Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Wewe ni mmojawapo wa hao wengi wanaoamini hivyo?? M4C ni nadharia au tayari ni wazo litendalo kazi??Kwa mtazamo wa wengi, kiunganishi hicho ni M4C;
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mmojawapo wa hao wengi wanaoamini hivyo?? M4C ni nadharia au tayari ni wazo litendalo kazi??Kwa mtazamo wa wengi, kiunganishi hicho ni M4C;
M4C ni mwanzo mzuri wa kuelekea katika mabadiliko ya kweli, iwe ni mapinduzi au mageuzi yanayokaribiana na mapinduzi, huo ni uamuzi wa walio wengi - UMMA, na ni wajibu wa chama cha CCM na serikali yake kushughulikia chanzo (root-cause) cha vuguvugu hili kuliko kushughulikia matokeo;CCM ikikaa chini na kuamua kutumia akili timamu, itagundua chanzo ni CCM yenyewe;Wewe ni mmojawapo wa hao wengi wanaoamini hivyo?? M4C ni nadharia au tayari ni wazo litendalo kazi??
Shayu,
Mkuu wangu nimekusoma sana lakini kusema kweli sijakuelewa kabisa. Na nitasema kwa nini hasa? Kwanza kabisa umesema mwenyewe unataka kuelewa 'Movement for Change" ina maanisha nini? halafu maajabu umekuja na tafisri yako kwa jinsi unavyofikiria wewe. Ungesubiri basi hata ujibiwe kabla hujawapa jina jingine la - Movement for Power..
2. Haya nikikusoma chini umezungumzia mengi sana yanayohusu UTAWALA BORA na kusisitiza kumpata kiongozi bora atakaye weza kuleta umoja wa Taifa na kuonyesha dira na mwongozo lakini pia umezungumzia uwezekano wa chama kinaweza kuwa Reformed kwa kubadili mitazamo yake na mwelekeo wake kinapoona kinakosea, wanapobadilika wanaweza kubadili dira na mwelekeo wa nchi. Hapa nashindwa kabisa kuelewa kabisa unaelekea wapi...Chama kikibadilisha DIRA sasa huyo kiongozi bora ataweza vipi kuwa mbora ikiwa dira alowaonyesha wananchi inaweza kubadilika njiani..
3. Umezungumzia swala la wananchi wabadilike, Na sidhani kama kuna njia bora zaidi ya kwanza kulaani vitendo viovu, Huwezi kupambana na Ufisadi nje ya Utawala kwa kujenga sera isipokuwa kulaani vitendo vinavyohujumu uchumi wa nchi. Kupambana na Ufisadi ni hoja ambayo inatanguliwa na kuharamishwa, na kama hutaweza kuwajenga wananchi imani ya kuogopa na kulaani Ufisadi basi kazi nyingine zote hazitakuwa na maana yoyote. Umesema mwenyewe ya kwamba - Maendeleo ya kweli kwa jamii yeyote ile ni transformation ya roho, akili, mwili na mali, bila ya vitu vyote hivyo kukamilika binadamu hajakamilika kimaendeleo. Hivyo sioni kosa lolote la M4C inapohamasisha watu na kuwaeleza mabaya ya ufisadi kuwa sehemu ya mchango mkubwa wa umaskini wao
4. Nakushangaa tena wewe mwenyewe unapopingana na dhana ya wale walookoka kuwa sehemu ya mkusanyiko huo huo ukiwaita ni watu wa kuokota okota. Ikiwa mtu kakubali na kutiwa maji unataka nini zaidi ya mtu huyo kuhudhuria ibada za chama, kujumuika na wengine na kueleza kaweza vipi yeye kutambua ubaya wa Ufisadi na ama kufanya kazi chini ya uongozi shalimu. Kwa nini mtu huyu aendelee kuonekana hafai wakati wajibu wetu wa kwanza ni kuwabadilisha wananchi hao hao wapate kuyaona mabaya na hivyo nao wawe maswahaba wa kutangaza yalokuwa mema maana hawa wametoka ktk Mabaya..
Pengine unashindwa kuelewa kwamba mtu yeyote msafi ambaye hajawahi kupatwa na majaribio kama haya, huwa hajui upande wa pili isipokuwa huijua tu laana ya vitabuni. Lakini yule alokwisha kuwa Fisadi na akaungama anaweza kuwa mbora zaidi yako kwa sababu kisha onja joto la jiwe na anaijua tanmu na chungu ya Ufisadi. kajua jindsi gani anavyowakwaza watu wengine na hivyo he became a freeman..Ktk imani za Dini sisi wote tulikuwa wenye madhambi na tumeingia dini kujinasua ktk dhambi hizo na leo ndio tunafundishana neno la Mungu..
Umeendelea kuikejeri M4C kama ni propaganda tu. Hii ina maana wewe binafsi huja Imani na Uongozi wa Chadema wala kazi wanayoifanya. Sema ukweli tukusikie vizuri maana hakuna sababu ya kuficha uso kiamini. Hivyo ingekuwa vizuri zaidi kama ungetuambia wewe kwa nini huna Imani na viongozi wa Chadema, huna imani na M4C hadi ukafikia kusema watafanya yale yale ya CCM. Ni dalili zipi zinazokuonyesha wewe kuwepo uwezekano huo..
Labda nimalizie tu kwa kusema M4C ni sehemu ya harakati za kukijenga chama mikoani, na Chadema wamejieleza sana tena sii mahala pamoja. Wewe kama unafiiria ama unategemea kuwa hizi ni propaganda za kuwaweka IKULU hilo umelifikiria wewe lakini wenzako wanachokifanya ni kukipeleka chama kwa wananchi huko vijijini. Mwalimu Nyerere alifanya hivyo hata kabla ya kuomba Uhuru na haikuwa hoja ya Nyerere atawafanyia nini watanzania bali kuwanasua toka ktk Ubeberu wa mwakoloni...
