Mdahalo kuhusu mfumo wa elimu Tanzania

Mzee_Wa_Conspiracy

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2014
Posts
667
Reaction score
352
Je unavyo fikiria wewe mfumo wa elimu Tanzania uko vipi ukilinganisha na nchi nyenginezo africa na Duniani kote? Hasa tukiangalia kuwa Tanzania ni moja katika nchi ambazo inawapotezea sana wanafunzi mda katika elimu na vile vile hawako competitive na inovative kama watu wanaotoka nje ya Tanzania.
 
Ww shule ulikuwa unatoka wa kwanza au mwisho unaakili sana.

Elimu ya Tz majanga mtu unasoma 13 hamna kitu
 
Huu ni mjadala mzuri. Tatizo ni kuwa watu wa JF wanapenda kuongea mambo ya ngono tu na siasia. Umaskini wa akili kweli waafrika ni janga. Ingekuwa uliuliza ni "Ni watu wangapi ulifanya nao mapenzi ulipokuwa shule ya msingi?" uzi huu ungekuwa umefika ukurasa wa 10.

Mwenyezi Mungu aturehemu
 
mbona ujachangia mada umetupa lawama ... WATANZANIA KWA LAWAMA .. TOA HOJA ACHA KULALAMA
 
Mfumo wa elimu ya Tanzania ni tunaangalia maksi na hii ni kutokana maana ya neno elimu tumecopy kutoka kwa wenzetuna jamii kuamini kuwa elimu ya darasani ndiyo kila kitu jambo ambalo linafanya wanafunzi kufikiria kuajiriwa badala ya kugundua......

Mimi naamini elimu ya Afrika nzima bado ipo kwenye kufocus kwenye kuajiriwa ofisi fulani na si kugundua kitu... leo hii msomi ukimwambia shika jembe unaweza lima ukafanikiwa atakujibu nimesoma kuja kulima ......

ELIMU YETU INATUFUNDISHA KUWA WAVIVU
 
Mambo ya ngono yameigiaje hapa? toa mtazamo wako juu ya maada, mfumo wa elimu katika nchi yetu unachangamoto zipi kuliko kutoa lawama
 
Mfumo wa elimu ya Tanzania hauwafanyi wanafunzi kuwa wabunifu yaani haina utofauti na elimu ya kikoloni kwa nchi za afrika, yaani inamjenga mwanafunzi awaze kuajiriwa tu na asipopata ajira asiweze kufanya chochote cha kumletea mafanikio ya maisha.

Technical school zimekufa, yaani tanzania mwanafunzi akifeli form four anaonekana hawezi wakati si kweli, unasoma miaka minne then unakuja kufanya mtihani mmoja kwa masaa matatu, ndo maana hata yule aliyekuwa na uelewa mdogo drsan anaweza kufauru kwa kuotea na akaonekana kichwa.

Leo hii tuna graduate wengi ambao wameshindwa kutafsiri elimu yao kulingana na mazingira yanayowazunguka wamebaki wakisubiri ajira bila kuwepo na matumaini yoyote.
 
Kiukweli mm cjardhshwa na ubadilishaji wa mifumo wa matokeo mfano BRN,GPA na ratiba za mitihani ya NECTA.

Wanadhani wanajenga kumbe wanabomoa naona bora Waziri mkuu wa elimu na mafunzo ufundi ateuliwe mtoto wa darasa la saba kuliko hawa wasio na mbele wala nyuma, kwani hawana uchungu na hii nchi kiukweli tumepotezwa.
 
Mfumo wa elimu wa tanzania haulidhishi kwa ujumla.Kuna haja ya kutizama upya aina ya elimu inayotolewa na kama inaendana na manzingira.
 
Elimu ya Tanzania inatolewa bila kuwekeza zaidi rasilimali za nchi katika sekta hiyo na hivyo kupelekea mambo yafuatayo kujitokeza. 1. kukaririsha wanafunzi, udanganyifu katika mitihani na upendeleo katika utoaji wa alama za mitihani za kwa baadhi ya walimu wa vyuo vikuu.
 
Mfumo wa elimu wa tz ni mbovu,, haujaangalia mazingira halisi ya mtanzania na tumefanya kitu knaitwa colonial legacy.. Yaan tunaendeleza mifumo ya kikolon ya kumfanya mwafrika awe job seekers and and not job creator.

Ushauri: Serikali ibadli mfumo na ihakikishe elimu inagusia zaid ujuzi kutokana na mazingira ya ktanzania hasa kuanzia primary to form four,, ili mtu akimalza awe na ujuzi flani utakaomsaidia ktk maisha.

Then kuanzia five na kuendelea chuo hapo sasa asome hata mambo mengne ambayo yatamfanya awe msomi wa kimataifa.
 
[MENTION]miss chaga[/MENTION] Daudi1 Samahani; ni hasira.

Kuhusu mfumo wa elimu wa TZ na Kenya, na nchi nyingi za Afrika, tatizo ni kuwa hakuna filosofia inayowaongoza viongozi wetu tukija kwenye sekta ya elimu.

Hapo awali, Mwalimu Nyerere aliongozwa na filosofia ya education for self-reliance. Na hata kama mfumo huo ulikuwa umekita mizizi katika sera ya ujamaa, kwa kweli uliongozwa na filisofia iliyokuwa imefikiriwa. Ukisoma hicho kitabu chake utapata matattizo yale yale aliyokuwa akijaribu kutatua siku hizo.

Lile jambo ambalo nyinyi mlijaribu na kufaulu nacho, ni kuiweka kiswahili kama medium of Instruction. Tatitozo ni kuwa hamkufatilisha hadi shule za upili na vyuo vikuu.

Jambo lingine ni kuwa mitihani inafanywa kimchezo tuu. Kama vile nilivyowahi sema hapa, kwa mda mrefu nilikuwa na shangaa itakuwaje idadi kubwa ya watu wasome kiingereza kwa miaka zaidi ya kumi ilhali wasiwe bado na uwezo wa kujieleza kwa kiingereza? nilipoona mtihani wa NECTA wa kidato cha nne, nilishangazwa na makosa mengi yanayofanywa na wataaluma

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ecta-ni-sahihi-post11504364.html#post11504364

Hata hivyo, suluhisho ni nini?

Suluhisho ni wewe na mimi tubadili kile tunachoweza. Viongozi wetu hawana mtazamo wala maono. Wanazidi wakileta sera za kipumbavu ilhali watoto wao wanasoma shule za ng'mba na zile za British System. Huku Kenya Professor mzima analeta sera za kipumbavu sana hata nashindwa kweli kama anafikiri.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…