MDAHALO: M4C, Hatima ni Mageuzi au Mapinduzi?

Mkubwa aksante sana kama unalielewa hilo. Mabadiliko ni zaidi ya kuiondoa ccm madarakani inagwaje ndio hatua ya kwanza kuelekea huko lakini Chadema ni lazima wawe na programu makini ili Taifa hili libadilike. MIMI Naamini kama nilivyoandika kwenye andiko langu mabadiliko ya kweli ni ya ki fikra. Katika chadema sijaona fikra mbadala na hii inanipelekea kuamini lengo lao ni kushika Dola tu na kupata ufahari wa madaraka na mali na sio mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mimi niko mwanza hapa hadithi ya matatizo ya chadema mwanza naijua.
 
Shayu,
Mkuu wangu nimekusoma sana lakini kusema kweli sijakuelewa kabisa. Na nitasema kwa nini hasa? Kwanza kabisa umesema mwenyewe unataka kuelewa 'Movement for Change" ina maanisha nini? halafu maajabu umekuja na tafisri yako kwa jinsi unavyofikiria wewe. Ungesubiri basi hata ujibiwe kabla hujawapa jina jingine la - Movement for Power..

2. Haya nikikusoma chini umezungumzia mengi sana yanayohusu UTAWALA BORA na kusisitiza kumpata kiongozi bora atakaye weza kuleta umoja wa Taifa na kuonyesha dira na mwongozo lakini pia umezungumzia uwezekano wa chama kinaweza kuwa Reformed kwa kubadili mitazamo yake na mwelekeo wake kinapoona kinakosea, wanapobadilika wanaweza kubadili dira na mwelekeo wa nchi. Hapa nashindwa kabisa kuelewa kabisa unaelekea wapi...Chama kikibadilisha DIRA sasa huyo kiongozi bora ataweza vipi kuwa mbora ikiwa dira alowaonyesha wananchi inaweza kubadilika njiani..

3. Umezungumzia swala la wananchi wabadilike, Na sidhani kama kuna njia bora zaidi ya kwanza kulaani vitendo viovu, Huwezi kupambana na Ufisadi nje ya Utawala kwa kujenga sera isipokuwa kulaani vitendo vinavyohujumu uchumi wa nchi. Kupambana na Ufisadi ni hoja ambayo inatanguliwa na kuharamishwa, na kama hutaweza kuwajenga wananchi imani ya kuogopa na kulaani Ufisadi basi kazi nyingine zote hazitakuwa na maana yoyote. Umesema mwenyewe ya kwamba - Maendeleo ya kweli kwa jamii yeyote ile ni transformation ya roho, akili, mwili na mali, bila ya vitu vyote hivyo kukamilika binadamu hajakamilika kimaendeleo. Hivyo sioni kosa lolote la M4C inapohamasisha watu na kuwaeleza mabaya ya ufisadi kuwa sehemu ya mchango mkubwa wa umaskini wao

4. Nakushangaa tena wewe mwenyewe unapopingana na dhana ya wale walookoka kuwa sehemu ya mkusanyiko huo huo ukiwaita ni watu wa kuokota okota. Ikiwa mtu kakubali na kutiwa maji unataka nini zaidi ya mtu huyo kuhudhuria ibada za chama, kujumuika na wengine na kueleza kaweza vipi yeye kutambua ubaya wa Ufisadi na ama kufanya kazi chini ya uongozi shalimu. Kwa nini mtu huyu aendelee kuonekana hafai wakati wajibu wetu wa kwanza ni kuwabadilisha wananchi hao hao wapate kuyaona mabaya na hivyo nao wawe maswahaba wa kutangaza yalokuwa mema maana hawa wametoka ktk Mabaya..

Pengine unashindwa kuelewa kwamba mtu yeyote msafi ambaye hajawahi kupatwa na majaribio kama haya, huwa hajui upande wa pili isipokuwa huijua tu laana ya vitabuni. Lakini yule alokwisha kuwa Fisadi na akaungama anaweza kuwa mbora zaidi yako kwa sababu kisha onja joto la jiwe na anaijua tanmu na chungu ya Ufisadi. kajua jindsi gani anavyowakwaza watu wengine na hivyo he became a freeman..Ktk imani za Dini sisi wote tulikuwa wenye madhambi na tumeingia dini kujinasua ktk dhambi hizo na leo ndio tunafundishana neno la Mungu..

