wewe umelelewa kwenu, mmekutana ukubwani, kisa cha kutoana roho kwa sononi na msongo wa mawazo ni nini....!?
Kila mtu anaweza kuchukua ustaarabu wake kwani huo sio mwisho wa maisha.... na maisha ni popote, hata kama ukisemwa au kusengenywa na mashoga thamani yako iko pale pale wala haiondoki, ni wewe tu unayeweza kuiondoa kwa kujishusha na kujiona dhalili mbele ya binadamu wenzio..............