Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Mjadala kuhusiana na Serikali ya Tanganyika ni mjadala wa muda mrefu sana. Awali, mjadala huu ulikuwa ni wa chini chini kutokana na hofu iliyotanda ambapo kitendo cha kujadili au kuhoji "nafasi ya Tanganyika" ndani ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kilichukuliwa karibia sawa na kosa la uhaini. Lakini chini ya mazingira mapya ya kidemokrasia nchini kuanzia mwaka 1992 (demokrasia ya uliberali), umma umekuwa unazidi kupata fursa ya kujadili kwa uwazi zaidi nafasi ya Tanganyika ndani ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, uliozaliwa Aprili 26, 1964, tarehe ambayo ndio Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar) ilizaliwa. Pamoja na umma kuzidi kupata fursa hii, kuna tatizo moja linalojitokeza - nalo ni aidha kwa makusudi au kwa kupotoshwa, sehemu kubwa ya umma kujadili mgogoro wa muungano kwa kuegemea zaidi upande kwamba kiini chake ni the "zanzibar question" wakati ukweli uliopo ni kwamba chanzo kikuu cha mgogoro wa muungano ni the "Tanganyika Question".

Ifikapo mwaka 2014, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar) itakuwa inaadhimisha miaka 50 tokea kuzaliwa kwake. Kwa kipindi karibia chote cha muungano, kuna suala moja ambalo pande zote za mjadala juu ya mfumo sahihi wa muungano pamoja na hatima ya muungano hazina budi kulikubali. Suala hili ni Kwamba, tunakaribia kuadhimisha miaka 50 ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) katika hali iliyotawaliwa zaidi na "Crisis and Instability" kuliko "Progress and Stability". Ni hali hii ambayo ina chimbuko la KIKATIBA, ndio imekuwa ikitishia uhai wa Muungano wetu kwa miaka zaidi ya 40 sasa. Swali linalofuatia hapa ni je, nini ni chimbuko la wananchi wa Tanganyika na wananchi wa Zanzibar kufarakana, je ni:

· Siasa zaidi?
· Uchumi zaidi?
· Jamii zaidii?
· Mchanganyiko wa yote haya matatu?
· Mchanganyiko wa baadhi ya haya?

Majibu kwa swali hili yanaweza kuonekana ni rahisi kuyapata lakini kwa jinsi tunavyozidi kuirudia historia ya Tanganyika na Zanzibar, ndivyo tunavyoweza baini kwamba kupatia majibu yaliyojitosheleza swali hili sio jambo rahisi kama tungevyopenda kufikiri. Lakini jinsi mtu unavyozidi kutafakari, ndivyo unavyoweza kugundua jinsi gani "siasa" zinavyochukua sehemu kubwa kama chanzo cha mfarakano huu. Ushirikiano na uhusiano baina ya wakazi wa Tanganyika na Zanzibar haukuletwa na muungano wa 1964 kwani wakazi wa pande hizi mbili wamekuwa na ushirikiano wa muda mrefu sana, wa vizazi na vizazi. Uhusiano na Ushirikiano huu ulijengwa na bado unajengwa na udugu wa damu, historia, ujirani na muingiliano wa kijamii na kiuchumi, vizazi na vizazi. Kwa maana hii, ni rahisi kubaini kwamba uhusiano na ushirikiano huu wa kiuchumi na kijamii ulionekana ni wa muhimu kwa wakazi wa pande zote hizi mbili vizazi na vizazi kabla hata ya muungano kuzaliwa Aprili 26, 1964. Muhimu zaidi ni kwamba, uhusiano na ushirikiano huu uliweza kumudu mikiki mikiki yote ya tawala za Ureno, Ujerumani, Uingereza na Uarabu, kwa nyakati tofauti. Maswali yanayofuatia ni Je:

· Kwanza, Kwanini Uhusiano na Ushirikiano wa KIUCHUMI na KIJAMII baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar haukuingia dosari yoyote kubwa kwa kipindi kirefu sana Vizazi na Vizazi, lakini uhusiano huo uje kuingia dosari ndani ya kipindi kifupi sana ambacho bado hata hakijakamilisha kizazi kimoja (miaka 50), kutokana na sababu za KISIASA?

· Pili, tunajisikiaje iwapo tunatambua fika kwamba mahusiano yetu ya KIUCHUMI NA KIJAMII yaliweza kudumu kwa muda mrefu licha ya jamii zetu kupitia dhoruba kali zilizotokana na hila za tawala za Ureno, Ujerumani, Uarabu, Uingereza (kwa vipindi tofauti), only kuja kuwa ‘caught up' na SIASA, ambazo zinatishia kuharibika kwa mahusiano haya, tena ndani ya kifupi tu?

Ni muhimu tukautazama muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kwa mapana na marefu. Tusiuangalie muungano huu kwa sura ya kisiasa bali tuutazame kama ni uhusiano na ushirikiano wa vizazi na vizazi, hasa Kiuchumi na Kijamii kama nilivyojadili awali. Ni muhimu pia tuelewe kwamba, per articles of the Union (1964), hakuna chochote kipya kilicholetwa mezani zaidi ya jitihada za kuhalalisha sasa rasmi na kwa mujibu wa sheria (Mkataba wa Muungano, 1964), mahusiano yaliyokuwepo kwa vizazi na vizazi kabla hata ya Muungano wa 1964. Ni kutokana na ukweli huu, ili sasa kuhalalisha mahusiano ambayo yalikuwepo tayari, Mkataba wa Muungano (1964) ukaja na nguvu ya kisheria kwa kulenga masuala kumi na moja tu ambayo sasa ndiyo yakakubaliwa Rasmi na kwa Mujibu wa Sheria, ndiyo yawe maeneo ya uhusiano na ushirikiano, na mengine yaliyosalia, yaendelee kuwa chini ya mamlaka ya dola mbili husika (Tanganyika na Zanzibar) kama ilivyokuwa kabla ya muungano. Masuala yaliyokubaliwa yawe ya ushirikiano na uhusiano rasmi kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, kabla ya kiini macho kuanza kipindi kifupi kilichofuatia, yalikuwa ni masuala kumi na moja kama ifuatavyo:

1. Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya nchi za nje.
3. Ulinzi.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na Biashara ya nje.
9. Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha, na
11. Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa Anga, Posta na Simu. Na Bunge na serikali vilivyotajwa kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kwa mambo yote juu na kwa ajili ya Tanganyika.