Umeendelea kuikejeri M4C kama ni propaganda tu. Hii ina maana wewe binafsi huja Imani na Uongozi wa Chadema wala kazi wanayoifanya. Sema ukweli tukusikie vizuri maana hakuna sababu ya kuficha uso kiamini. Hivyo ingekuwa vizuri zaidi kama ungetuambia wewe kwa nini huna Imani na viongozi wa Chadema, huna imani na M4C hadi ukafikia kusema watafanya yale yale ya CCM. Ni dalili zipi zinazokuonyesha wewe kuwepo uwezekano huo..

Labda nimalizie tu kwa kusema M4C ni sehemu ya harakati za kukijenga chama mikoani, na Chadema wamejieleza sana tena sii mahala pamoja. Wewe kama unafiiria ama unategemea kuwa hizi ni propaganda za kuwaweka IKULU hilo umelifikiria wewe lakini wenzako wanachokifanya ni kukipeleka chama kwa wananchi huko vijijini. Mwalimu Nyerere alifanya hivyo hata kabla ya kuomba Uhuru na haikuwa hoja ya Nyerere atawafanyia nini watanzania bali kuwanasua toka ktk Ubeberu wa mwakoloni...

Pengine ungeweza sana kuchangia hoja pale unapoona Chadema wanachelewa kujieleza wakiingia IKULU watafanya nini lakini pia umesahau ya kwamba wakifanya hivyo itaonekana wameanza kampeni za Uchaguzi mapema na kinyume cha sheria. Kama kweli unataka kujua Chadema kama chama kitaleta mabadiliko gani kwa wananchi basi soma SERA zao ktk tovuti yao na kama kuna jambo ambalo hukubaliani nalo liweke hapa tulijadili. Binafsi yangu miye kama Mtanzania, I can't wait kuona CCM wanaondoka madarakani kwanza halafu nitawapima Chadema kulingana na sera zao pamoja na ahadi watakazo zitoa. Leo hii ni mapema sana kutangaza watafanya nini wakiingia IKULU hiyo itakuwa kuvunja sheria na kanuni za uchaguzi mkuu...
 
kitu kikubwa kinachotusumbua ni POVERTY & IGNORANCE. hakuna kitu kibaya katika dunia ya sasa kama Ignorance... this bring poverty. Wakati wa kuuhalalisha muungano waliwauliza wananchi wakasema ndiyo, kuhalalisha mapinduzi tuliulizwa tukasema ndiyo, vyama vingi tulisema ndiyo, sasa katiba mpya tumesema ndiyo. Ila kiuhalisia hamna jambo hata moja lilobadilisha maisha yetu. Isitoshe mengi yaliyoamuliwa tumeona yana mapungufu makubwa. Hii ni kwasababu moja kubwa WATANZANIA WENGI HATUJUI KINACHOENDELEA. MABADILIKO TUNAYOTAKA NI YA KIELIMU KAMA FIRST PRIORTY.
 
Wewe ni mmojawapo wa hao wengi wanaoamini hivyo?? M4C ni nadharia au tayari ni wazo litendalo kazi??
M4C ni mwanzo mzuri wa kuelekea katika mabadiliko ya kweli, iwe ni mapinduzi au mageuzi yanayokaribiana na mapinduzi, huo ni uamuzi wa walio wengi - UMMA, na ni wajibu wa chama cha CCM na serikali yake kushughulikia chanzo (root-cause) cha vuguvugu hili kuliko kushughulikia matokeo;CCM ikikaa chini na kuamua kutumia akili timamu, itagundua chanzo ni CCM yenyewe;
 


Ngoja nikwambie ndugu yangu, Binadamu ni jinsi anavyofikiri . Ni mawazo yake. Ninaposema chama kikibadili mitazamo yake kitabadili dira yake nilikuwa namaanisha chama kitakapobadili philosophia yao ya kutawala, kinaweza kubadili mwelekeo wake. Ni ukweli kwamba ubora wa kiongozi yeyote hutokana na ubora wa vile anavyofikiri. Ni wazi ya kwamba kiongozi yeyote yule bora huzalisha fikra bora na zenye manufaa. Na kiongozi mbovu ni kinyume chake.