Pengine ungeweza sana kuchangia hoja pale unapoona Chadema wanachelewa kujieleza wakiingia IKULU watafanya nini lakini pia umesahau ya kwamba wakifanya hivyo itaonekana wameanza kampeni za Uchaguzi mapema na kinyume cha sheria. Kama kweli unataka kujua Chadema kama chama kitaleta mabadiliko gani kwa wananchi basi soma SERA zao ktk tovuti yao na kama kuna jambo ambalo hukubaliani nalo liweke hapa tulijadili. Binafsi yangu miye kama Mtanzania, I can't wait kuona CCM wanaondoka madarakani kwanza halafu nitawapima Chadema kulingana na sera zao pamoja na ahadi watakazo zitoa. Leo hii ni mapema sana kutangaza watafanya nini wakiingia IKULU hiyo itakuwa kuvunja sheria na kanuni za uchaguzi mkuu...
Kiongozi makini ni nahodha ktk meli yetu hivyo tunachokihitaji ni ujuzi wake kutufikisha tunakotaka. SERA za chama ndio mwongozo wetu wote na ndizo tutakazo chagua njia hiyo kwenda ktk safari yetu. Chama hakiwezi kubadili dira isipokuwa wanaweza kubalidilisha priority zao kutokana na mazingira yaliyopo safarini.Ngoja nikwambie ndugu yangu, Binadamu ni jinsi anavyofikiri . Ni mawazo yake. Ninaposema chama kikibadili mitazamo yake kitabadili dira yake nilikuwa namaanisha chama kitakapobadili philosophia yao ya kutawala, kinaweza kubadili mwelekeo wake. Ni ukweli kwamba ubora wa kiongozi yeyote hutokana na ubora wa vile anavyofikiri. Ni wazi ya kwamba kiongozi yeyote yule bora huzalisha fikra bora na zenye manufaa. Na kiongozi mbovu ni kinyume chake.
Kitu ninachosema tena, kitu tunachohitaji katika Taifa letu ni Ku reprogramming peoples mind. Kwa kuingiza fikra mpya miongoni mwa mamilioni ya watu wa Taifa hili kuhusu Utaifa na kujenga umoja na malengo ya pamoja. Akili zetu zimefocus katika ubinafsi na sio utaifa hatutaweza kupiga hatua pasipo kubadili hiyo mentality. Mobilization ya watu ni kitu muhimu sana ili watu wawe malengo. Ili Taifa liwe na malengo. Nimeongea mengi sana kama ukinisoma kwa umakini utagundua umuhimu wa mambo mengi niliyoongelea. Nilazima tusukumwe na utaifa zaidi kuliko ubinafsi ili tujenge hilo na hili sijaliona katika CDM. Wamefocus zaidi katika kushika dola pasipo program makini ambazo wakiingia madarakani kwanza watabadilisha fikra za watu lakini pili wataleta maendeleo. Lakini pili sidhani kama viongozi wote waliohamia Chadema walifuata Sera au itikadi za chadema bali uongozi na kujinufaisha. Hapa ndipo tulipofikia kama Taifa.
Mtoa mada amekwazika padogo sana pamoja na maelezo marefu, anaifahamu njia ya kuleta maendeleo lakini hajaitambua. Ukisoma maelezo yako mwanzo mpaka mwisho unakiri kwamba kuna tatizo na uongozi uliopo, kuna tatizo la mfumo na kwamba kunahitajika mabadiliko. Lakini hujui ni kwa namna gani yatokee hayo mabadiliko. Mabadiliko chanya huanzia kwenye fikra, hayo yakiwa katika jamii ni lazima yataleta msuguano (sababu fikra za watu tofauti hazifanani). Iwapo kundi kubwa katika jamii litakombolewa kifikra na kuwa na muono unaokaribiana, hapo ndipo mabadiliko ya kweli yatatokea. Katika mabadiliko hutokea pia mabadiliko ya uongozi, na jamii yoyote ni lazima iwe na uongozi wake, hivyo wanajamii kutaka kuwa sehemu ya viongozi si uchu wa madaraka kama unavyoamini bali ni haki na wajibu wa kikatiba/ sheria na taratibu. Ndio maana haki hiyo iko wazi. Uchu wa madaraka ni neno la kifedhuli lililoasisiwa na walafi wa madaraka ambao kwao uongozi ni ufalme badala ya utumishi. Na sitoshangaa ukawa mmoja wa hao ambao wanaamini kwamba walizaliwa kutawala. C4M imelenga katika kufufua fikra huru, na kuwaamsha wananchi katika utumwa wa kuomba hisani kwa serikali waliyoiweka madarakani, badala ya kuituma kazi na kuiwajibisha inaposhindwa kutekeleza jukumu lake la msingi la kusimamia ustawi wa watu wake. Hii kazi ni ya kizalendo zaidi ya kudhani ni uchu wa madaraka, kwani wananchi wakipata uelewa wa kujua nguvu yao dhidi ya serikali, ndio utakuwa mwisho wa kukandamizwa na watawala dhalimu, wanaotumia ujinga wa watu kama nguzo ya kuficha uovu wao. Kutokana na M4C matunda yameanza kuonekana, watawala wanahaha kutumia kila mbinu ujumbe usizidi kuenea. M4C inaanza na wewe, just change, otherwise change will change you.(QUOTE)
Unapozungumza kukombolewa kifikra unazungumza kukombolewa kifikra kupi? Je ni kule kutakako mfanya kuwa raia responsible? na anayejitegemea kifikra? anayetambua yeye ni nani na ana nafasi gani katika Taifa lake? Anayeangalia familia yake na kulea watoto wake katika maadili? Lazima tutambue kila raia anawajibu kwa Taifa lake lakini pia ana haki zake kama raia. Tujiulize tunawajibika ipasavyo kwa hili Taifa? Je tunajitolea vya kutosha kulilinda, kuliendeleza kwa faida yetu na vizazi vijavyo? Kukombolewa kupi kifikra? Nationalism consciousness? Je watoto wetu wanaamini katika Taifa hili? mabadiliko ya kifikra ninayohitaji ni yale yatayopelekea watu wa Taifa hili kufikiria kuhusu Taifa lao na kulitumikia kwa umoja. Ukombozi upi wa kuiondoa CCM na kuiweka CHADEMA madarakani? Ni kweli kwa kuingia madarakani chadema fikra za watu zitabadilika kuhusu ufisadi na uwajibikaji? ''All this need a deep thoughts''