Ukitizama masuala haya kumi na moja kwa umakini, sio vigumu kuelewa kwamba hapakuwa na lolote jipya na la ajabu zaidi tu ya kuufanya uhusiano na ushirikiano baina ya watu wa pande hizi mbili, uhusiano ambao tayari ulikuwepo vizazi na vizazi, sasa kuufanya uwe rasmi na kwa mujibu wa sheria na kwa faida ya pande zote mbili.

Hivi karibuni kumekuwa na nukuu za Mwalimu Nyerere zikitembea, ziinazojadili kwamba "Tanganyika ni sumu Kwa Muungano". Kuna dalili kwamba, kwenye mchakato wa Katiba Mpya, hoja hii ya Mwalimu Nyerere itachukuliwa kama ndio msimamo rasmi wa CCM na Serikali yake na itatumiwa na CCM katika kutetea Sera yake ya mfumo wa Serikali mbili ambayo kiini chake ni Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, na Katiba ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa kufuatia ndoa baina ya TANU na ASP, iliyopelekea Tanzania kuwa nchi inayofuata mfumo wa chama kimoja cha Siasa. Kuanzia 1977, CCM (sio Serikali au Bunge) ikachukua mamlaka yote juu ya masuala ya muungano, pamoja na masula yasiyokuwa ya muungano – yani masuala ndani ya Tanganyika na ndani ya Zanzibar.

Kama tupo sawa hadi kufikia hatua hii, nadhani sasa huu ni wakati muafaka wa kuhoji na kujadiliana kwa hoja maswali makuu yafuatayo:

· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?

· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?

Vijana wenzangu, sasa umefikia wakati ambapo wananchi wa Tanganyika (kama wenzetu wa Zanzibar walivyokwisha elimishwa), wanatuhitaji kuliko wakati mwingine wowote. Tuna wito wa kuwaelimisha watanzania wenzetu wasiokuwa na uelewa mkubwa juu ya kiini cha mgogoro wa muungano wetu pamoja na tiba ya mgogoro huu. Kufanya hivyo kutasaidia wananchi wa Tanganyika (ukipenda waite Tanzania bara) kwanza, wadai haki yao ya kupigia suala husika kura ya maoni (sio kupitia mabaraza ya katiba), na pili, wawe katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa lao (na Muungano wao), sio kwa manufaa ya wanasiasa.

Vijana wenzangu, tutumie mdahalo huu kutimiza wito huu muhimu sana kwa faida ya watoto, wajukuu na vitukuu vyetu huko mbeleni. Huu ni wito na wajibu wetu muhimu hasa sisi tulio bahatika kupata elimu, uelewa na upeo wa masuala kama haya kutokana na jasho la walipa kodi wa Tanganyika. Vijana hatuna budi kutimiza wajibu wetu muhimu wa kulipa fadhila kwa jamii ambayo kwa bahati mbaya, sehemu kubwa yake kubwa haipati fursa ya kuchambua na kuelewa suala hili ambalo ni muhimu sana kwa maisha yao na ya vizazi vyao vya baadae.

Tuepuke kurubuniwa lakini pia kupoteza muda wetu adimu kufarakana na wanafiki wa muungano wanaotumwa na nguvu za kisiasa na uchumi binafsi zaidi kuliko mapenzi na uzalendo wa taifa lao la Tanzania.

TUMESHATAMBUA KWAMBA BILA YA ZANZIBAR, TANZANIA HAIWEZEKANI. KWAHIYO NI MUHIMU TUKATAMBUA KWAMBA, PIA BILA YA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI.

Cc Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, EMT, AshaDii, JokaKuu, Nape Nnauye, Kobello, Kimbunga, FaizaFoxy, THE BIG SHOW, Barubaru, Zakumi SOBY, Mimibaba, Candid Scope, Mag3, Pasco, Bongolader, Ngongo et al.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu naomba mnisikilize:


Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!


Mimi nadhani kilichotufanya tuungane kwanza ni kutaka kuonesha njia kwa mataifa mengine ya Afrika. Kuonesha njia ambayo baadaye ingetufikisha pale ambapo Afrika nzima ingekuwa moja. Nyerere alikuwa na haki na wajibu wa kuipoteza Tanganyika ili kuidhihirishia Afrika na dunia imani yake kwenye Muungano wa Afrika! Kipindi kile ilikuwa ni sifa kubwa sana kupigania Umoja wa Afrika.


Sababu ya pili ilikuwa ni ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwa wakati ule!


Sababu zote hizo hapo juu hazina mashiko tena kwenye zama hizi za ubepari! Sasa kwa nini tuendelee kuishi imani zisizokuwepo!


Ikumbukwe kuwa zile juhudi za kuliunganisha bara la Afrika zilikufa hata kabla hazijafika mbali kwa sababu wengi wa waliokuwa wanaamini kwenye umoja wa Afrika walitoweka na mawazo yao!


Hata zile juhudi za kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki hazina uhai tena. Sisi ni mashuhuda wa kifo chake kitakatifu; tunasubiria tu kitangazwe rasmi siku za usoni!


Nauliza maswali hapa: Ni kwa nini kuwepo na muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine? Hata kwenye ndoa haiwezekani ndugu ni lazima walete chokochoko mwenzi mmoja akitoweka!
Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo! Ni kwanini nchi ijione haina uwezo wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?


Kama kujiendesha kwake ni kwa kutegemea taifa lingine haioni kuwa ina uhuru wa bendera tu?
Kama Zanzibar wa hofu wakiungana rasilimali zake kama mafuta n.k zitapotea; je, Tanganyika yenye gesi, mafuta, wanyamapori, makaa ya mawe, madini ndiyo iendelee kujitoa sadaka???! Basi Tanganyika itakuwa ni nchi nzuri sana ya kuishi kwa sababu haina hofu ya kuishiwa rasilimali!