Kitu ninachosema tena, kitu tunachohitaji katika Taifa letu ni Ku reprogramming peoples mind. Kwa kuingiza fikra mpya miongoni mwa mamilioni ya watu wa Taifa hili kuhusu Utaifa na kujenga umoja na malengo ya pamoja. Akili zetu zimefocus katika ubinafsi na sio utaifa hatutaweza kupiga hatua pasipo kubadili hiyo mentality. Mobilization ya watu ni kitu muhimu sana ili watu wawe malengo. Ili Taifa liwe na malengo. Nimeongea mengi sana kama ukinisoma kwa umakini utagundua umuhimu wa mambo mengi niliyoongelea. Nilazima tusukumwe na utaifa zaidi kuliko ubinafsi ili tujenge hilo na hili sijaliona katika CDM. Wamefocus zaidi katika kushika dola pasipo program makini ambazo wakiingia madarakani kwanza watabadilisha fikra za watu lakini pili wataleta maendeleo. Lakini pili sidhani kama viongozi wote waliohamia Chadema walifuata Sera au itikadi za chadema bali uongozi na kujinufaisha. Hapa ndipo tulipofikia kama Taifa.
 
Kiongozi makini ni nahodha ktk meli yetu hivyo tunachokihitaji ni ujuzi wake kutufikisha tunakotaka. SERA za chama ndio mwongozo wetu wote na ndizo tutakazo chagua njia hiyo kwenda ktk safari yetu. Chama hakiwezi kubadili dira isipokuwa wanaweza kubalidilisha priority zao kutokana na mazingira yaliyopo safarini.

Kuhusu UMOJA wetu sidhani kama kuna chama hata kimoja kinachoweza ama kudiriki kuzungumzia hilo kwa sababu tayari wananchi tumeisha gawanyika. Hata UDINI uliopo umetokana na UBINAFSI hivyo ili kuondosha UBINAFSI ni lazima kwanza kuondosha Udini jambo ambalo hakuna chama kitathubutu kufanya hivyo. Kuna ukweli mkubwa sana kuhusu M4C kuchelewa. Hii kitu ilitakiwa kuanza 2010 baada tu ya Uchaguzi lakini tukumbuke pia kwamba CCM walianza kupiga madongo kuwa uchaguzi umekwisha hizi habari za kukikosoa chama ni kuleta vurugu nchini - wananchi wameisha chagua!.

Muda huu Chadema walitakiwa kuwa ktk uchaguzi mkuu ndani ya chama tayari kwa maandalizi ya kampeni na hii inatokana na kwamba viongozi wetu wameshika majukumu mengi na mazito kiasi kwamba hawana hata muda wa kupanga maandalizi ya mikutano ya chama. Makosa makubwa yaliyofanyika ni kuwaweka Wabunge kuwa pia viongozi wa chama na kuunda sekretariet, wamejibebesha mzigo mkubwa kuwa na kofia zaidi ya mbili lakini pia sidhani kama viongozi hao wako tayari kuachia nafasi za Ubunge au za uongozi wa chama kutokana na kutokuwa na IMANI na watu wengine, hivyo kukifanya chama kionekane kina wenyewe!
 