The notion that if we remove ccm all will going well is totally wrong. Kuna vitu vingi vya ku address vinavyohusiana na taifa hili kama tunahitaji ukombozi wa kweli sio siasa tu. We need to reprogram our people jinsi wanavyofikiri kuhusu Taifa lao tukiisha badili mitazamo yao kwa Taifa hili hiyo itakuwa hatua ya kwanza. Watu wetu watakapo lipenda Taifa hili itakuwa hatua moja kubwa ya maendeleo kwetu, they will be willingly to work for this country. So how we will mobilize our people ili walitumikie Taifa hili? Ni pale tu tutakapoweza kuzitoa akili za watu kutoka katika ubinafsi na hii itawezekana kama tutakuwa ni Taifa lenye malengo na Dira na sio Taifa la watu wanaotafuta Mkate tu wa kula kila siku. Swali kubwa la kujiuliza tutawezaje kutoka hapa tulipo? hii inahitaji jitihada kubwa za pamoja. Kama watu wetu watakuwa na spirit moja ya kutaka maendeleo ya Taifa hili kwanini tusifanikiwe?
Swali kama tutawatoa maadui zetu ambao ni mafisadi wa CCM hatua ya pili itakua nini tumejitayarishaje kutawala katika misingi ya haki na wajibu? kuwaongoza watanzania katika umoja na malengo? Naamini kabisa Chadema inaweza kuingia madarakani lakini haitokuwa Tofauti sana na CCM na pengine baadae pengine kitaibuka chama kingine ambacho kitadai ndio mkombozi wa kweli wa Watanzania. Katika andiko hili nimeongelea kuhusu chama ambacho kitaikomboa hii nchi kinatakiwa kiweje kama ulinisoma vizuri. Ili tulikomboeTaifa hili lazima tujadili issues zinazolikwamisha hili Taifa zote kabisa na jinsi gani tutatatua hayo matatizo, kitu tunachohitaji ni Taifa hili kusonga mbele katika umoja wake.
Ndugu yangu, kuna maneno ya hekima sana tuliachiwa na Hayati Mwalimu Nyerere ni maneno mazito sana na yanahitaji wenye hekima kuyafasiri. "Ili tuendelee tanahitaji mambo manne 1. Watu 2. Ardhi 3. Siasa safi 4. Uongozi bora". Sasa matatizo yetu kimsingi yanatokana na kushindwa kuelewa hii falsafa. Kwamba tuanze na nini, na kwamba tunadhani tunavyo vitu hivyo. Falsafa hii nzito inatuambia ili tuendelee tunahitaji kuwa na watu kwanza, na watu si idadi bali ni skills (skilled personel is the key to almost every problem), tujengee watu uwezo (empowerment), si kuwajaza mafedha such as JK idea, but uwezo wa kiakili na kimaadili. Na hapa ninamaanisha, elimu ya utambuzi na ujuzi sio hii brain wash education. Ukiwa na taifa lenye watu walioelimika, watafanya kazi kwa tija, wataongozana kiufanisi. Lakini ili yote yafanikiwe ni lazima kuwe na uongozi bora. Hii combination ndiyo inayokosekana, hivyo ni lazima tukubali kubadili mfumo wa uongozi. Na mwisho kaka, wewe na mimi na yule ndio tunaoweka serikali madarakani, na ndio tunaoweza kuiondoa. Kama hatujitambui, tutabaki kuwa watumwa wa nafsi.Unapozungumza kukombolewa kifikra unazungumza kukombolewa kifikra kupi? Je ni kule kutakako mfanya kuwa raia responsible? na anayejitegemea kifikra? anayetambua yeye ni nani na ana nafasi gani katika Taifa lake? Anayeangalia familia yake na kulea watoto wake katika maadili? Lazima tutambue kila raia anawajibu kwa Taifa lake lakini pia ana haki zake kama raia. Tujiulize tunawajibika ipasavyo kwa hili Taifa? Je tunajitolea vya kutosha kulilinda, kuliendeleza kwa faida yetu na vizazi vijavyo? Kukombolewa kupi kifikra? Nationalism consciousness? Je watoto wetu wanaamini katika Taifa hili? mabadiliko ya kifikra ninayohitaji ni yale yatayopelekea watu wa Taifa hili kufikiria kuhusu Taifa lao na kulitumikia kwa umoja. Ukombozi upi wa kuiondoa CCM na kuiweka CHADEMA madarakani? Ni kweli kwa kuingia madarakani chadema fikra za watu zitabadilika kuhusu ufisadi na uwajibikaji? ''All this need a deep thoughts''
The notion that if we remove ccm all will going well is totally wrong. Kuna vitu vingi vya ku address vinavyohusiana na taifa hili kama tunahitaji ukombozi wa kweli sio siasa tu. We need to reprogram our people jinsi wanavyofikiri kuhusu Taifa lao tukiisha badili mitazamo yao kwa Taifa hili hiyo itakuwa hatua ya kwanza. Watu wetu watakapo lipenda Taifa hili itakuwa hatua moja kubwa ya maendeleo kwetu, they will be willingly to work for this country. So how we will mobilize our people ili walitumikie Taifa hili? Ni pale tu tutakapoweza kuzitoa akili za watu kutoka katika ubinafsi na hii itawezekana kama tutakuwa ni Taifa lenye malengo na Dira na sio Taifa la watu wanaotafuta Mkate tu wa kula kila siku. Swali kubwa la kujiuliza tutawezaje kutoka hapa tulipo? hii inahitaji jitihada kubwa za pamoja. Kama watu wetu watakuwa na spirit moja ya kutaka maendeleo ya Taifa hili kwanini tusifanikiwe?
