EMT,
Asante kwa somo lako zuri; Nimepata masuala matatu muhimu sana katika hoja zako nayo ni: Kwanza ni suala la Volcano – kwamba ikiwa tayari to erupt, ina erupt tu, eruption sio kitu cha kuairishwa; Pili, hoja kwamba ‘no matter how good things are or get, it is in human nature to ask or dream for more'; na Tatu, ni kuhusu the Frog in the boiling pot;
Nikianza na suala la Volcano…, sidhani kama nitakuwa nimekosea nikisema kwamba kwa ujumla wake, tatizo linalowakabili watanzania, au pengine changamoto kubwa ni UJINGA WAO; Na ndio maana Ujinga ni moja ya mambo makubwa ambayo Nyerere declared ni maadui katika Maendeleo, na suala hili alilivalia njuga wakati wote kulitokomeza; Ni hadi pale UJINGA miongoni mwa watanzania utakapopungua ndio UMMA utaweza KUAMKA; na naungana na hoja yako kwamba UMMA lazima uwe tayari kusaidiwa kujitambua – lakini Main Agent of Change in this Agent in my belief, ni KUPUNGUA KWA UJINGA, ambao kwa sasa umetapakaa katika kila kona ya nchi yetu; Iwapo hadi hapa unakubaliana na mimi, Kama tunakubaliana hadi hapa, swali linalofuatia ni je, ni Jukumu la Nani kupunguza Huu Ujinga miongoni mwa UMMA, na je una faida Kisiasa kwa CCM au ni Liability? Sitegemei majibu kutoka kwako juu ya hili, ni suala tu la kutafakari;
Kuhusu hoja yako kwamba it is in human nature to ask for more and more no matter how much better it gets…; Kimsingi nakubaliana na wewe katika hili, kwani hata kwenye nchi za wenzetu zilizoendelea kiuchumu, huwa tunaona machafuko ya hapa na pale ya UMMA ukidai
MORE Political, Economic and Social Justice; Lakini pamoja na ukweli huu, binafsi nadhani bado kuna Certain Threshold ambayo lazima kama Taifa, tuiweke sawa kabla hatujasema kwa kujiamini kwamba tumefanikisha hili au lile..; Kwa mfano, inasikitisha kuona nchi ndogo kama Rwanda ikiendelea kufanikiwa na sera yake kuondokana na nyuma za udongo na nyumba za nyasi sambamba na target waliyojiwekea; Sisi tunashindwa nini kufanikisha mambo ya msingi kama haya? Yapo masuala mengi in terms of basic needs ambayo tukiamua kama taifa kuyawekea priority na commitment, maisha ya watanzania yatakuwa bora sana ndani ya kipindi kifupi tu, hata miaka 20 inaweza ikawa ni mingi;
Na mwisho ni kuhusu suala la Frog in the boiling Pot; umetoa mfano mzuri sana kwani mfano huu fits very well na hulka yetu watanzania; kwa mfano, tukiamua kupiga kelele za kroo kroo kroo, hakika majumbani hakulaliki; Pia tunajua wazi kabisa kwamba pamoja na udogo wetu, tuna uwezo wa kumwangusha Tembo ambae huangushwa na Simba peke yake, tena kwa taabu sana, kwani tembo lazima aje kunywa maji mtoni kwenye makazi yetu na tunajua siri ndogo sana ya pakumkamatia; This is similar to Wanasiasa wa CCM wanapokuja kwetu wananchi wakati wa msimu wa kuomba kura kila baada ya miaka mitano, na kutoa ahadi lukuki ambazo tayari kupitia uzoefu wetu, tunajua fika kwamba hazitekelezeki; but guess what, tunawarudisha madarakani wale wale;
Ningependa nimalizie na maneno ya Mwalimu Nyerere kwa UMMA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TANU mwaka 1970:
"I hope that both candidates in each election will be intelligent enough to recognize that not everything can be done at once, and that nothing in this world is FREE. For the fact is that if a person is urging more communal services or better communal services, he or she is probably also urging that you, as the voter, should be willing to pay more local rates or more taxes. For is they are promising lots of new activities if they are elected, and if they are promising that these will be done without any cost to you, or effort on your part, they are either deliberately misleading you – thinking you are fools or they themselves are fools"
Source: Socialism and Participation: Tanzania's 1970s Elections: The Elections Study Committee, UDSM (1974).