Endapo atajitokeza mtu wa kuainisha pasipo shaka mipaka ya mapato na matumizi baina ya Tanzania Bara, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitafarijika sana! Nasema hivi kwa sababu ninachokiona mimi ni kuwa chochote kipatikanacho Tanzania Bara ni faida ya wote na cha Zanzibar ni kwa faida ya Zanzibar tu pekee.


Je, hii inaonesha kuwa Tanzania Bara inajiamini kuwa yenyewe ndiyo yenye uwezo wa gharamia serikali ya muungano na inaona fahari kufanya hivyo?! Au labda kuna masuala mengine Tanzania Bara inanufaika nayo ambayo sisi wananchi hatujui!
Je, Zanzibar nayo inaona fahari tu kuhudumiwa kila kitu kwenye muungano na wala haioni kuwa Tanzania Bara imebeba jukumu zito? Na je Zanzibar isipotimiziwa mambo kadhaa watakuwa radhi kulalamika ilhali wamebebwa katika mambo mengi?


Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharama kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!


Tusijidanganye; Tanzania ni jina! Nchi ni sisi wananchi! Na wananchi wa pande zote za Muungano wamechoka kulazimishiwa muungano wa serikali mbili! Tunaowaona wanatetea ni baadhi ya watawala ambao muungano uliopo sasa unawanufaisha kwa namna fulani.
Kama wananchi wengi wanadai muungano hauwatendei sasa inabidi tuseme imetosha tutafute kitakachotupa haki na usawa. Na hiki si kingine zaidi ya nchi zote kuungana na kuwa chini ya serikali moja itakayohakikisha kila raia anakuwa na haki sawa na mwenzake bila kujali atokako!


Ingependeza tuwe na serikali tatu kila nchi ijihudumie kwani kila nchi ilidai uhuru ili iwe huru! Lakini watu wanaeneza mawazo hasi ya ukubwa wa gharama!Umaskini na uvivu wa fikra! Ikumbukwe chochote kizuri ni sharti kiwe na gharama yake; tena gharama kubwa!
Kama tunakimbilia unafuu wa serikali mbili tufahamu wazi kuwa nafuu mara zote ni ghali zaidi na mara zote hazidumu!


Muungano wa serikali mbili vilio vya unyonyaji! Muungano wa serikali tatu tunaogopa gharama! Basi muungano unaotufaa ni wa serikali moja. Kama hatuwezi muungano wa serikali moja, muungano wowote ule utakaokuwepo aidha wa serikali mbili, tatu au zaidi hautatuliza kiu ya wananchi! Narudia tena: Tanzania ni jina; nchi ni wananchi!


Nashangaa nchi zenye watu zinaogopa kujiwekea mifumo ambayo itawastawisha na kumaliza chokochoko kwa visingizio visivyoisha! Ina maana pamoja na rasili mali tulizonazo viongozi wetu wanataka kututhibitishia kuwa hawawezi kuweka mifumo ya kuliendesha taifa kwa ustawi!


Hoja ya kuwa kuna udugu wa damu kati ya Tanganyika na Zanzibar ni hoja ya kibaguzi kwani uhusiano wa damu upo pia baina ya Tanganyika na nchi nyingine. Swali hapa: Ni kwa nini tusiungane na Kenya, Uganda, Msumbiji, Burundi, Malawi, Zambia, n.k kwa sababu hata huko wapo watanganyika wana ndugu zao?
Kama hoja ni udugu ni kwanini Zanzibar wanapochagua wabunge wa kuja kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano, upande wa Tanzania Bara nao wasichague wawakilishi wachache kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuukuza zaidi huo unaoitwa udugu???
Udugu unaonufaisha upande mmoja zaidi ya mwingine si mzuri jamani! Tuache propaganda. Kama tunaamini umoja ni nguvu utengano ni udhaifu basi tuungane tuwe nchi moja, serikali moja, rais mmoja na Tanzania moja ili tuwe ndugu kweli!


Watasema ni chuki lakini kama hatuwezi kumaliza tofauti zetu kwa kuunda serikali tatu au moja basi ni bora kila nchi ijendee kivyake! Hata Kenya na Uganda ni ndugu zetu lakini hatujaugana nao kutengeneza taifa la kusadikika!


Litakuwa ni kosa sana kuendelea kuwa na muungano ambao upande wa Tanganyika tu ndiyo unaendelea kupoteza historia yake wakati mshirika wake Zanzibar akibakiwa na ziada hata kama ni sawa na wilaya moja ya Tanganyika!


Wakuu; naombeni kuwasilisha hoja!
 
Watanzania bara wamevumilia maneno ya baadhi ya visiwani kuwa wananyonywa kwa muda mrefu sana, tokea 1964 mpaka muda huu. Mimi nafikiri tufanye haki ambayo baadhi ya wana visiwani wanataka, TURUDISHE TANGANYIKA kama vile ZANZIBAR ilivyo hai.

Mfumo si suala la majadiliano...lakini kwa ukubwa, kwa uchumi Serikali ya Tanganyika ndio itakayokuwa na nguvu, hili nalo litazamwe...wale wenye ndoto za mchana watakuja na povu hapa...Au kama wazo hili linapingwa basi kuwe na SERIKALI MOJA TU
 
utafikiri mbunge unawasilisha hoja bungeni kusikofikika sauti yako wala kuonwa
Wakuu naomba mnisikilize:


Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!
 
Kwako wewe unaejiita Mchambuzi,

Huu Muungano una faida gani kwa Zanzibar na Tanganyika, oops, hakuna nchi iitwayo Tanganyika, (Tanzania bara)?

Niliuliza swali kama hilo kwenye nyuzi yako nyingine inayoongelea huu huu Muungano.

Naona umekuja na pumba zingine kibao lakini maswali ya msingi unayakwepa.
 
Mkuu Mchambuzi wanasiasa wengi hasa wa CCM hawapendi uwepo wa Tanganyika na ikifika sehemu wanayolazimika kuizungumzia wanatupachika jina la Tanzania bara wanasahau Tanzania Bara ina visiwa vya Mafia na visiwa vingine vingi.Wanasiasa wengi wa Tanganyika wanajua hakuna madhara ya kisiasa unapoikana Tanganyika kwakuwa watanganyika wenyewe bado hawajaiona thamani ya nchi yao inayoitwa Tanganyika na si Tanzania Bara.Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini unashangaa Zanzibar ipo Tanganyika haipo kwanini na kwa faida ya nani nalo ni swali la kutafakari.

Kati ya mambo ambayo sikuwahi kukubaliana na Mwl Nyerere ni hili suala la muungano.Mwl Nyerere alikuwa mwanasiasa mahiri mwenye ujuzi mkubwa wa kufafanua jambo ambalo wanasiasa wengine wasingeweza lakini mpaka leo kila nikipitia hotuba zake kuhusiana na muungano hazinishawishi hata kidogo.Hili ni moja ya maeneo ambayo Mwl Nyerere alitumia udikteta zaidi ya nguvu ya hoja.Wapo wanasiasa wengi waliojikuta wakianguka katika ulingo wa siasa kwasababu ya kujaribu kuboresha au kuhoji muungano.Mpaka leo sijaona kosa la Malecela na Aboud Jumbe zaidi ya udikteta wa Mwl Nyerere linapokuja suala la muungano.

Ni wazi waTanganyika wengi hawajali uwepo wa taifa lao labda kwasababu ya udogo wa Zanzibar.Sidhani kama Tanganyika ingeungana na Kenya halafu Kenya ikabakiza jina na utaifa wake ,bendera yake,wimbo wake wa taifa,rais wake na uraia wake halafu waTanganyika wakapuuza wakadhani hilo si tatizo !.Udogo wa Zanzibar kwa maana ya idadi ya watu wake,ukubwa wa eneo lake umewafanya waTanganyika wachelewe kudai haki zao za msingi ikiwemo utaifa wao.Utashangaa zaidi utakapobaini JMT ina utaifa mara mbili.Kuna mtanzania ambaye ni mtanganyika na mzanzibar halafu kuna uraia wa Zanzibar ambao unamweka kando mtanganyika.

Tukitaka kujadili katiba ya JMT ni lazima kwanza tujadili katiba ya Tanganyika.Zanzibar wanayo katiba yao kwanini inakuwa nongwa upande wa Tanganyika ?.
 
Kwako wewe unaejiita Mchambuzi,

Huu Muungano una faida gani kwa Zanzibar na Tanganyika, oops, hakuna nchi iitwayo Tanganyika, (Tanzania bara)?

Niliuliza swali kama hilo kwenye nyuzi yako nyingine inayoongelea huu huu Muungano.

Naona umekuja na pumba zingine kibao lakini maswali ya msingi unayakwepa.
Ahlaan wasalan!!, I thought you've moved on to better things.

Umesoma uzi wote? Au umekurupuka maana sababu na faida amezitaja.

Karibia mtapata mnachotaka, kwa sababu karibia nasi tutapata tunachotaka.
 
Ahlaan wasalan!!, I thought you've moved on to better things.

Umesoma uzi wote? Au umekurupuka maana sababu na faida amezitaja.

Karibia mtapata mnachotaka, kwa sababu karibia nasi tutapata tunachotaka.

Tazama vizuri swali langu.
 
Nimelitazama vizuri sana, je wewe umesoma uzi huu wote? Hilo ndiyo la muhimu zaidi.

Huu uzi pamoja na hiyo yako una posts 10 tu, nimeupitia tena wote kwa mara ya pili, sikuona jibu la swali langu hata moja. Upo hapo ulipo?
 
Huu uzi pamoja na hiyo yako una posts 10 tu, nimeupitia tena wote kwa mara ya pili, sikuona jibu la swali langu hata moja. Upo hapo ulipo?
Nipo!

Rudia kusoma aya (paragraph) ya nne, mstari wa sita na kuendelea.Post #1 .
Je, upo???
 
Nipo!

Rudia kusoma aya (paragraph) ya nne, mstari wa sita na kuendelea.Post #1 .
Je, upo???

Kama wewe umeliona libandike hilo jibu hapa, mimi sikuliona, yanini unaandikia mate na wino upo?
 
Kama wewe umeliona libandike hilo jibu hapa, mimi sikuliona, yanini unaandikia mate na wino upo?
Haya, soma hapo chini.

ushirikiano wa muda mrefu sana, wa vizazi na vizazi. Uhusiano na Ushirikiano huu ulijengwa na bado unajengwa na udugu wa damu, historia, ujirani na muingiliano wa kijamii na kiuchumi, vizazi na vizazi. Kwa maana hii, ni rahisi kubaini kwamba uhusiano na ushirikiano huu wa kiuchumi na kijamii ulionekana ni wa muhimu kwa wakazi wa pande zote hizi mbili vizazi na vizazi kabla hata ya muungano kuzaliwa Aprili 26, 1964. Muhimu zaidi ni kwamba, uhusiano na ushirikiano huu uliweza kumudu mikiki mikiki yote ya tawala za Ureno, Ujerumani, Uingereza na Uarabu, kwa nyakati tofauti
 
i liked this....
"... Kufanya hivyo
kutasaidia wananchi wa
Tanganyika (ukipenda waite
Tanzania bara) kwanza, wadai haki
yao ya kupigia suala husika kura
ya maoni (sio kupitia mabaraza ya
katiba), na pili, wawe katika nafasi
nzuri zaidi ya kufanya maamuzi
kwa manufaa ya Taifa lao (na
Muungano wao), sio kwa manufaa
ya wanasiasa ....."
 
Jp Omuga,

Asante kwa mchango wako mzuri; Una hoja nyingi za msingi lakini naomba nizijadili moja baada ya nyingine kwa jinsi tunavyoendelea na mjadala wetu; Naomba nianze kwa kusema kwamba - sababu kubwa kwanini nimekuja na mjadala huu ni kujaribhu kubaini upande upi wa hoja una nguvu zaidi baina ya:

Kuikubali Tanganyika ni sumu ya Muungano

Dhidi ya hoja:

Kuikataa Tanganyika ni sumu ya Muungano;

Lengo hapa ni kujaribu tupate makundi mawili/pande mbili za hoja na kusikia kila upande una hoja zipi; Nilishawishika kuja na mada hii baada ya kuona bandiko la kijana mwenzetu Nape Nnauye, Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Uenezi CCM (Taifa), ambae hivi karibuni alikuja na nukuu ya mwalimu kwamba "Serikali Ya Tanganyika ni Sumu ya Muungano." Kuna ishara kubwa kwamba bandiko la Nape Nnauye maana yake ni kwamba huo ndio utakuwa msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na muundo wa Muungano wetu katika muktadha wa Katiba Mpya.

Licha ya umuhimu wa nukuu hii ya Mwalimu kupitia Nape, kwa bahati mbaya, Nape hakurudi kujadili hoja yake licha ya watu wengi kujadili nukuu husika ya mwalimu kwa hoja mbalimbali; Lakini licha ya Nape kutoweka katika mjadala, wengi tulijaribu kuendelea kujadiliana kuhusiana na suala husika kwani ni sehemu muhimu sana ya mchakato wa katiba mpya, lakini kwa bahati mbaya (again), Mods wa Jamiiforums waliutoa uzi ule wa nape kuhusiana na nukuu ya Mwalimu na kuunganisha na uzi mwingine wa siku nyingi wa mdau mwenzetu Willy Gamba, kitendo ambacho kikapelekea mjadala juu ya uzito wa nukuu ya mwalimu per Nape and potential position ya CCM kuelekea katiba mpya, kutoweka; Haya ndio yamenisukuma nije na uzi mpya ambao utatupatia fursa ya kujadiliana kwa kina kuhusiana na nukuu ya mwalimu kwamba Serikali ya Tangayika ni sumu kwa muungano, huku tuki bear in mind kwamba inawezekana hiyo pia ikawa ndio established position ya CCM katika muktadha wa Katiba Mpya ya JMT; Kama tupo pamoja, nadhani sote mtakubaliana nami kwamba hili ni jambo zito ambalo linahitaji uzi unaojitegemea, hasa iwapo nukuu za Baba wa Taifa ambae mara nyingi alikubali kuteleza kwenye mengi, anatumika kama njia ya kushawishi watanzania wafikie maamuzi katika muktadha muhimu kama huu wa Katiba Mpya;

Vile vile, naomba niseme hapa kwamba hakuna ubishi kwamba mijadala juu ya Tanganyika humu JF ni mingi, hivyo kufikia near saturation point; Pamoja na umuhimu wa mijadala hii, moja ya mapungufu yake imekuwa ni kwamba - mijadala mingi imekuwa stimulated na haja ya kurudisha serikali ya Tanganyika kwa sababu - aidha wenzetu wazanzibari wao wamechukua uamuzi wa kuelekea kuwa dola kamili au kwa sababu serikali ya muungano inazidi kuwa mzigo kwa upande wa Tanganyika; Pamoja na uzito wa hoja mbalimbali kuhusiana na haya, kuna uhaba mkubwa wa mjadala unaoangalia Tanganyika per se. Swali linalofuatia hapa ni kwamba:

· Hivi ni sawa kwa mijadala juu ya Serikali Ya Tanganyika kuibuka pale tu Wazanzibari wanapo amka kutaka uhuru wao kidola na sio wakati wowote mwingine?

Kwa mfano, in the 1990s, hoja ya Tanganyika iliibuliwa na kundi la wabunge (G55) baada ya sakata la Zanzibar na OIC, na mara baada ya Baba wa Taifa kufanikiwa kuizima hoja ya Zanzibar na OIC, (nje ya mtikila) hakuna mtanganyika aliyeendelea kuona umuhimu wa serikali ya Tanganyika, huku lawama ya mgogoro wa muungano ukielekezwa kwa wazanzibari;

Miaka mingi baade kufuatia sakata la OIC kumalizika, mjadala wa Tanganyika umeibuka tena, na sio kwa sababu ya watangayika kudai Tanganyika yao on merit, bali kutokana na Zanzibar kuamua kuanza safari ya kuwa Dola kamili Per Katiba ya Zanzibar (2010); Kutokana na hili tena, Watanganyika wameibuka tena na kudai ‘kilicho chao'; Tafsiri juu ya hili ni nyingi miongoni ikiwa ni:

· Kwanza, kumbe Cha watanganyika kinakuwa cha watanganyika pale tu wazanzibari wanapodai cha wazanzibari; Kumbuka, mfumo uliodhamiriwa wa shirikisho chini ya mkataba wa muungano 1964 ulilenga yawepo ya wazanzibari, ya watanganyika na yakuchangia wazanzibari na watanganyika;
· Pili, kumbe Serikali ya Tanganyika IPO, ila inafichwa na kiini macho; Tazama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoteua mawaziri wa wizara za muungano na wizara zisizo za muungano – za Tangayika (Afya, Elimu, Kilimo n.k) na pia wakuu wa taasisi za muungano na zile za Tanganyka tu; Upande mwingine wa muungano, Rais wa Zanzibar nae anaunda vyombo vya kuendesha dola ya Zanzibar; Jamani, kwa miwani ya ujana isiyohitaji miwani, hatuoni in practice zipo serikali tatu kwa miaka karibia 50 sasa? Ndio maana nazidi kusisitiza kwamba hoja kwamba serikali tatu ni gharama ni hoja mufilisi kwani gharama zimekuwepo kwa miaka 50 ya muungano, na gharama hizi ni kubwa zaidi kutokana na juhudi za kuficha kiini macho "kitaasisi", wakati zingekuwa ndogo zaidi iwapo kiini macho husika kingeondolewa; Na
· Tatu, kumbe umuhimu wa Tanganyika unakuwa mkubwa zaidi kwa watanganyika pale tu wenzetu wazanzibari wanapodai uhuru wao wa kidola, uhuru ambao ndio uliodhamiriwa chini ya Mkataba wa Muungano, 1964; Hii inaendanana tafsiri ya kwanza hapo juu;

Swali muhimu linalofuata ni je:

· Kwanini watanganyika hawaoni umuhimu wa kudai Tanganyika yao bila ya kuhusisha maamuzi ya wenzetu wazanzibari?

