Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Mjadala kuhusiana na Serikali ya Tanganyika ni mjadala wa muda mrefu sana. Awali, mjadala huu ulikuwa ni wa chini chini kutokana na hofu iliyotanda ambapo kitendo cha kujadili au kuhoji "nafasi ya Tanganyika" ndani ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kilichukuliwa karibia sawa na kosa la uhaini. Lakini chini ya mazingira mapya ya kidemokrasia nchini kuanzia mwaka 1992 (demokrasia ya uliberali), umma umekuwa unazidi kupata fursa ya kujadili kwa uwazi zaidi nafasi ya Tanganyika ndani ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, uliozaliwa Aprili 26, 1964, tarehe ambayo ndio Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar) ilizaliwa. Pamoja na umma kuzidi kupata fursa hii, kuna tatizo moja linalojitokeza - nalo ni aidha kwa makusudi au kwa kupotoshwa, sehemu kubwa ya umma kujadili mgogoro wa muungano kwa kuegemea zaidi upande kwamba kiini chake ni the "zanzibar question" wakati ukweli uliopo ni kwamba chanzo kikuu cha mgogoro wa muungano ni the "Tanganyika Question".
Ifikapo mwaka 2014, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar) itakuwa inaadhimisha miaka 50 tokea kuzaliwa kwake. Kwa kipindi karibia chote cha muungano, kuna suala moja ambalo pande zote za mjadala juu ya mfumo sahihi wa muungano pamoja na hatima ya muungano hazina budi kulikubali. Suala hili ni Kwamba, tunakaribia kuadhimisha miaka 50 ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) katika hali iliyotawaliwa zaidi na "Crisis and Instability" kuliko "Progress and Stability". Ni hali hii ambayo ina chimbuko la KIKATIBA, ndio imekuwa ikitishia uhai wa Muungano wetu kwa miaka zaidi ya 40 sasa. Swali linalofuatia hapa ni je, nini ni chimbuko la wananchi wa Tanganyika na wananchi wa Zanzibar kufarakana, je ni:
· Siasa zaidi?
· Uchumi zaidi?
· Jamii zaidii?
· Mchanganyiko wa yote haya matatu?
· Mchanganyiko wa baadhi ya haya?
Majibu kwa swali hili yanaweza kuonekana ni rahisi kuyapata lakini kwa jinsi tunavyozidi kuirudia historia ya Tanganyika na Zanzibar, ndivyo tunavyoweza baini kwamba kupatia majibu yaliyojitosheleza swali hili sio jambo rahisi kama tungevyopenda kufikiri. Lakini jinsi mtu unavyozidi kutafakari, ndivyo unavyoweza kugundua jinsi gani "siasa" zinavyochukua sehemu kubwa kama chanzo cha mfarakano huu. Ushirikiano na uhusiano baina ya wakazi wa Tanganyika na Zanzibar haukuletwa na muungano wa 1964 kwani wakazi wa pande hizi mbili wamekuwa na ushirikiano wa muda mrefu sana, wa vizazi na vizazi. Uhusiano na Ushirikiano huu ulijengwa na bado unajengwa na udugu wa damu, historia, ujirani na muingiliano wa kijamii na kiuchumi, vizazi na vizazi. Kwa maana hii, ni rahisi kubaini kwamba uhusiano na ushirikiano huu wa kiuchumi na kijamii ulionekana ni wa muhimu kwa wakazi wa pande zote hizi mbili vizazi na vizazi kabla hata ya muungano kuzaliwa Aprili 26, 1964. Muhimu zaidi ni kwamba, uhusiano na ushirikiano huu uliweza kumudu mikiki mikiki yote ya tawala za Ureno, Ujerumani, Uingereza na Uarabu, kwa nyakati tofauti. Maswali yanayofuatia ni Je:
· Kwanza, Kwanini Uhusiano na Ushirikiano wa KIUCHUMI na KIJAMII baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar haukuingia dosari yoyote kubwa kwa kipindi kirefu sana Vizazi na Vizazi, lakini uhusiano huo uje kuingia dosari ndani ya kipindi kifupi sana ambacho bado hata hakijakamilisha kizazi kimoja (miaka 50), kutokana na sababu za KISIASA?
· Pili, tunajisikiaje iwapo tunatambua fika kwamba mahusiano yetu ya KIUCHUMI NA KIJAMII yaliweza kudumu kwa muda mrefu licha ya jamii zetu kupitia dhoruba kali zilizotokana na hila za tawala za Ureno, Ujerumani, Uarabu, Uingereza (kwa vipindi tofauti), only kuja kuwa ‘caught up' na SIASA, ambazo zinatishia kuharibika kwa mahusiano haya, tena ndani ya kifupi tu?
