Dr Slaa amezungumza vizuri sana. Kwa yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania na alibahatika kuangalia kipindi kile ni lazima ampe kura Dr Slaa, vinginevyo mtu huyo haitakii mema nchi yetu. Nilikuwa nimekaa na wadada wawili ambao wote kabla ya mdahalo kuanza walisema kura zao watampa Kikwete na wabunge wa CCM hata kabla ya kipindi kuisha walikuwa wamebadili mawazo na kusema kwamba kura zao watampa Dr Slaa na wagombea ubunge wa chadema. Hongera sana Rais Mtarajiwa Dr Slaa, hongera sana chadema kwa kuwa makini sana katika kampeni zenu zilizowawezesha kuzikonga nyoyo nyingi za Watanzania.