Hii ni ajabu, hasa ikizingatiwa kwamba:

· Kwanza, wanachofanya wazanzibari ndicho kilichokubaliwa chini ya Mkataba wa muuungano, 1964, juu ya uwepo wa masuala ya muungano na yasio ya muungano – kwa maana hii, ya Zanzibar nay a Tanganyika;
· Pili, wanachofanya wazanzibari ndicho ilitakiwa na sisi watanganyika tukifanye miaka 46 iliyopita ambapo Tanganyika ilifutwa rasmi kwa mujibu wa sheria namba 24 ya mwaka 1967.

Kama hadi hapa tupo pamoja, niulize swali lingine:

· Kwanini kitu kilichofutwa kimaandishi kwa mujibu wa sheria namba 24, 1967 (Tanganyika), lakini bado kipo in practice (rejea mjadala juu ya uteuzi wa Rais wa JMT wa wizara na taasisi nchini hapo juu) – kwanini kiitwe sumu badala ya kiini macho?

Mkataba wa muungano, 1964 ulidhamiria ushirikiano wa mambo kumi na moja tu, huku mengine yote yakibakia kwa watanganyika na wazanzibari; Kwa maana nyingine, sumu ya muungano sio serikali ya Tanganyika bali ni Katiba ya muda ya JMT (1965) na Katiba ya sasa ya JMT (1977) ambazo ndio zimezaa kiini macho cha Muungano, na kupelekea watanzania wengi kutojua kiini cha tatizo kipo wapi, suala ambalo ndio furaha ya watawala; Inasikitisha kwamba tunajaribu kukwepa accountability ya mgogoro wa muungano, hasa kwa kuigeuza dawa kuwa sumu ya muungano (Tanganyika); Kutokana na dynamics za dunia ya leo, nina uhakika karibia wa 99% kwamba kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai leo, angebadili mtazamo wake juu ya Tanganyika, kama vile alivyobadili mtazamo wake juu ya CCM ambapo alifikia hatua ya kusema "CCM SIO MAMA YAKE, ANAWEZA ACHANA NAYO";

Haya ni baadhi tu ya masuala ambayo nililenga tuyajadii kwa kina katika mjadala wetu huu; Vinginevyo sote tunaelewa kwamba mijadala ya Tanganyika humu JF imeshakuwa mingi kiasi cha kufikia saturation point; Na tukijisahau na kutoka kwenye mada, tutapoteza fursa muhimu sana ya kujadili suala hili muhimu kwa mustakabali wa taifa letu la leo na kesho (rejea kichwa cha uzi huu); Baada ya kusema hayo, naomba sasa niende moja kwa moja katika maswali yako muhimu sana kwenye bandiko lako #2 la uzi huu:

· Kwanini kuwepo muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine?

Naomba nijibu swali lako la kwanza kama ifuatavyo:

Aliyekubali kupoteza ni Tanganyika, sio Zanzibar; Turejee historia kidogo: Tanganyika ilifutwa rasmi kwa mujibu wa sheria namba 24 ya Bunge mwaka 1967, na kupewa jina jipya la "Tanzania Bara"; Licha ya hili kutokea, hakuna mtanganyika (wapo wazanzibari wachache walio ona tatizo) aliyeona kwamba hatua hii ni ujenzi wa mgogoro mkubwa siku za mbeleni, kwani ulikuwa mwanzo wa uvurugaji wa makubaliano ya muungano kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, (1964); Licha ya haya, bado tuliweza kukaa bila mgogoro mkubwa kwa miaka 13 (1964 – 1977) sababu kubwa ikiwa ni kwamba – nchi ilikuwa chini ya Katiba ya Muda (1965 – 1977), hivyo kutoa fursa ya kuahirisha mgogoro wa muungano;

Sababu kubwa ya Katiba ya Muda ilikuwa ni kwamba – uongozi wan chi ulipata wakati mgumu kuja na muundo wa serikali nje ya ule uliokusudiwa chini ya Mkataba wa muungano, 1964 (serikali tatu) bila ya kuleta mgogoro wa muungano; Baada ya miaka kumi na mbili (1965 – 1977), uongozi ukapata jibu ambalo assumption yake ilikuwa – mfumo wa Chama Kimoja ungedumu milele Tanzania, hivyo kuviuguanisha vyama vya TANU (cha Tanganyika) na chama cha ASP (cha Zanzibar) kuwa chama kimoja cha CCM (1977); Sambamba na hili, CCM ikasimamia mchakato wa Katiba ya JMT (1977) ambapo muswada wa katiba mpya ulipelekwa bungeni, ukajadiliwa kwa siku moja tu na kupitisha; Chini ya Katiba mpya ya JMT (1977), chama cha CCM kikapewa mamlaka makubwa kuliko Serikali na Bunge, hasa katika kusimamia, kuratibu na kuendesha masuala ya Muungano na masuala yasiyokuwa ya muungano – yani ya Zanzibar (Tanzania Zanzibar) na ya Tanzania Bara (Tanganyika);

Tufahamu pia kwamba Katiba ya JMT (1977) ililizika rasmi utambulisho wa Zanzibar na sasa ikaitwa Tanzania Zanzibar, huku Tanganyika yeye tayari akiwa na mazoea juu ya kufutiwa utambulisho wake wa Tanganyika kwa miaka 12 sasa (rejea sheria namba 24, 1967 iliyoua Tanganyika na kuzalisha Tanzania Bara); Sasa napojenga hoja kwamba aliyekubali kupoteza ni Tanganyika na sio Zanzibar, hii ni kwa vile ilichukua miaka miwili tu kwa Zanzibar kugundua tatizo lililopo kwani mwaka 1979 tunaona Zanzibar wakihamaki warudishiwe utambulisho kwani miaka miwili baada ya kuzaliwa kwa katiba ya JMT (1977)m Zanzibar wakagundua mapungufu ya katiba hii hivyo kuja na katiba yao ya kwanza mwaka 1979, Katiba ya kwanza kwa taifa la Zanzibar tangia mapinduzi yao ya mwaka 1964; Hii ilikuwa ni hatua ya Zanzibar kujiweka sawa dhidi ya katiba mbovu ya JMT (1977), lakini walitaka kufanya mambo kwa hatua na umakini mkubwa, hasa wakilenga kufanya maamuzi kwa mujibu wa mkataba wa muungano, 1964;

