Miwatamu,
Asante sana kwa mchango wako mzuri; Ningependa kujibu hoja zako kama ifuatavyo:
Mosi – Mdahalo Wangu na Hofu Kwa Wafuasi wa M4C
Wakati najiandaa na mdahalo huu, niligundua kwamba upo uwezekano wa HOJA yangu kutoeleweka vizuri, kupotoshwa au kuwekwa completely out of context; Kutokana na hili, ndio maana awali kabisa katika my original thread, nikaomba radhi kwamba ingawa ni mdahalo, nitatumia muda kidogo kuweka mambo fulani fulani sawa ili kuepusha matatizo haya; Nashukuru kwamba juhudi hizo zimezaa matunda kwa kiasi kikubwa sana kwani wadau wengi wamekuwa wanaenda moja kwa moja kwenye hoja huku wakitoa maoni kwamba - nilichokiweka kinatosha kwa kuanzia;
Hadi sasa, ni wadau wawili tu (mwingine ni Joka Kuu), ndio wamekuja na hoja kama yako, hasa accusations kwamba mdahalo wangu unalenga kujeruhi Chadema na Demokrasia kwa ujumla; Nimejaribu kulifafanua hili kwa ufasaha, na ukipata muda naomba usome Post Number 45, ambayo ni majibu yangu kwa Joka Kuu kuhusu suala la mdahalo huu kuwa na nia ya kujeruhi harakati za Chadema, na Demokrasia kwa ujumla; ukipata muda, majibu yangu kwa hoja yako huu utayakuta huko;
Pili – Uhafifu wa Marejeo/Reference Kitaaluma
Kama ilivyo mimi, wewe, au yule, we are both not perfect; Tuna mapungufu yetu kiuwezo wa akili, uelewa, uchambuzi, ujengaji hoja, lakini muhimu zaidi, tuna tofauti za kimtazamo; Ndio maana mdau kama Nguruvi3 ana uzi wake mzuri sana wenye kichwa "Mgongano wa Mawazo", kwani katika mijadala, given our differences, lazima mgongano wa mawazo uwepo; Kwahiyo, niseme tu kwamba uwezo wangu wa kurahisisha mdahalo huu uliishia hapo unapopaona pana mapungufu, suala ambalo ni la kawaida kabisa na nalitarajia in terms of constructive criticisms.
All that said and done, ingawa nilichofanya haikuwa presentation ya utafiti, tafiti zote zimejaa GAPS, ndio maana hata mtafiti atunukiwe Nobel Awards mia moja katika fani ile ile, bado kutakuwa na mgongano wa mawazo. Hii ni kwa sababu lengo la UTAFITI sio KUTOA MAJIBU, bali -
to shed more light into the body of knowledge that exists; na kilicho muhimu zaidi katika mchakato huu ni METHODOLOGY AU MBINU zinazotumika katika kuongezea mwanga kwenye ufahamu uliopo; Hata kwenye PhD levels za fani zote, wanachoangalia zaidi Examiners na kukipa Marks, sio utafiti ambao uta change the world, bali the Methodology used katika juhudi za ku-shed more light to the existing body of knowledge;
All that said, kama uliangalia kwa makini hoja yangu ya msingi, nilijitahidi kuheshimu kanuni zote hizi ambapo nilielezea kwamba MABADILIKO huja kwa sura kuu mbili: MAGEUZI au MAPINDUZI, na nikajaribu kufafanua, japo kwa ufupi maana ya dhana hizi mbili; Vile vile, iwapo ulinisoma vizuri, nilielezea jinsi gani Tanzania imekuwa inapitia mageuzi hasa baada ya kuondokana na Sera ya Ujamaa mwaka 1985; katika hili, nilielezea kwa kirefu sana suala zima la the
NEW PUBLIC MANAGEMENT under the auspices of the World Bank and the IMF, ambapo literary masuala ya Privatization, Marketization na Liberalization yanatokea huku na kuja kwetu kwa sura ya MAGEUZI ya aina mbalimbali; Kwa mtu yoyote muelewa au mwenye shauku ya kujua Reforms in Sub Saharan Africa zinafuata mkondo gani, ndani ya sekunde chache atakutana na suala la New Public Management ambalo mimi niliingia zaidi kuangalia kwa undani zaidi reforms katika sekta ya Uchumi, Utumishi wa umma, Usimamizi wa Fedha za Umma, n.k. Na katika suala la MAPINDUZI, nilizungumzia mapinduzi ambayo ni incremental vis-à-vis Mapinduzi ambayo ni radical; All in all, niligusia maeneo yote muhimu ambayo ni lenin-marxist in nature, japo kwa juu juu;
Suala lingine muhimu pia niliweka wazi kwamba nia yangu pia ni kuanza kujenga hadidu rejea, nikitarajia ushirikiano wa wadau wengine katika kufanikisha hili; ndio maana iwapo utakuwa unaendelea kupitia majadiliano ya humu ndani, utagundua kwamba kuna exchanges kadhaa baina yangu na Kobello, Jmushi1, na wengineo ambapo tumekuwa tukielimishana juu ya matumizi na maana ya dhana mbalimbali, hasa Mapinduzi, Poverty, Injustice, Class structures in society n.k. Na katika exchanges hizo, nimekuwa nakiri kujifunza mengi, na nina imani kwamba nitaendelea kujifunza mengi zaidi;
Baada ya kujibu masuala haya, sasa niingine moja kwa moja kwenye hoja zako zinazolenga kujibu maswali makuu matano niliyoyauliza kama a guide for our debate.