Ni muhimu tukautazama muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar kwa mapana na marefu. Tusiuangalie muungano huu kwa sura ya kisiasa bali tuutazame kama ni uhusiano na ushirikiano wa vizazi na vizazi, hasa Kiuchumi na Kijamii kama nilivyojadili awali. Ni muhimu pia tuelewe kwamba, per articles of the Union (1964), hakuna chochote kipya kilicholetwa mezani zaidi ya jitihada za kuhalalisha sasa rasmi na kwa mujibu wa sheria (Mkataba wa Muungano, 1964), mahusiano yaliyokuwepo kwa vizazi na vizazi kabla hata ya Muungano wa 1964. Ni kutokana na ukweli huu, ili sasa kuhalalisha mahusiano ambayo yalikuwepo tayari, Mkataba wa Muungano (1964) ukaja na nguvu ya kisheria kwa kulenga masuala kumi na moja tu ambayo sasa ndiyo yakakubaliwa Rasmi na kwa Mujibu wa Sheria, ndiyo yawe maeneo ya uhusiano na ushirikiano, na mengine yaliyosalia, yaendelee kuwa chini ya mamlaka ya dola mbili husika (Tanganyika na Zanzibar) kama ilivyokuwa kabla ya muungano. Masuala yaliyokubaliwa yawe ya ushirikiano na uhusiano rasmi kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, kabla ya kiini macho kuanza kipindi kifupi kilichofuatia, yalikuwa ni masuala kumi na moja kama ifuatavyo:
1. Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya nchi za nje.
3. Ulinzi.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na Biashara ya nje.
9. Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha, na
11. Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa Anga, Posta na Simu. Na Bunge na serikali vilivyotajwa kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kwa mambo yote juu na kwa ajili ya Tanganyika.
Ukitizama masuala haya kumi na moja kwa umakini, sio vigumu kuelewa kwamba hapakuwa na lolote jipya na la ajabu zaidi tu ya kuufanya uhusiano na ushirikiano baina ya watu wa pande hizi mbili, uhusiano ambao tayari ulikuwepo vizazi na vizazi, sasa kuufanya uwe rasmi na kwa mujibu wa sheria na kwa faida ya pande zote mbili.
Hivi karibuni kumekuwa na nukuu za Mwalimu Nyerere zikitembea, ziinazojadili kwamba "Tanganyika ni sumu Kwa Muungano". Kuna dalili kwamba, kwenye mchakato wa Katiba Mpya, hoja hii ya Mwalimu Nyerere itachukuliwa kama ndio msimamo rasmi wa CCM na Serikali yake na itatumiwa na CCM katika kutetea Sera yake ya mfumo wa Serikali mbili ambayo kiini chake ni Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, na Katiba ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa kufuatia ndoa baina ya TANU na ASP, iliyopelekea Tanzania kuwa nchi inayofuata mfumo wa chama kimoja cha Siasa. Kuanzia 1977, CCM (sio Serikali au Bunge) ikachukua mamlaka yote juu ya masuala ya muungano, pamoja na masula yasiyokuwa ya muungano – yani masuala ndani ya Tanganyika na ndani ya Zanzibar.
Kama tupo sawa hadi kufikia hatua hii, nadhani sasa huu ni wakati muafaka wa kuhoji na kujadiliana kwa hoja maswali makuu yafuatayo:
· Kwanza, Sumu anayoijadili Mwalimu Nyerere ambayo kuna dalili kwamba sasa ndio msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na suala la Tanganyika ndani ya Muungano, Je SUMU hii, asili yake ni kitu gani?
· Pili, kipi ni hatari zaidi Kwa uhai wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Je ni Kitendo cha kuikataa Tanganyika au ni Kitendo cha Kuikubali Tanganyika?
Vijana wenzangu, sasa umefikia wakati ambapo wananchi wa Tanganyika (kama wenzetu wa Zanzibar walivyokwisha elimishwa), wanatuhitaji kuliko wakati mwingine wowote. Tuna wito wa kuwaelimisha watanzania wenzetu wasiokuwa na uelewa mkubwa juu ya kiini cha mgogoro wa muungano wetu pamoja na tiba ya mgogoro huu. Kufanya hivyo kutasaidia wananchi wa Tanganyika (ukipenda waite Tanzania bara) kwanza, wadai haki yao ya kupigia suala husika kura ya maoni (sio kupitia mabaraza ya katiba), na pili, wawe katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa lao (na Muungano wao), sio kwa manufaa ya wanasiasa.
Vijana wenzangu, tutumie mdahalo huu kutimiza wito huu muhimu sana kwa faida ya watoto, wajukuu na vitukuu vyetu huko mbeleni. Huu ni wito na wajibu wetu muhimu hasa sisi tulio bahatika kupata elimu, uelewa na upeo wa masuala kama haya kutokana na jasho la walipa kodi wa Tanganyika. Vijana hatuna budi kutimiza wajibu wetu muhimu wa kulipa fadhila kwa jamii ambayo kwa bahati mbaya, sehemu kubwa yake kubwa haipati fursa ya kuchambua na kuelewa suala hili ambalo ni muhimu sana kwa maisha yao na ya vizazi vyao vya baadae.
Tuepuke kurubuniwa lakini pia kupoteza muda wetu adimu kufarakana na wanafiki wa muungano wanaotumwa na nguvu za kisiasa na uchumi binafsi zaidi kuliko mapenzi na uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
TUMESHATAMBUA KWAMBA BILA YA ZANZIBAR, TANZANIA HAIWEZEKANI. KWAHIYO NI MUHIMU TUKATAMBUA KWAMBA, PIA BILA YA TANGANYIKA, TANZANIA HAIWEZEKANI.
Cc Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, EMT, AshaDii, JokaKuu, Nape Nnauye, Kobello, Kimbunga, FaizaFoxy, THE BIG SHOW, Barubaru, Zakumi SOBY, Mimibaba, Candid Scope, Mag3, Pasco, Bongolader, Ngongo et al.

Last edited by a moderator: