Swali Umezungumzia kushuka kwa elimu, je utashughulikiaje wanaofoji vyeti na kuingia kufundisha vyuoni
Swali, kwa nini baadhi ya wananchi wanawaona wanaharakati kama wapiga kelele tu
Majibu,
Dr. anaanza na swali la mwisho, anasema yeye mwenyewe ni mwanaharakati, anasema NGO Serious zinatakiwa zipewe nafasi, na NGO briefcase ziwe discouraged. Kwa hiyo wanaharakati ni muhimu sana na wapewe support.
Swala la Uwoga wa itakuwaje CCM ikiondoka,
Hakuna shule ya Uraisi duniani, uraisi ni kwanza Mwenyezi Mungu akikubari, pili Busara na hakina, pia jamii unaishirikisha kiasi gani, pia Ukweli na uwaz… (missed some points here sorry!!)
Anasema anaukaribu sana na wananchi na wanamwelewa kwa kuwaambia ukweli.
Anasema ni maafa kuendelea kuwa na CCM, wengine wanalala kitanda cha ngozi wakati mafisadi wana magorofa, watanzania waondoe woga.
Sababu moja ya kubadilisha mfumo wa elimu ni kutengeneza mazingira mazuri ya Ajira. Tanzania kumekuwa na kasumba kuwa ajira ili ziwepo ni lazima aje mwekezaje, anasema hizi ni fikra mgando na ni tatizo la kutokuwa na plan,
Anasema kila mwaka kuna mabilioni ya pesa kwa ajili ya elimu ya watu wazima, lakini hazifanyi kile zinazotakiwa kufanya na watanzania hawajui hilo.
Anasema lazima pesa hizo ziwasaidie watanzania, anasema mikopo inatolewa na zinaliwa na wajanja na waziri anakili bungeni kuwa zimekwenda kwa wajanja, huo ni ubabaishaji
Swala la kutunza kura
Kura inadhamani kuliko shati, mbona shati haliibiwi, kwa nini kura ziibiwe,
Karatu iko Tanzania, moshi iko Tanzania, tarime pia, kwa nini kule zisiibiwe na kwingine ziibiwe, ni kwa sababu wananchi waliamua kuzilinda, kwa nini wewe usizilinde? Kura ni maji, kura ni Elimu, kura ni maendeleo, kwa hiyo basi inatakiwa zilindwe.
Anaongelea swala la mafisadi, jinsi ambavyo kikwete ameshindwa kuwashughulikia. Anasema haiwezekani mtu akaiba mali ya uma ukamwaacha anadunda, anasema ni kwa kuwa kikwete alifaidika na ufisadi kwa hiyo hawezi kuwafanya kitu.
Chadema haitaruhusu Fisadi adunde mitaani, ukiiba unashughulikiwa.