jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Fighting injustice is fighting poverty.is this the same as saying Poverty is Injustice therefore fighting Poverty is Fighting Injustice?
Kwanza tuanze na definition hii ya injustice...
Rushwa ni injustice,ufisadi ni injustice.(vinasababisha umasikini)in·jus·tice
   /ɪnˈdʒʌstɪs/ Show Spelled[in-juhs-tis] Show IPA
noun 1. the quality or fact of being unjust; inequity.
2. violation of the rights of others; unjust or unfair action or treatment.
3. an unjust or unfair act; wrong.
Utawala unaotumia nguvu ni injustice,polisi kuuwa wananchi wasio na hatia ni injustice(vina violate haki za kimsingi za wananchi)
Chochote kinachofanywa na watawala wetu ambacho kina negative impact kwenye maisha ya wananchi wake ni injustice.
So yes poverty is injustice,and therefore fighting injustice is fighting poverty amongst others.
m4c is for educating the mass on their rights,and the state of their economic and political affairs,that equals to fighting injustice.
Kuhusu wether lengo la m4c ni reforms au revolution,nadhani swali lako hilo ni la kimtego zaidi.Kwasababu umezungumzia economic ferorms peke yake na ndiyo maana ukazungumzia issue za world bank etc.Je unataka kusema hata hizo reforms ambazo zimefanyiwa kazi na ccm zilifanikiwa?Jibu ni hapana!Sababu zake,bado ni injustices inayotokana na poor implementations.Ni kweli sera nyingi za world bank na imf siyo very helpfull kwa mataifa masikini,lakini bado tungeweza kufanya vyema kuliko sasa.
Same thing kuhusiana na rasilimali zetu,yes makampuni makubwa yanatubana kuhusiana na wanacholipa,lakini corruptions na 10 percent ndiyo injustices kwa wananchi.Hayo yangekuwa fixed kwanza,ndiyo tuangalie whats next kuhusiana na kuifanya mikataba itunufaishe.Hatuwezi kuzungumzia kuhusu mikataba kutunufaisha na wakati kuna viongozi wanaopendwa na hayo makampuni kwasababu in reality wanawakilisha matumbo yao badala ya maslahi ya taifa.
Wala hakuna haja ya kujiumiza kichwa kuuliza kama ni revolution ama reforms,kwasababu hayo ni matokeo ya maamuzi ya wananchi na wala si chama cha siasa.Chama cha siasa kinaweza kujikita kutoa elimu hiyo(m4c),lakini ni juu ya wananchi kufanya maamuzi.Na ndiyo maana tunatabiri kuwa maamuzi hayo watayafanya 2015.
Ila ikitokea kuwa watawala wanawanyima wananchi wake haki zao za kimsingi(unyanyasaji na mauwaji kwenye m4c),basi ujuwe kuwa watawala ndiyo wanaweza kusababisha mapinduzi kutokana na injustice.Hayo mambo hayapangwi,bali hutokea kwenye proccess ya wananchi kudai haki na wao kubinywa,hapo ndipo wana revolt kutokana na udhalimu wa watawala.
Nafahamu kwamba umetoa definitions kadhaa za mapinduzi ie umezungumzia mapinduzi ya kiuchumi,hayo hayahusiana na injustice,kwa mfano industrial revolution,hayo ni mapinduzi ya viwanda,kilichofanyika si sawa na tunachozungumzia hapa na wala hakina relation yoyote na yatakayoweza kutokea kutokana na m4c.Hilo haliwezekani kwasababu chadema siyo chama cha kisoshalisti wala kikomunisti.Hivyo hakutaweza kuwa na rapid change of the economic system(characteristic ya economic revolution).
However tunaweza kuwa na economic revolution kama tukiwekeza pesa nyingi kwenye ukuwaji wa viwanda badala ya mafisadi kuziweka uswisi na kwingineko.