Swali kama tutawatoa maadui zetu ambao ni mafisadi wa CCM hatua ya pili itakua nini tumejitayarishaje kutawala katika misingi ya haki na wajibu? kuwaongoza watanzania katika umoja na malengo? Naamini kabisa Chadema inaweza kuingia madarakani lakini haitokuwa Tofauti sana na CCM na pengine baadae pengine kitaibuka chama kingine ambacho kitadai ndio mkombozi wa kweli wa Watanzania. Katika andiko hili nimeongelea kuhusu chama ambacho kitaikomboa hii nchi kinatakiwa kiweje kama ulinisoma vizuri. Ili tulikomboeTaifa hili lazima tujadili issues zinazolikwamisha hili Taifa zote kabisa na jinsi gani tutatatua hayo matatizo, kitu tunachohitaji ni Taifa hili kusonga mbele katika umoja wake.
umeandika theory ndefu za darasani! Nchi yenye wananchi desperate kama TZ inahitaji mabadiliko ya aina zote na yoyote!! Jiunge na M4C utoe mchango wako wa mabadiliko. Hizo "mindset change" unazorejea ni mchakato wa mabadiliko. Lakini kwanza tunahitaji mabadiliko yatakayotoa nafasi yote ya mawazo mazuri kama yako!! Kumbuka nadharia hugeuka vitendo kwa commitment tu!!Chadema wanapozungumzia (M4C) wana maanisha nini? M4C inasimama badala ya movement for Change ina maana kubwa.
Mabadiliko kama mabadiliko yana maana na dhana kubwa mno ambayo inahitaji umakini kujadili kwa kina.
Dhana ya M4C ya chadema sijaielewa kabisa. Ndio maana mimi naiita movement for power na hii M4C ni kivuli tu cha kufikia malengo yao ambayo kwa uhakika sio yenye malengo ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu.
Msuguano uliopo sasa hivi kati ya CCM na Chadema ni msuguano wa kugombea madaraka na hauna chochote cha kufanya kwa mabadiliko ya umma. Ni uchu ule ule wa madaraka unawaongoza viongozi wengi wa Afrika hadi kuleta machafuko katika nchi zao. Sioni tumaini lolote kwa watu wa Taifa hili litakaloletwa na watu wa vyama hivyo hata kidogo.
Tunahitaji uongozi na mwelekeo, hatujui tunapoelekea kama Taifa. Tunahitaji uongozi. Taifa hili halitopata mabadiliko yeyote pasipo uongozi. Tunahitaji kuondoka kutoka hapa tulipo. Hatuwezi kuondoka hapa tulipo pasipo Order. Na order huletwa na kiongozi madhubuti. Anayejua nini nachotaka kufanya na wapi anataka kulipeleka Taifa. Kiongozi atakayeleta umoja wa Taifa na kuonyesha dira na mwongozo. kiongozi atakayeaminika kwa wanachi kwa maneno na matendo. Atakayeonyesha mfano kwa vizazi vijavyo. Kwamba hii ni njia ambayo kama Taifa tunapaswa kupita, kwasasa mapito yetu kama Taifa hayajulikani. Kwasasa siioni baadae yetu itakuwaje hakuna tumaini la baadae na haijulikani Taifa hili litakuwaje, hakuna tumaini.
Tumaini la vizazi vyetu liko gizani kutokana na kukosa uongozi. Sisi kama taifa tunapaswa kukusanya nguvu na kukua. Lengo la Taifa lolote ni utawala na uongozi wa dunia hatujawa Taifa ili tuwe wa mwisho au tutawaliwe daima. Ni lazima tukue kama Taifa na tuonyeshe uwezo wetu na hili litafanikiwa kama tukiwa wenye nia moja.
Tunahitaji kiongozi atakayeleta tumaini na mwelekeo katika Taifa letu, tumaini ambalo limeondoka miongoni mwa mamilioni ya watu wa Taifa hili. Umoja wetu ndio msingi wa kukua na kuendelea kwa Taifa hili. Hatuwezi kukua kama kila mtu atajiangalia mwenyewe na kuacha yale ambayo yametuunganisha kama Taifa. Tutaendelea haraka zaidi na kwa kasi kama tutakuwa wamoja na kila mmoja wetu kama atajitolea kwa moyo wake wote kulijenga Taifa hili na kulipenda. Kitu ambacho kimetuunganisha sisi ni Taifa letu na ni lazima tulijenge na tuwe na mapenzi nalo.