Ilipofika mwaka 1984, Zanzibar ikaingia katika awamu yake ya pili ya kujirudishia utambulisho wake uliopotezwa na katiba mbovu ya JMT (1977) ambapo walirudisha rasmi utamblushi wao wa Zanzibar na kuufuta ule wa Tanzania Zanzibar, kwani Muungano wa 1964 haukuwa baina ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, bali Tanganyika na Zanzibar; Mkataba wa muungano ulilenga muundo wa shirikisho la serikali tatu, sio serikali mbili kama Katiba ya JMT (1977) ilivyogeuza rasmi kufanya sera ya CCM kuwa ndio sheria ya muungano; Kwa upande wetu Tanganyika, kama kawaida yetu ni watu wa kulala na tukiamka, tunasingizia wenzetu wazanzibari kwamba ndio chanzo cha mgogoro wa muungano wetu, kwani licha ya mabadiliko haya ya Zanzibar yaliyoipatia Zanzibar Katiba yao, Tanganyika tuliendelea kuishi bila kuona tatizo la Katiba ya JMT kuwa ndio hiyo hiyo Katiba ya Tanganyika; Baadae Mchungaji Mtikila miaka ya tisini akaja na hoja ya Tanganyika, lakini kama kawaida, akijitokeza mtanzania na hoja ya maana lakini akawa hana ukaribu na watawala, haungwi mkono au hana ushawishi ndani ya ccm au hana madaraka makubwa, licha ya elimu, upeo na uelewa wake wa mambo, tumelelewa kumwona sio lolote bali mwehu, mwenye njaa, na mwenye wivu na walio madarakani; Hivyo ndivyo wengi walimwona mtikila; Lakini niseme tu kwamba utamaduni huu umeanza kutoweka chini ya mfumo wa vyama vingi, hasa kuanzia mwaka 2000;

Baadae pia tunaona kilio cha Tanganyika kikirudi tena kupitia G-55 bungeni, lakini kwa bahati mbaya, madai haya hayakuwa internal driven (kutokana na mahitaji ya watanganyika) bali external driven (kutokana na matendo/maamuzi ya wenzetu Zanzibar kuhusiana na OIC); Ndio maana nazidi kuhoji je:

· Ni kwanini wakati wote madai yetu juu ya Tanganyika huwa ni External driven na sio Internal driven?

Nikija kwenye swali lako la pili:
· Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo, wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?

Kwanza, ni muhimu nisema yafuatayo:

1. Siku ya Muungano, 26[SUP]th[/SUP] April 1964, Zanzibar ilikuwa ndio kwanza imejipatia uhuru wake. Zanzibar haikuwa na katiba yake bali mchakato wa katiba mpya ulikuwa katika hatua ya maandalizi – sio katiba ya JMT, bali Katiba kuendesha dola mpya huru ya Zanzibar;
2. Tofauti na Zanzibar, Tanganyika tayari ilikuwa na katiba yake iliyopatikana mwaka 1962; Hivyo mwaka 1964 (mwaka wa muungano), Tanganyika tayari ilikuwa na katiba yake kwa miaka miwili;

Kutokana na uhalisia huu, Mkataba wa Muungano (1964) ukaweka bayana kwamba, kwa vile katiba ya Tanganyika ipo, basi katiba hiyo ichukuliwe na kufanyiwa marekebisho katika vipengele kadhaa ili iwe ni Katiba ya Muda ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; In the meantime, Katiba ya Tanganyika (1962) iendelee kuwa Katiba ya Tanganyika, na Zanzibar nao waendelee na mchakato wa kujipatia Katiba yao kwa masuala nje ya yale yaliyokubaliwa yawe ya muungano (masuala kumi na moja – rejea bandiko namba moja hapo juu); Muhimu zaidi – Mkataba wa Muungano ukasema kwamba Marais wa Tanganyika na Zanzibar watateua tume ya kusimamia mchakato wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili - yani kabla ya Tarehe 26, April, 1965; Kilichofuatia kikawa ni kinyume kabisa na Mkataba wa Muungano, 1964):

· Kwanza, just before expiry date ya Marais wa pande mbili kuja na tume ya kuratibu katiba mpya na ya KUDUMU ya JMT per articles of the union (1964), badala ya tume hii, tunaona ujio wa Katiba ya MUDA (1965), kinyume cha makubaliano ya Mkataba wa Muungano (1964);
· Pili, Katiba ya Muda (1965) inamtangaza rasmi Rais wa Tanganyika kuwa ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Msisitizo hapa sio Urais wa JMT bali - Rais wa Tanganyika pia anakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Iwapo dola hiz mbili zilikuwa ni dola kamili na sawa, basi ilibidi siku moja, Rais wa Zanzibar awe pia Rais wa JMT; Lakini cha msingi hapa ni kwamba Tanganyika ikamezwa na Serikali ya Muungano, huku serikali ya Zanzibar ikiendelea kuwepo na masuala yake yaliyo nje ya muungano;
· Tatu, ili kuhalalisha kifo cha Serikali ya Tanganyika, miaka miwili baada ya ujio wa katiba ya Muda – yani mwaka 1967, Bunge likapitisha sheria namba 24 ambayo ilitanganza rasmi kwamba Utambulisho wa TANGANYIKA umefutwa rasmi, na badala yake eneo husika kuanzia 1967 kwa mujibu wa sheria namba 24, litaitwa TANZANIA BARA, huku Zanzibar ikiendelea kuitwa Zanzibar;

MUHIMU PIA:

Siku chache baada ya Muungano (1964), ilitolewa Amri ya Utaratibu wa Kipindi cha Mpito (a decree) ambayo sehemu ya tisa ikatoa amri kwamba masuala yafuatayo yaanze kutekelezwa mara moja:

"Mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya Tanganyika, na mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya watu wa Zanzibar zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au milikiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano, chini ya jamhuri ya muungano"

