Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.

Shedafa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2008
Posts
802
Reaction score
175
Uchaguzi mkuu ukiwa unakaribia na hata tarehe tayari imetangazwa, nahisi litakuwa jambo la busara kama Jamii Forums ikafikiria kuandaa mdahalo kwa wagombea uraisi.

Naiona JF kuwa na nafasi nzuri kufanikisha hili kwa kuwa haiegemei upande wowote, tofauti na vyombo vingine vya habari hapa nchini. Ni muhimu mwaka huu kuwa na mdahalo kwa kuwa kuna kila dalili baadhi ya wagombea hawatapewe nafasi ya kutosha kuyafikisha mawazo yao kwa wananchi, pia itatoa fursa kwa atakayetaka kututumikia kwa nafasi ya uraisi kujibu maswali ya msingi juu ya mustakabali wa nchi yetu live.

Tumeona uchaguzi wa Marekani jinsi mdahalo ulivyosaidia kuwajua wagombea kabla ya uchaguzi, na tumeona mdahalo wa wagombea U-PM wa Uingereza ulivyosaidia kumuonyesha mtu ambaye asingepewa nafasi na vyombo vya habari. Kama JF ikiona haiweza yenyewe basi itafute ushawishi kwa taasisi au NGO yenye uwezo kuandaa, kwani sifikiri kuwa ni issue kubwa sana. Mbona marehemu Palela aliweza mwaka 2000, na wala hakuwa mwandishi wa habari wa ajabu!

Natanguliza shukrani zangu nikitumai mtalipa uzito.
 
Idea nzuri sana na hapo ndio utaona vizuri uwezo wa viongozi wetu kama bado ujawajua vizuri.
 
a. Kikwete hawezi na hatokuwa tayari kushiriki mdahalo wowote.

b. JF ikiandaa nani atagharimia?
 
Kikwete hawezi kuthubutu "kudahalo" na wengine. He'll get creamed and look bad and I don't think he's ready to lose his shine in that fashion....
 
Idea nzuri sana na hapo ndio utaona vizuri uwezo wa viongozi wetu kama bado ujawajua vizuri.
Profesa, hawa jamaa wengine kwa maneno utawakubali lakini katika matendo, Mungu apishe mbali, si mnamwona mzee wamsafari ma misafara alivyotuvuta 2005 tukadhani Nyerere amerudi kumbe ni maneno tu hata kwenye kanga yapo. But nauheshimu sana mchango wako!
 
Wapinzani ndio waombe huo mdahalo ufanyike hiwe challenge kwa ccm tuone kama watakubali.na wakikubali hio siku jk lazima apate safari ya ghafla lol. Mkuu genekai cha ajabu hata maneno hawana mbona ya kuweza kumfanya mtu mwenye akili timamu kuingia mkenge.maneno yenyewe ni"maisha bora kwa kila mtanzania" bila ya kuweka wazi mikakati yoyote .hata mtoto wa miaka saba anaweza kutumia huo mstari mbona.
 
a. Kikwete hawezi na hatokuwa tayari kushiriki mdahalo wowote.

b. JF ikiandaa nani atagharimia?
Mheshimiwa kwa la kwanza sina jibu, ila la pili nafikiri palipo na nia pana njia. Ukweli kama kuna uwezekano wowote wa kusaidia basi ndio wakati, hasa kwa mtu kama wewe mkuu.
Natanguliza shukrani.
 
Mr 'me, I and myself' yupo.

Ama
JF Senior Expert Member

Join Date Fri Jan 2010

Mkuu upo kwa ajili ya kazi moja tu nayo ni kazi moja tu???? Could it be possible to be rational in some subject?

 
- Nafikiri it is not about mdahalo, but atadahalo na nani mwenye enough credibility to dahalo, au tutakuwa tunadahalo tu for the sake ya kudahalo? Maana unpataje a serious dahalo na kina Mrema? Labda Mpendazoe akiwa on the other side, nina wasi wasi sana na alternatives tulizonazo as far as national leadership is concerning labda the serious candidates hawajajitokeza, lakini I have a big problem na wengi tulionao tayari kwamba they are not up to the challenge,

- Guys nafikiri seriously Tanzania tuna National leadership crisis, au?

Respect.


FMEs!
 
FMES,
It would be interesting to see Kikwete debate Dr. Slaa.
 
FMES,
Unaweza ukawa uko sawa, lakini tunahitaji kuwaona hata hao unaowatilia mashaka. Yaani wapewe nafasi ya kweli ya kujiuza sivyo ilivyo sasa, mdahalo nafikiri ni mahali pazuri maana ni ana kwa ana. Hupati msaada wa wataalamu, maana wengine wanaonekana wazuri kwa kuwa wana msaada.
 
FMES,
It would be interesting to see Kikwete debate Dr. Slaa.