Hatuwezi kuendelea kama tutakandamizana wenyewe kwa wenyewe tabaka moja likijiona bora zaidi ya jingine. Tutaendelea kama tutaheshimiana kama watu wa Taifa moja na wenye nia na dhamira moja ya kulijenga Taifa hili hadi kufikia kilele chake cha maendeleo na ukuaji.
Taifa limekosa uongozi ni Taifa la watu walalamikaji hakuna anayeonyesha uongozi kwa kile kinachopaswa kufanywa kama Taifa. Watu wetu lazima wajue Taifa lao linaelekea wapi na ni nini wanaamini kama TAIFA.
Taifa letu liko katika mgawanyiko mkubwa na kutoridhika kwa watu wake juu ya mwelekeo na baadae ya Taifa. Tunahitaji tumaini hili linyanyuke. Tumaini hili ambalo wazee wetu waliopigania uhuru katika Afrika waliokuwa nalo, kuiona Afrika ikijitegemea na kuwa huru. Hili ni tumaini ambalo lazima liwepo mioyoni mwetu wote na ni lazima lifanikishwe kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Hatutaweza pasipokuwa na uongozi wenye maono, pasipo uongozi imara Afrika itaendelea kudumaa na kuwa tegemezi Daima. Lakini Afrika na Tanzania inahitaji kukua. Hii ni changamoto ambayo tunayo na inahitaji jitihada zisizofifia ili kuikamilisha ndoto yetu ya kuwa huru na watu wanaojitegemea. Sidhani pasipo umoja tunaweza kufaniisha hili. Tunahitaji viongozi wasio wabinafsi ili Afrika na Tanzania ikue. Tunahitaji viongozi wasio tetereka katika dhamira zao kuifanya Tanzania na Afrika kuwa huru na zenye kujitegemea. Hii ni vita na ni lazima ipiganwe.
Tunachangamoto katika taasisi zetu ambazo ndizo mashine katika maendeleo yetu kama Taifa. Kuna kutoridhika na kukosa uzalendo miongoni mwa wasomi wa Taifa hili. Matatizo katika mifumo yetu ya elimu na Afya. Ambayo imepelekea migogoro ya mara kwa mara baina ya serikali na watumishi hawa wa umma.
Ni dhahiri lazima tufahamu kwamba sisi sote lazima tuwe na dhamira moja ya kulijenga Taifa hili na hatutaweza kulijenga Taifa hili pasipo juhudi za pamoja na kujitolea kwa upande wa serikali na kwa upande wa watumishi wa UMMA. Serikali inawajibika kuwapelekea nyenzo na kila msaada ambao utasaidia watumishi wa umma kufanikisha kazi yao ya kutumikia umma. Lakini watumishi wa umma wanawajibika kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu kutumikia watu wa Taifa lao na kuwa na mapenzi kwa Taifa lao. Hatutaweza kulisukuma gurudumu la Taifa hili pasipo jitijada za pamoja na dhamira ya pamoja.
Lazima tutengeneze serikali ya watu ambayo raia na viongozi wao watakuwa pamoja katika jitihada zao za ujenzi wa Taifa lao, kwa manufaa yao na sio kikundi kidogo cha watu au chama. Hili ni TAIFA ambalo nalihitaji ambalo kila mtu anachangia katika maendeleo ya Taifa lake kwa moyo mmoja na kujitolea, kila mtu akitambuliwa kutokana na mchango wake na kuheshimiwa. hili ndilo Taifa ninalohitaji.
Taifa ambalo litamwezesha mtu kukua na kukuza kipaji chake. Taifa la watu huru na wanaofuata na kuheshimu sheria zilizo tungwa kwa misingi ya Haki. Haya ndio mabadiliko ninayoyahitaji na hii ndio M4C INAYOHITAJIKA KUWEPO Kubadili mitazamo ya watu kutoka katika ubinafsi kuja katika utaifa ili tujenge Taifa hili kwa moyo mmoja na kujitolea. Hatutaweza kubadili taifa hili kama hatutakuwa wamoja. Badiliko ya kweli ni kubadili fikra na mitazamo ya watu kuhusu Taifa lao, na watakapo fikiria chanya kuhusu Taifa lao hapo ndipo mabadiliko yatakapo tokea. Ya kwamba tuna uwezo wa kukua na tunauwezo wa kuendelea na kuwa kama Taifa lolote kubwa haya ndio matumaini yangu.
Watu wa Taifa hili wanahitaji kukua, wanahitaji kuona Taifa lao likinyanyuka na kuendelea, wanahitaji kuona Taifa lao likiwa Imara wamechoshwa na udhaifu. We will only achieve this if we have strong leadership. We can move as the Nation, we can be strong and independent. We have that potential.
Tuna mapambano mawili kuwaondoa viongozi mafisadi wote nchini mwetu lakini tunawajibu wa kulijenga na kuliendeleza Taifa hili kwa moyo wetu wote bila kubakiza kitu. Mapambano yetu sio kuondoa ufisadi tu bali kujenga nchi. Kujenga jamii zetu na kuleta ustaarabu. Kuleta umoja wa kitaifa na Wajibu. Tunaweza kuondoa chama kimoja tukikiingiza chama kingine cha kifisadi na nchi yetu ikaendelea kuwa palepale. Kinachojalisha ni mawazo mapya yatakayokuja na kubadilisha dira na mwelekeo wa Taifa hili kama upepo wa kisulisuli. Kuleta uzalendo na uwajibikaji katika Taifa.