Mtoa mada amekwazika padogo sana pamoja na maelezo marefu, anaifahamu njia ya kuleta maendeleo lakini hajaitambua. Ukisoma maelezo yako mwanzo mpaka mwisho unakiri kwamba kuna tatizo na uongozi uliopo, kuna tatizo la mfumo na kwamba kunahitajika mabadiliko. Lakini hujui ni kwa namna gani yatokee hayo mabadiliko. Mabadiliko chanya huanzia kwenye fikra, hayo yakiwa katika jamii ni lazima yataleta msuguano (sababu fikra za watu tofauti hazifanani). Iwapo kundi kubwa katika jamii litakombolewa kifikra na kuwa na muono unaokaribiana, hapo ndipo mabadiliko ya kweli yatatokea. Katika mabadiliko hutokea pia mabadiliko ya uongozi, na jamii yoyote ni lazima iwe na uongozi wake, hivyo wanajamii kutaka kuwa sehemu ya viongozi si uchu wa madaraka kama unavyoamini bali ni haki na wajibu wa kikatiba/ sheria na taratibu. Ndio maana haki hiyo iko wazi. Uchu wa madaraka ni neno la kifedhuli lililoasisiwa na walafi wa madaraka ambao kwao uongozi ni ufalme badala ya utumishi. Na sitoshangaa ukawa mmoja wa hao ambao wanaamini kwamba walizaliwa kutawala. C4M imelenga katika kufufua fikra huru, na kuwaamsha wananchi katika utumwa wa kuomba hisani kwa serikali waliyoiweka madarakani, badala ya kuituma kazi na kuiwajibisha inaposhindwa kutekeleza jukumu lake la msingi la kusimamia ustawi wa watu wake. Hii kazi ni ya kizalendo zaidi ya kudhani ni uchu wa madaraka, kwani wananchi wakipata uelewa wa kujua nguvu yao dhidi ya serikali, ndio utakuwa mwisho wa kukandamizwa na watawala dhalimu, wanaotumia ujinga wa watu kama nguzo ya kuficha uovu wao. Kutokana na M4C matunda yameanza kuonekana, watawala wanahaha kutumia kila mbinu ujumbe usizidi kuenea. M4C inaanza na wewe, just change, otherwise change will change you.
 
 
Onyesha njia mbadala na sio kuendekeza chuki zako binafsi dhidi ya CHADEMA.
 
 
umeandika theory ndefu za darasani! Nchi yenye wananchi desperate kama TZ inahitaji mabadiliko ya aina zote na yoyote!! Jiunge na M4C utoe mchango wako wa mabadiliko. Hizo "mindset change" unazorejea ni mchakato wa mabadiliko. Lakini kwanza tunahitaji mabadiliko yatakayotoa nafasi yote ya mawazo mazuri kama yako!! Kumbuka nadharia hugeuka vitendo kwa commitment tu!!
 
Mtatoa mawazo mazuri yanayotakiwa kuzingatiwa lakini sitegemei mpumbavu/punguani/taahira yoyote kujitahidi kutetea mfumo na uongozi uliopo!! eti CCM No never!!
 
Ukiona mtu anashindwa kuona mapungufu ya utawala uliopo na kuanza kutoa matokeo ya utawala unaotarajiwa wewe fahamu ni wale wale, unawezaje kusema CHADEMA hawana hiki wala kile so what? waliopo madarakani ndio waendeleze ushenzi wao kwa sababu wanaotaka kuja nao wanaonekana wana mapungufu?Tuwahukumu CHADEMA kwa maoni yetu hata kabla hawajaingia uwanjani,wakati waliopo uwanjani wameshajifunga goli 20. Chadema watapewa nafasi na kama nao watashindwa tutaangalia pengine,hii nchi si ya CCM, wala si ya CHADEMA ni ya watanzania! tuache kuleta mawazo ya kifisadi hapa tukijifanya tunaikosoa CHADEMA kwa lengo la kuihalalisha CCM.
 
 

Ndio maana huwa nahimiza kwamba, ili Chadema wafanikiwa 2015, lazima waje na A HOLISTIC APPROCH - kisera na kiitikadi na kuishindanisha na ile ya CCM; Suala la ufisadi, pamoja na umuhimu wake wote, sio guarantee ya kuipa Chadema nguvu ya kushinda 2015, hasa ikizingatiwa kwamba as of today, bado vyama vyote viwili - Chadema na CCM, vinaweza kushinda kwa kura nyingi sana kwa kutumia tiketi ya kupingana na ufisadi; Ndio maaana ni muhimu kwa Chadema kuja na holistic approach itakayoonyesha kwamba - chini ya ccm tumetoka wapi, tupo wapi, na tunaelekea wapi, huku Chadema pia ikija na mkakati wake wa muda mfupi, wa kati, na mrefu - kuanzia hapo, sasa tutakuwa na ushindani mzuri sana wa kisiasa wenye tija kwa wananchi; Bila ya hivyo, CCM itarudi madarakani 2020, kama sio kabla ya 2020...
 
I am inspired by the commitment of the M4C campaigners. Bravo, guys! You have our all salutes towards 2015.
 
I am inspired by the commitment of the M4C campaigners. Bravo, guys! You have our all salutes towards 2015.

Chui hawezi kuwakomboa swala ni jukumu la Swala wenyewe kujikomboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…