Hoja yangu ya msingi katika nukuu hiyo hapo juu ni kwamba – tunalizungumzia suala la Zanzibar kuwa tegemezi kwa Tanganyika bila ya kuwa na uelewa jinsi gani tumefikia hapo; Tufahamu kwamba, AMRI hiyo hapo juu ilitolewa miezi michache tu baada ya mapinduzi ya Zanzibar, katika kipindi ambacho wananchi wa taifa hili jipya na huru (Zanzibar) walikuwa ndio kwanza bado wanasafisha magwanda yao ya mapambano yaliyojaa damu ya ushindi katika harakati za mapinduzi mitaani, na dola hii huru (Zanzibar) ndio kwanza ilikuwa inajaribu kujiweka sawa katika dhamana zake mpya kama taifa huru, na hata hizo mali mpya zinazoamrishwa kupelekwa Tanganyika (kupitia serikali ya muungano ambayo rais wake pia ni rais wa Tanganyika), zikiwa hata hazijafanyiwa tathmini yoyote ya maana ili kubaini mchango wa Zanzibar katika Muungano ni upi; Tukumbuke pia kwamba miaka ya nyuma – kipindi kabla ya uhuru, Zanzibar ilikuwa ni moja ya maeneo makubwa kabisa ya kibiashara katika eneo la Afrika mashariki na kati, na uchumi wake ulikuwa at least on par level, kama sio zaidi ya maeneo mengi ya Tanganyika (including Dar-es-salaam);

Nitarejea kujadili hoja zako nyingine muhimu za bandiko #2 kama vile ndoto za Mwalimu Nyerere on United States of Africa n.k;

Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, EMT, AshaDii, JokaKuu, Nape Nnauye, Kobello, Kimbunga, FaizaFoxy, THE BIG SHOW,Barubaru, Zakumi SOBY, Mimibaba, Candid Scope, Mag3, Pasco, Bongolader, Ngongo et al.

 
Kwako wewe unaejiita Mchambuzi,

Huu Muungano una faida gani kwa Zanzibar na Tanganyika, oops, hakuna nchi iitwayo Tanganyika, (Tanzania bara)?

Niliuliza swali kama hilo kwenye nyuzi yako nyingine inayoongelea huu huu Muungano.

Naona umekuja na pumba zingine kibao lakini maswali ya msingi unayakwepa.

Kwako wewe unayejiita faizafoxy,

Pamoja na wewe kuamua kufumbia macho faida nilizojadili ( na kobello nashukuru kwa kumwelekeza eneo husika), uzi huu haulengi kujadii faida za muungano kwa Tanganyika na Zanzibar, bali unalenga kujadili maswali makuu mawili kama niliyoainisha kwenye bandiko namba moja, na ningependa kuyarudia tena:

· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?

· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?

Vinginevyo mjadala juu ya faida za muungano kwa Zanzibar na Tanzania bara (Tanganyika) ni mjadala ambao umeshakuwa exhausted vya kutosha humu JF kwani tumeshajadili sana hili (rejea hoja mbalimbali za watu kama Mzee mwanakijiji, nguruvi3, Joka Kuu n.k), na hoja karibia zote juu ya faida na hasara zimeshajadiliwa na kueleweka; Ukiamua kuzileta humu, zitakuwa na maana iwapo unalengo la kuzitumia kufafanua hoja zako kuhusiana na maswali yangu mawili hapo juu;

Karibu katika mjadala;
 
Kwako wewe unayejiita faizafoxy,

Pamoja na wewe kuamua kufumbia macho faida nilizojadili ( na kobello nashukuru kwa kumwelekeza eneo husika), uzi huu haulengi kujadii faida za muungano kwa Tanganyika na Zanzibar, bali unalenga kujadili maswali makuu mawili kama niliyoainisha kwenye bandiko namba moja, na ningependa kuyarudia tena:

· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?

· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?

Vinginevyo mjadala juu ya faida za muungano kwa Zanzibar na Tanzania bara (Tanganyika) ni mjadala ambao umeshakuwa exhausted vya kutosha humu JF kwani tumeshajadili sana hili (rejea hoja mbalimbali za watu kama Mzee mwanakijiji, nguruvi3, Joka Kuu n.k), na hoja karibia zote juu ya faida na hasara zimeshajadiliwa na kueleweka; Ukiamua kuzileta humu, zitakuwa na maana iwapo unalengo la kuzitumia kufafanua hoja zako kuhusiana na maswali yangu mawili hapo juu;

Karibu katika mjadala;

Kama haulengi kuongelea faida za Muungano huu uzi una faida gani? Waste of time and energy.

Sijaiona hiyo faida ulioongelea na wala Kobelo aliyoiongelea, kama iko iwekeni tena hapa tujadili faida za Muungano kama mmeshindwa, kwaheri na siku nyingine usinialike kwenye nyuzi ya Muungano kama haziongelewi faida zake.
 
Kama haulengi kuongelea faida za Muungano huu uzi una faida gani? Waste of time and energy.

Sijaiona hiyo faida ulioongelea na wala Kobelo aliyoiongelea, kama iko iwekeni tena hapa tujadili faida za Muungano kama mmeshindwa, kwaheri na siku nyingine usinialike kwenye nyuzi ya Muungano kama hauongelei faida zake.

Kabla ya kutuaga rasmi kwenye mjadala huu, per title ya thread husika, naomba kusikia mawazo yako juu ya haya:


· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?

· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?

Baada ya maoni yako juu ya haya, utakuwa umetutendea wema, hivyo kwenda zako...
 
Kabla ya kutuaga rasmi kwenye mjadala huu, per title ya thread husika, naomba kusikia mawazo yako juu ya haya:


· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?

· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?

Baada ya maoni yako juu ya haya, utakuwa umetutendea wema, hivyo kwenda zako...

Hakuna mada hapo. Nyerere kisha aga dunia na hakuna chenya maana alichokiacha duniani zaidi ya wanawe.

Naona hiyo "kwenda zako" ni hasira za kukwambia sina haja ya kujadili jambo lisiloongelea faida ya Muungano. Utakasirika sana. Jadili na Kobelo. Bye.
 
Back
Top Bottom