Mabadiliko ya kweli katika Taifa hili yatakuja kutoka katika mabadiliko ya Fikra na Chama. Kwakuwa chama kinaweza kuwa Reformed kwa kubadili mitazamo yake na mwelekeo wake kinapoona kinakosea, wanapobadilika wanaweza kubadili dira na mwelekeo wa nchi.
Chadema na movement for Change ni propaganda tu. Wanaweza kuingia madarakani lakini maisha ya watu yakaendelea kuwa duni na yasiyo na matumaini. Sioni tofauti kati Ya CCM na CHADEMA katika mawazo yao na jinsi wanavyoendesha siasa zao. Hawawezi kulikomboa Taifa hili wala kuleta matumaini kwa waliokata tamaa. M4C is the movement for power. We are going to replace one tyranny with the Other. Uhuru wa kweli na maendeleo bado ni mgumu kwa aina za siasa ninazoziona.
The only true revolution is by changing the way people are thinking, by implementing new ideology and new values. We can not develop by the same thinking and the same values, we must change how we think. Watu wetu lazima waelewe hili tunalijenga Taifa letu kwa mawazo yetu, ubora wa mawazo yetu ndio ubora wa Taifa letu. Tunahitaji kiongozi atakayeleta mawazo mapya, mwenye akili na maono.
Lengo la kiongozi yeyote yule makini ni kuleta watu pamoja ili kujenga Taifa lao kwa manufaa yao kwa pamoja. Binadamu amepata maendeleo makubwa pale tu walipoanza kuishi pamoja na kuundwa serikali zao kwa manufaa yao. Hatujaunda serikali kusudi itawale na kunyima haki raia. Siasa ni chombo pekee chenye uwezo wa kukusanya watu kwa kushawishi juu ya faida ya pamoja tutakayoipata kama tutafanya jambo fulani kwa faida ya sasa na ya baadae ya taifa. Ni Siasa iliyokusanya watu na kuwa mataifa. Watu walishawishika kuunda mataifa kwasababu ya faida ya pamoja itakayopatikana kutokana na mtu kuishi katika Taifa. Siasa ikiwa chanzo cha vurugu na mgawanyiko katika Taifa hupoteza maana yake. Viongozi wenye uchu ambao hawafikiria chochote zaidi ya faida ya kipindi kifupi na sio baadae yetu na baadae ya vizazi vyetu.
Tuna kitu kimoja cha kufanya na kilichotuunganisha. Ni Taifa hili. Ni Tanzania. Naweza kukuita ndugu yangu kwakuwa tunaishi Taifa moja. Taifa hili likizama wote tunazama. Baadae ya Taifa hili inatutegemea sisi hakuna atakayejenga baadae yetu zaidi yetu. Kitu pekee ninachotaka kukiona ni kuliona Taifa hili likinyanyuka na likichukua nafasi yake katika Dunia. Hili ni tumaini ambalo kila mmoja wetu lazima awe nalo na kila mtu atakaye kabidhiwa mamlaka ya uraisi lazima awe nalo, kuwanyanyua watu wetu kutoka hapa tulipo. Sio ubinafsi na wala sio maslahi ya Chama bali dhamira yetu ya kulifanya Taifa hili liwe kubwa iliyozama ndani ya mioyo yetu. Ni lazima tuamini hivi ama sivyo hatutafanikiwa. Ni lazima tuamini tunauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama Mataifa mengine na tutie jitihada kwa kufanikisha hilo.
Tumekuwa Taifa kutoka katoka katika makabila, koo na familia. Tumeunda kitu kimoja. Nguvu yetu itategemea sana umoja wetu pasipo kuangalia tofauti zetu za kikabila wala kidini ila dhamira yetu ya pamoja ya kujenga Taifa imara kwa vizazi vingi Vijavyo.
Mabadiliko ya kweli yatakayo likomboa Taifa hili ni mabadiliko ya fikra na mitazamo ya Watu. Tukifanikiwa kubadilisha mitazamo ya watu. Tutafanikiwa kubadilisha tabia na mabadiliko ya kimatendo tutarudi katika Taifa letu na kulitumikia kwa pamoja kwa maslahi ya wote.
Ni lazima tuangalie upya dhamira zetu kwa Taifa hili. Na tuwe wa kweli wa nafsi. Tujenge undugu wa watu wa Taifa moja. Tufikiri na kuamua mambo kutokana na fikra sahihi. Taifa hili litajengwa na busara na maono yetu.
Swali langu kwa Chadema movement for Change what change the want to bring in our country? Kuibadilisha CCM na kuwaweka wao madarakani? Watanzania wanahitaji zaidi ya hilo. Wanahitaji heshima na maendeleo ya Taifa lao. Wanatakiwa kutushawishi ni aina ya Taifa gani wanataka kulijenga. Tunu gani wanataka kuziweka kwenye Taifa letu na mwelekeo wao ni upi kama Chadema ni nini wanaamini? Wataleta matumaini gani kwa Tanzania? Tumeona katika Afrika vyama vingi vilikuja kama wakombozi wa wananchi lakini viliishia kuwa vyama visivyo kuwa na dira na vya kifisadi.Kwasababu waliongozwa na uchu ul ule sawasawa na wa watu walioko madarakani. Watanzania awahitaji ku replace tyranny with another Tyranny wanahitaji uhuru na maendeleo.
kitu Tanzania inachohitaji ni programmu itayobadili mitazamo na fikra za watu wetu juu ya nchi yetu. Kuingiza mioyoni mwa watu roho ya kulitumikia Taifa na uzalendo kwakuwa bila vitu hivi viwili Taifa haliwezi kusonga mbele. Bila umoja kamwe hatutaweza kusonga mbele. Lakini TAIFA hili linahitaji kukua na kusonga mbele katika umoja wetu. Naamini kabisa kama tukiwa wamoja na tukiwa determined kuliondoa Taifa hapa lilipo tunaweza.
