Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 402
Ngoja tusubiri watakavyotoka sisi m kesho manake Rais Mtarajiwa ameongea kwa kujiamini kabisa. Tutamsikia mzee anayelisha familia yake kwa propaganda bw(bi?) tembweleza.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninavyo jua mimi Kuchakachua ni kubadilishabadili/kuangaunga, je hapo juu uliimanisha nini au hili neno maana yake nini?tunamshukuru sana Dr Slaa ameweza kuchakachua vyema msimamo wa chadema kabla na baada ya uchaguzi
Mkuu bila kuomba radhi umetenda haki kabisa.Anaongelea nyumba za Tembe na Majani, mtu ananyumba imekaribia kuanguka lakini ameweka picha ya chagua kikwete, anashangaa sana.
Dr. ana data ya pesa ambazo CCm wamelipia mabango na hayajalipiwa ushuru, anasema kama haya yanawezekana kutapanya mabango nchi nzima, je elimu ya mtoto wako haiwezekani,
Kama unaweza kwenda kunywa chain a obama, kwa nini useme elimu bure haiwezekani?
Dr. anasema yuko tayari kula mihogo ikulu ila elimu iwe bure.
Anasema pesa ziko zimesambaa kote kwenye idara za serikali, kinachotakiwa ni uwajibikaji. Anasema kila mahali kuna uchafu, miezi ya kwanza ni kurekebisha na kurejesha uwajibikaji. Kwenye swala hili ametoa mifano kibao alipokuwa somewhere mawilayani.
Anataarifiwa kuwa zimebaki dakika saba, anatoa points za mwisho mwisho
Anawashukuru sana watanzania
Anawaomba radhi majimbo ambayo ameshindwa kufika leo kwa sababu ya wimbi zito
Anasema katika siku 71 ni vigumu kufika majimbo yote hata kwa kutumia helikopta, ila anawaomba wote kura zao.
Anasema yeye hataki kuona damu ya mtanazania inamwagika
Anasema Tanzania itakuwepo hata baada ya uchaguzi
Anasema kwa siku nane zilizobaki, ukipigwa kofi basi geuza la pili maana hautakufa
Anasema, ukitaka kumuumiza aliyekupiga, wewe mpuuze, inauma zidi ya kulipiza kisasi
Anamwomba kikwete awe makini, anasema vurugu zitaletwa na serikali, na polisi na watendaji wengine, ametoa mifano ya mwanza, ambapo hakulindwa na polisi, vijana wakajitokeza kumlinda.
Mwisho, anawaomba watanzania wote wampatie kura, Chadema ni Tumaini jipya, makofi kibaoooo, anasema tuanze mabadiliko pamoja
Anasema hataki kuona watu wanalala kwenye nyasi, na tembe; kwa kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi.
Anasema Elimu ya bure inawezekana, atalisimamia swala hilo ili vijana wetu wapate matumaini mapya,
La mwisho kabisa, kuna maswala yanamgusa mtanzania wa kawaida ambayo hawajayazungumzia kwa kuwa hawajafanya utafiti, ila watashughulikia ili watanzania wawe na maisha bora ya kweli.
Kwamba, maendeleo yaitakiwi yawe ya vitu bali ya watu.
Mwisho, Asanteni sana na poleni kwa Spell error, ni kwa sababu speed ya kuongea na kuandika ni tofauti.
Tuko pamoja,
MC
Hilo swali la mgombea mwenza kalijibu vizuri sana.. Aisee Dr Slaa ni kiboko! CCM Kwisha kazi....
kumbe ndo maana kinana alisema ushindi sio lazima
kwasababu alijua kabisa haya mambo yatatokea
Malaria Suguuuuuuuuu uko wapi jamani hahahahahahahhhaaaa aibuuuuuuuu
Dogo ananiambia home Ifakara watu wamelipuka kushangilia utadhani Asoamoah Gyan kasawazisha goli ile siku ya Ghana na Uruguay
malaria suguuuuuuuuu uko wapi jamani hahahahahahahhhaaaa aibuuuuuuuu