GE2025 Mdahalo wa wagombea urais 1995: Kwanini siku hizi inashindikana? Samia anaweza?

GE2025 Mdahalo wa wagombea urais 1995: Kwanini siku hizi inashindikana? Samia anaweza?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
1759136121865.jpeg

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, wakati tayari Tanzania ilikuwa imeshabadili mfumo wa chama kimoja kuwa mfumo wa vyama vingi, kulifanyika mdalaho wa wagombea nafasi ya Urais wakati huo kutoka katika vyama vinne vilivyoshiriki uchaguzi, yaani CCM, NCCR Mageuzi, UDP pamoja na CUF

  • CCM mgombea wake alikuwa Benjamin Mkapa
  • CUF mgombea wake alikuwa Prof. Ibrahim Lipumba
  • UPD mgombea wake alikuwa John Cheyo
  • NCCR mageuzi mgombea wake alikuwa Augustine Mrema
Uchaguzi huu wa mwaka 1995 ni moja ya uchaguzi unaosemwa kuwa na upinzani mkubwa hasa kati ya CCM na NCCR Mageuzi baada ya Mrema kujivua uanachama wa CCM na kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi ambapo aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, na baadaye kama mgombea Urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho

Mrema alipohamia Mageuzi alisepana kijiji akiondoka na wanachama wa kutosha pamoja na viongozi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro huku CCM wakikiri kumpoteza kada muhimu na kete moja matata ambayo ingewaongezea ushindi CCM lakini sasa amegeuka kuwa mwiba kwa Mkapa.

CCM ilishinda uchaguzi huo kwa Mkapa kupata 61.8% ya kura, ikifuatiwa na NCCR Mageuzi ambapo Mrema alipata 27.8% ya kura, CUF - 6.4%, na UDP wakiambulia kura laki 2 na ushee.

Pamoja na upinzani kuwa mkali na presha kuwa kubwa Mkapa hakukimbia mdahalo, alishiriki vizuri na kumwaga sera zake na uchaguzi ukafanyika vizuri tu bila kashkash yoyote



Kwanini hili linashindikan wakati huu? CCM imekuwa kama kunguru mwoga, kila anapoitwa kwenye mdahalo wao ni kukimbia na kutafuta kila kiaingizio kuepuka midahalo hiyo.

Mdalaho ukiitishwa sasa Samia anaweza kujitokeza? Lakini pia nawaza Samia kushiriki kwenye mdahalo wa Urais na Mgombea kama Lissu:BearLaugh::BearLaugh::KEKWlaugh: hata ingekuwa wewe Mkuu si ungekimbi nduki kali tusione hat kivuli chako?

Ila hata kwa Mpina, we ungekuwa Samia ungekubali kuaibika kwenye televisheni ya taifa na hadi Gen Z waliangalia?:BearLaugh::BearLaugh::KEKWlaugh:

Unadhani CCM inakwama wapi kushiriki kwenye midahalo ya wagombea urais?
 
CCM wanaogopa, tangu Mkapa hawajawi pata mgombea jasiri wa kumwamini kuweza kupanga hoja na kuongea uhalisia wa kile atakachofanya akiwa Rais.

Sasa sijui wanaongozaje nchi kama mgombea anashindwa kujibu maswali ya waandishi wa habari waliozaliwa tanzania, wakasoma tanzania katika shule alizosoma pia yeye.

Kama alivyowahi kusema prof Assad, hata hawajui wanapigania kwenda ikulu kufanya nini. Hawana focus. Na mtu asipokuwa na focus sio rahisi kumudu mdahalo.

Ndo maana muda wote hata kufungua vikongamano vidogo hawawezi kutoa vitu kichwani mpaka wasome.
 
Hakuna hata mmoja kati ya Mkapa, Mrema na Lipumba alipa division zero form four. Hawa wote walikuwa wasomi kiwango cha lami Europe union standard.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM aliyekuwa na nguvu kipindi hicho hakuwa na GPA ya 2.0 katika digree yake na hii na ndio sababu debate inyooka.
 
Mgombea wa ccm angejaliwa uwezo japo nusu tu ya uwezo wa Lissu wangekubali mdahalo fastaa!
 
Hakuna hata mmoja kati ya Mkapa, Mrema na Lipumba alipa division zero form four. Hawa wote walikuwa wasomi kiwango cha lami Europe union standard.

Mwenyekiti mstaafu wa CCM aliyekuwa na nguvu kipindi hicho hakuwa na GPA ya 2.0 katika digree yake na hii na ndio sababu debate inyooka.
Kwahiyo nani alipata Zero
 
Dr SS atawashinda wote kwenye mdahalo. Ila ikiwapendeza awe ana piga Public lecture National college of Tourism maana royal tour imepanua sana utalii.

Mambo ya clean cooking energy pia awe ana piga public intellectual lectures udsm hasa watu wa engineering.

Unajua Pres. William Ruto au Hata JK alikuwa anapigaga intellectual lectures kule National Defence College
 
Back
Top Bottom