Pia hata ubepari wenyewe,umepitia reforms na bado unaendelea kupitia reforms.Na ndiyo maana hata mimi nimekuwa nikisema kuwa tunayapokea ya ubepari bila kujitathimini,haina maana kwamba tukiyafanyia teforms basi ni kwamba hatuupendi ubepari,la hasha!La msingi kuelewa hapa,ni kwamba hata ubepari bado unahitaji reforms na ndicho kinachoendelea hata kwenye mataifa ya wenzetu.Kila mara kuna reforms zinazofanyika ili kuweza kuwanufaisha wananchi na ku eliminate injustices as much as possible.
Njia ya kujaribu kubadili ubepari, au 'mageuzi', ni mojawapo ya njia ambazo zimewahi kuchukuliwa na wenzetu ambapo walitaka kuboresha jamii. Baadhi ya mageuzi yamesaidia kuboresha maisha yao kwa ujumla na mazingira yao ya kazi.
Kiukweli,hakuna ubaya kuona kampeni(m4c) kwa ajili ya mageuzi ya kuleta maboresho muhimu na kuongeza ubora wa maisha ya wananchi.Kuna mifano ya hili katika nyanja kama vile elimu, makazi(mipango mji nk),na usalama wa kijamii.Tumeona kuna matatizo kwenye idara ya afya(migomo ya madaktari,wagonjwa kulala chini,ukosefu wa vifaa na madwa etc etc),tumeona pia kuhusiana na elimu(malipo ya walimu,na hali halisi ya shule zetu pamoja na vifaa,madarasa nk).
Mageuzi hayo ambayo hata wenzetu waliyafanya chini ya mfumo wa kibepari,yamesaidia sana.Ni kweli hayajamaliza matatizo yote,lakini yamesaidia.Kujaribu kutaka kuyamaliza matatizo yote ya ubepari,ni kujaribu mfumo mwingine tofauti na ubepari(REVOLUTION),jambo ambalo sidhani kama linaendana na sera na itikadi za chadema,ambao wameshasema kuwa wao ni a "right wing party"
Ni kweli kwamba kumekuwepo na reforms ama shinikizo la reforms kutoka kwa world bank na IMF kuhusiana na mikopo wanayotupa,mingine ina masharti ya kupeleka pesa hizo kwenye nyanja ambazo binafsi huwa naona kama sizo ambazo tungezichaguwa sisi endapo tungepewa uhuru huo.Kwa maana ya kwamba there are strings attached that tends to be unbeneficial to us,however bado unaweza kuona kwamba hata hiyo mikopo bado tunai missuse.Hili linahitaji reforms in terms of how we manage the funds and how we implement the projects.Hilo linahitaji serikali mbadala.
WB na IMF kiukweli,zilianzishwa ili kukabiliana na usoshalisti pamoja na ukomunisti,(my take)haswa baada ya serikali zenye mirengo hiyo kutengwa,na baada ya chumi zake kuyumba,ndipo zikaja hizo institutions.
Kama unakumbuka,hayo ni baadhi ya mambo ambayo mwalimu Nyerere alikubaliana nayo kwa shingo upande,na masharti yao yalikuwa ni reforms ambazo hata yeye mwalimu aliona ni kinyume kabisa na maono yake kwa taifa hili.(ujamaa na kujitegemea)
Pamoja na hayo,bado serikali zetu zimekuwa kama zinacheza upatu kwa kuyaweka maisha ya wananchi wake rehani.
Niishie hapo kwasasa...Na kama ikiwezekana,ama kama umenielewa,basi tuyazungumzie hayo ya reforms tulizozifanya(chini ya ccm), ili kuweza kuendana na mapendekezo ya WB na IMF.Hilo litatusaidia kuona kuwa ni wapi tumeshindwa na kama sababu hizo za kushindwa huko ni za kwetu sisi ama kama ni za hizo instituiton.Au pengine labda ni a combination of both factors.
The bottomline ni kwamba m4c haina nia mbaya na taifa letu,unless kama unaamini kwamba tuko on the right track.
Undo edits