Najua watu wa Tanzania wako katika Great distress na wamepoteza matumaini. Wengi wao wanajihisi sio sehemu ya Taifa hili. Tuna tatzio ni sawa na Chama kilichopo cha CCM ambacho kwa hakika hakina uhalali wa kuendelea kuwepo kutokana na ufisadi na kushindwa kuliongoza Taifa hili. Lakini pia vyama vyetu vya kisiasa vingi haviko imara kuleta mabadiliko ambayo tunahitaji ya kifikra, Wame focus mno katika kuitoa CCM madarakani bila kutayarisha programmu mbadala kwaajili ya kuleta mabadiliko kwa watu wa Taifa hili.
Chama chochote kitakacholeta mabadiliko katika Taifa hili ni kile ambacho kina maadili ndani yake. viongozi wake wana discipline na wanaheshimiana. Chenye ideology inayoeleweka na inayosambazwa kwa wananchi ili waijue na wajue chama chao kikiingia madarakani kitawafanyia nini. Kisicho okota okota ovyo viongozi wa kugombea katika majimbo bali kuwatayarisha katika maadili na discipline ya hali ya juu. Chenye Viongozi wanaoheshimu familia na majirani. Chenye watu wanaopenda jamii na kujitolea kujenga jamii.
Maendeleo ya kweli kwa jamii yeyote ile ni transformation ya roho, akili, mwili na mali, bila ya vitu vyote hivyo kukamilika binadamu hajakamilika kimaendeleo. Kwahiyo maendeleo ya binadamu sio ya mali tu lakini ya vile anavyofikiri, roho yake na ubora wa afya yake. Katika Taifa hli tunahitaji Order na bila order tunatambua taifa lolote halitoweza kuendelea. Na order hii itakuwepo tu kwa kuwa na viongozi wanaoheshimiwa na jamii. Utii huu wa jamii kwa kiongozi wao utakuja tu viongozi pale watakapojiheshimu na kuwa wa kweli na kuangalia mienendo yao ya kimaadili. Tunahitaji kiongozi atakayesema na watu kumsikiliza na kuhimiza utii wa sheria.
Tunawalea watoto wetu bila kufahamu haki zao na wajibu wao kwa Taifa kama Raia.
kila raia ana haki na wajibu kwa Taifa lake. Wajibu huu lazima uwe ndani kabisa ya kila mmoja wetu. Kwasababu sisi sote kama Taifa tumeungana kwa sababu ya lengo fulani, kuna sehemu tunahitaji kufika kwa pamoja, ni lazima tuwe na dira. Dira hii itapatikana kwa viongozi wenye maono. Kwahiyo kuwa wamoja ni muhimu. Hatuwezi kugawanyika kama Taifa tukafikiri tutafika popote hakuna. Those who are sincere in their hearts and speaks truth will bring direction to this Nation. Hatutaweza kuleta dira katika Taifa hili kwa propaganda na uongo. Sisi ni watu wamoja na muelekeo wetu ni mmoja. Hatutaweza kuleta ukombozi wa Taifa hili kwa style hii tunayoenda nayo.
Kwahiyo nina wasiwasi na Vuguvugu hili ambalo vijana wengi wanaliamini litabadili maisha yao. Ukweli ni kwamba vijana wa Taifa hili kwanza ni lazima wabadili tabia zao na kuwa watu wa kufikiri zaidi na watu wa kulipenda Taifa hili kiukweli. Wawe raia wanaowajibika kwa Taifa lao na wenye maadili. Kwasababu wao pekee ndio wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa Taifa hili kama wana fikra sahihi na kama ni wamoja na wazalendo. Kuna tatizo la kimaadili miongoni mwa vijana hili i lazima tulisema na baadae ya Taifa lolote inategemea sana vijana wao wamewaandaaje. Hii ni kazi ya wazazi katika familia na shule. Kwahiyo ni lazima tuangalie upya uundaji wa kijana wa Taifa katika fikra sahihi ili tupate raia bora.
Tunaweza kubadili CCM na kuwaweka CHADEMA ili kubadili chama tu. Lakini bila programmu sahihi na watu sahihi ili kubadili fikra za watu wa Taifa hili , Taifa letu litaendelea kubaki palepale bila kupiga hatua yeyote kubwa. Kwasababu bila Order katika jamii Taifa lolote halitoweza kupiga hatua. Na order hii inaenda deep mpaka ngazi ya familia. Ni jinsi gani tunaendesha familia zetu katika misingi ya adabu? Je tuna akina baba wawajibikaji wanaoweza kutawala familia zao katika misingi bora? Taifa huundwa katika ngazi ya familia. Ubora wa Taifa lolote hutegemea ubora wa familia. Lakini familia haiishi peke yake kuna majirani na mahusiano yakiwa mazuri katika ngazi hiyo ni hatua moja kubwa ya kuwa na mahusiano mazuri ya kitu kilichokikubwa zaidi ambacho ni Taifa. Bila mahusiano haya kama Taifa hatutapiga hatua. Kwahiyo Taifa letu linahitaji Social reformation, political reformation na economic reformation. Lakini kitu muhimu zaidi ni mahusiano yetu kama Taifa na kama mtu mmoja mmoja. Tukifikia hatua hii tutakuwa tayari kumpigania mtanzania mwenzetu hata mmoja atakapopata matatizo katika mataifa mengine. Ni lazima tupendane kama Taifa na kama mtu mmojammoja.