Swali la Kwanza, je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI? Jibu lako:
Kwanza kabisa naomba nikujulishe kuwa asilimia kubwa ya wale wanataka na kushabikia M4C ni vijana moto na wenye upeo mkubwa katika uwanja wa siasa na si ajabu umekaa nao darasa moja au ni walimu wako….. (Tzm: Maprofesa na wengineo)
Nakubaliana na wewe katika hili, lakini roho inasikitika kidogo iwapo mvuto wa M4C kwa hao watajwa ni Ushabiki badala ya believers, followers au kitu kingine more concrete;
Swali la Pili: Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI? Jibu lako:
Kiu wanayo! Ndiyo maana nilieleza hapo juu kuwa yawezekana unachokiandika, aidha unakijua kwa kuwa unakiona uhalisia wake au unajaribu kupima… Lakini kubwa katika hali ya sasa nchi zote zenye maendeleo ni zile zenye utawala wa zaidi ya chama kimoja; anza na Marekani, Uingereza, Ujerumani,Uholanzi Japani Russia na kweingineko….!
Sioni mantiki yako ya kusema kwamba napima upepo wakati katika my original post nilisema haya:
"Suala la UMMA WA TANZANIA Kuwa na kiu ya mabadiliko halina mjadala tena, badala yake, mjadala sasa ni juu ya AINA ya Mabadiliko ambayo Umma unayahitaji, kuelekea 2015".
Vile vile katika majibu yako kwa swali langu la pili unasema haya:
….walichonacho wale wanaotaka mabadiliko ya utawala na wala si MAPINDUZI kama wewe unavyotaka kuwaaminisha. Kwa ujumla wake watu wanahitaji kupata mikakati mbadala na sura tofauti hasa ikiwa na ile tabia ya kuendesha nchi kama kampuni ya kifamilia.
Hapa unayumba kihoja kwani kwanza – unani accuse kwamba nataka kuaminisha UMMA kwamba mabadiliko ya kweli ni Mapinduzi wakati kwa walionisoma vizuri wanaelewa kwamba my presentation ni kwamba kuna aina mbili za mabadiliko – Mageuzi na Mapinduzi, huku nikijenga hoja kwamba ni muhimu kwa umma kujua tofauti hizi, hasa kuhusu nini M4C inadhamiria kufanikisha;
Kuyumba kwako kihoja kunazidi kushika kasi pale unapojichanganya kwa maneno kwamba – wananchi wanataka kupata mikakati mbadala na sura tofauti, bila ya kujua kwamba hizi ni elemements za mapinduzi kwani Mageuzi hayahusiani na mkakati mbadala bali marekebisho ya mikakati au sera zilizopo; bila ya kujijua, hii kauli yako ipo more revolutionary…, na inazidi kusindikizwa na elements za Mapinduzi pale unapoonyesha una machungu na utawala wa kifamilia, wakati sote tunajua hatima ya machungu kwa tawala za namna hii huwa ni nini;
Swali la tatu niliuliza hivi: TATU, Je: Viongozi wanaoendesha "Mass Movements" wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi "Mass Movements" wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi? Jibu lako ni:
Ili kuonesha kuwa CCM sasa hivi inafanya kazi kama chama cha upinzani; kwanza ni hali yake ya kufanya kazi zake kwa kutekeleza matakwa ya Chadema, mpaka hapo utaona kuwa tayari chadema ipo madarakani hivyo kilichobaki ni kuthibitishwa kwa wananchi tu. Jambo la pili ni lile la IMF na WB kuiburuza nchi kana kwamba haina watawala wenye fikra ya kusema hiki ni sawa au la! Kama hivyo mbona kuna mambo ambayo nyerere alikuwa akiwakatalia?!! Utaifa kwanza.
Kwenye hili tupo pamoja; lakini ni muhimu sana kwa Chadema ikaze kamba zaidi kusahihisha masuala mengine yaliyobakia ya msingi ambayo bila ya kuyafanyia kazi, haitaingia Ikulu 2015; mfano, kanuni ya mshindi ni mshindi – mimi nazidi kuamini kwamba iwapo kanuni hii itabakia kama ilivyo, mgombea wowote wa CCM atapita 2015 dhidi ya Chadema, kwani hata matokeo ya Urais 2015 kwa CCM by 50.01% na Chadema 49.99%, Mshindi ni CCM; Vinginevyo ukipata muda, soma hoja zangu nyingine kuhusu utayari wa chadema kutawala 2015 kwa kugonga hapa
https://www.jamiiforums.com/great-t...tujadili-utayari-wa-kutawala-nchi-2015-a.html
Swali la nne niliuliza:Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA? Jibu lako:
CCM imekuwepo madarakani kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitano sasa! Kama imeshindwa kwenda mbele kwa kipindi chote hicho na badala yake inarudi nyuma kwa kasi ya ajabu! Je, leo itaweza kufanya Reforms ndani ya miaka hii miwili iliyosalia? CCM imebaki ikifanana na baba mlevi ambaye pindi arudipo nyumbani watoto hukimbilia kukaa jikoni na mama yao badala ya kumshangilia na kumkumbatia. Hivyo hata mtoto akikuta amelala sebuleni hatamuamsha. Jipange upya kwani watu wanajua wanachokitaka.
ANGALIZO: kinachoonekana kwa sasa CCM ndiyo inayojiandaa kufanya Mass Revolutions pindi wakishindwa kutokana na jinsi kinavyotumia nguvu nyingi katika kudhibiti wanamageuzi.
Nakubaliana na hoja zako ingawa point yako ya mwisho imetoka kijazba; Nijipange kama nani? Mwanachama wa CCM? Kiongozi wa CCM? Kibaraka wa CCM? Mpambe wa Mgombea Fulani?