- Sawa sawa, lakini mjadala utakuwa very limited in producing national's solutions kwa sababu, Chadema as chama recently kimekuwa na muelekeo unaofanana sana na CCM, infact hata viongozi wao wengi katika kutetea mienendo yao mibovu ya kuipindisha Demokraisa wamewa-cite sana CCM, ndio maana ninasema kwamba hata mjadala na Dr. Slaa hautakuwa what it should kwa sababu ya the resemblance ya ubovu wa hivi vyama, sawa Dr. Slaa anaweza kusimama as leader on his own capacity, lakini sasa on that pace ni vigumu sana kupata jawabu kwa taifa kwa sababu linatakiwa jawabu la chama collectivelly kama unataka kum-demolish Rais na CCM,

- Ninasema ninapata sana kigugumizi na alternatives tulizonazo as far as uongozi wa taifa na hasa on political parties level, huenda hatuna if you know what I mean! Maana hata Mwenyekiti wa Chadema si ameshasema hatagombea urais atatafuta ubunge that is depressing! Slaa hawezi kugombea urais on his own bila a strong backing ya chama cha siasa, sasa labda kiwe chama cha CCJ ambacho so far hatukijui, lakini sio mashetani tunayoyajua tayari!

Respect.


FMEs!
 

- Tatatizo ni kwamba wengiwao ni CCM agents, sasa kweli unaamini Mwenyekiti wa CCM atapata tatizo kudahalo na his plants? I mean huenda kuna walio clean lakini binafsi ninapata wasi wasi sana na what is an alternative to CCM.

Respect.


FMEs!
 
Mdahalo ukifanyika kwenye TV ataangalia nani? Ni asilimia ndogo sana ya Watanzania wana TV. Hata wenye umeme wa hiyo TV ni wachache sana. Au tunazungumzia mdahalo wa redio?

Mzee ES anasema kuna crisis ya viongozi Tanzania. Kwa maana gani? Hakuna uhaba wa wenye vipaji vya uongozi. Tuko milioni 40. Tatizo ni kwamba wenye vipaji hawana nafasi ya kujitokeza. CCM imehodhi madaraka, na kuzuia wengine kupata nafasi.

Akijitokeza kiongozi nje ya "wenzetu", basi mara utasikia ana UCHU WA MADARAKA. Ila CCM wenyewe hawana uchu wa madaraka!

Dr Slaa could take on JK, anytime, anywehre. But JF does not have the wherewithal to organise such a match!
 
Ukumbuke mheshimiwa si mara ya kwanza kufanyika mdahalo hapa Tz, ulishafanyika huko nyuma na ulifanyika kwa njia ya TV. Kwa hiyo wazo kuwa watu hawataona kwa kuwa hawana TV si la msingi, la msingi ni jinsi gani itawezekana kufanyika mdahalo. Bahati mbaya inaonekana uko nje ya Tz, ungekuwa nyumbani ungekuwa umeona mfano mdogo tu. Katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku uliopita kilionyeshwa kijiji nafikiri ni Mara kimezingirwa na mafuriko lakini jamaa wanakula nyuzi toka kwenye luninga yao wakiwa wameiweka juu ya stuli huku chumba kizima kikiwa kimejaa maji. Utafurahi nikikwambia kuwa bado wanatumia ungo, ina maana wanapata matangazo kwa gharama kubwa lakini wanajua umuhimu wa habari.
 
Ni watu(wapiga kura) wangapi wanategemea kushudia mdahalo huo?Endapo kutafanyika mdahalo huo
 
It is a very good idea.lakini je do we think kwamba watanzania wanachagua mtu anayejua kujieleza au wana vigezo vyao vingine?Kwa sasa Tz hatujafikia hali ya kufanya midhahalo kwa wagombea wetu kwani mpaka sasa ninavyoandika tayari watu wanajua watamchagua nani bila kujali anajua kujieleza ama la.Hayo ya midahalo labda kwenye siku za usoni lakini sio sasa ni kupoteza muda tu.
 

FMES
Unaposema hujaona kiongozi wa kufanya mdahalo na Kikwete sijakuelewa na hao viongozi mashetani unaowasema ni akina nani na unajuaje huyo Mpendazoe na CCJ yake sio yale yale mashetani unayoyasema au Kikwete naye yuko ndani ya hayo mashetani ya uongozi

Mdahalo ni sehemu ya demokrasia hivyo hata hao viongozi mashetani unaowaita tunawataka wafanye debate tuwajue tutawachuja na kuchuja pumba zao na si speculations tu kuwa hawafai. Debate si sehemu ya ku solve matizo ya taifa ni kujua personal confidence ya mgombea anavyoweza kujieleza mwenyewe na kuelezea masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa mdomo wake si kwa kusoma alichoandikiwa hata kama anayajua yako kwenye mafaili yake lakini watu wanataka kusikia na kuona uwezo alionao wa kumbukumbu kichwani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…