Mwisho Taifa hili linahitaji busara. Ni kiongozi mwenye busara na maono tu, atakayeweza kuliongoza taifa hili na kulitoa hapa lilipo. Atakayeunganisha vipande vilivyopo ili vifanye kazi kwa ufanisi na kutoa mazao. Tuna watu wa fani tofauti na vipaji tofauti lakini hatujafanikiwa kwasababu tumekosa kiongozi atayeunganisha vipande hivyo ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi. We are not a well productive society kwasababu tumekosa a Leader. Ambaye kila mtu ata m admire na kumsikiliza because of ''intellegent, wisdom and Virtue''
Mtatoa mawazo mazuri yanayotakiwa kuzingatiwa lakini sitegemei mpumbavu/punguani/taahira yoyote kujitahidi kutetea mfumo na uongozi uliopo!! eti CCM No never!!M4C ni kiini macho cha kupata dola fullstop. hamna mikakati mahsusi ya kubadilisha serikali na mifumo yake kadhaa wa kadhaa ikiwemo. Kwa mfano hii theme ya ufisadi inayotawala siasa zetu kwa sasa, si Mbowe wala Dr Slaa aliyediriki kwenda hatua moja mbele na kusema hatua gani mahsusi zitachukuliwa kwa wahusika hawa pindi wakipata dola na hii ni uvugu vugu usioendana na matakwa ya watz wengi. Kwenye kura za maoni za katiba mpya wapo wananchi wengi wanadiriki bila haya wala kuulizwa kwamba wasisahau katiba kuwashughulikia mafisadi kwa adhabu kali ikiwemo kunyongwa, sasa CDM hawako page moja na kiu ya mageuzi hapa Tz namna hii.
A movement ni mass mobilization ya wananchi ili kupata nguvu kubwa ya kuwawakilisha hawa watu na mawazo yao na kutekeleza kiu yao ya muda mrefu, bila CDM kuoanisha taswira ya jamii (siyo lazima wawanyonge wahusika wa ufisadi ili kuuzika ufisadi wenyewe ) na yao inayolalia kwenye mantiki ya kua Taifa linahitaji kua tune up kidogo tu kwa kubadilisha vipaumbele na chama, kwa hili CDM naweza kusema siyo msemaji wa wanachi wa ukweli.
Ili M4C iwe ni mageuzi halisi ni lazima CDM wachore mstari chini waseme watabadilisha kabisa-a total overhaul of a system na siyo kua vugu vugu kama walivyo wenyewe. Change hapa siyo tu kubadilisha chama na sura zile za juu, ni kufukia kabisa mfumo ulioshindwa na wahusika wake waliopita. Kwa nini hatusikii marekebisho ya mikataba ya madini, kurudisha nyumba za serikali, kufilisi wahusika wa ufisadi, sheria za ardhi kwa wazawa, makazi mijini na nyumba za NHC kwa watz wakima cha kati (mnaogopa misaada ya Sabodo), mapinduzi ya kielimu (labda kutumia kiswahili mashuleni), mahakama maalumu kwa ajili ya kesi za ardhi n.k haya ni machache tu tunayotaka sisi wapenda mabadiliko na siyo kubadili rangi za chama na sura, mifano hii ndiyo mageuzi ya ukweli na siyo kupita pita kuikosoa serikali bila kuonyesha kwa kina nyinyi mtaleta nini.
Ndugu yangu, kuna maneno ya hekima sana tuliachiwa na Hayati Mwalimu Nyerere ni maneno mazito sana na yanahitaji wenye hekima kuyafasiri. "Ili tuendelee tanahitaji mambo manne 1. Watu 2. Ardhi 3. Siasa safi 4. Uongozi bora". Sasa matatizo yetu kimsingi yanatokana na kushindwa kuelewa hii falsafa. Kwamba tuanze na nini, na kwamba tunadhani tunavyo vitu hivyo. Falsafa hii nzito inatuambia ili tuendelee tunahitaji kuwa na watu kwanza, na watu si idadi bali ni skills (skilled personel is the key to almost every problem), tujengee watu uwezo (empowerment), si kuwajaza mafedha such as JK idea, but uwezo wa kiakili na kimaadili. Na hapa ninamaanisha, elimu ya utambuzi na ujuzi sio hii brain wash education. Ukiwa na taifa lenye watu walioelimika, watafanya kazi kwa tija, wataongozana kiufanisi. Lakini ili yote yafanikiwe ni lazima kuwe na uongozi bora. Hii combination ndiyo inayokosekana, hivyo ni lazima tukubali kubadili mfumo wa uongozi. Na mwisho kaka, wewe na mimi na yule ndio tunaoweka serikali madarakani, na ndio tunaoweza kuiondoa. Kama hatujitambui, tutabaki kuwa watumwa wa nafsi.
Aisee Nimekuelewa ipasavyo kwa uliyoandika nafikiri tuko pamoja ila tunatofautiana mahali padogo sana ni wote kwa hakika ni wazi tunahitaji mabadiliko.
Wanagombania kututawala sio kutongoza.
Kwa mantiki hii, Kama wangekuwa wanajua na kufuata njia ya kuondokana na ufisadi, kwa nini wasiwafukuze mafisadi au kuacha kuwapa nafasi za uongozi? Hata hivyo sasa tunajua bila shaka yoyoye kwamba ufisadi ni moja ya 'sera bubu za CCM' Na kwa misingi hiyo pamoja na ahadi nyingi za uongo ambazo hutolewa kwa wananchi wakati wa uchaguzi, maisha bora kwa Kila mtanzania yataendelea kuwa ndoto chini ya CCM.
I am inspired by the commitment of the M4C campaigners. Bravo, guys! You have our all salutes towards 2015.