Shedafa
JF-Expert Member
- May 21, 2008
- 802
- 175
Uchaguzi mkuu ukiwa unakaribia na hata tarehe tayari imetangazwa, nahisi litakuwa jambo la busara kama Jamii Forums ikafikiria kuandaa mdahalo kwa wagombea uraisi.
Naiona JF kuwa na nafasi nzuri kufanikisha hili kwa kuwa haiegemei upande wowote, tofauti na vyombo vingine vya habari hapa nchini. Ni muhimu mwaka huu kuwa na mdahalo kwa kuwa kuna kila dalili baadhi ya wagombea hawatapewe nafasi ya kutosha kuyafikisha mawazo yao kwa wananchi, pia itatoa fursa kwa atakayetaka kututumikia kwa nafasi ya uraisi kujibu maswali ya msingi juu ya mustakabali wa nchi yetu live.
Tumeona uchaguzi wa Marekani jinsi mdahalo ulivyosaidia kuwajua wagombea kabla ya uchaguzi, na tumeona mdahalo wa wagombea U-PM wa Uingereza ulivyosaidia kumuonyesha mtu ambaye asingepewa nafasi na vyombo vya habari. Kama JF ikiona haiweza yenyewe basi itafute ushawishi kwa taasisi au NGO yenye uwezo kuandaa, kwani sifikiri kuwa ni issue kubwa sana. Mbona marehemu Palela aliweza mwaka 2000, na wala hakuwa mwandishi wa habari wa ajabu!
Natanguliza shukrani zangu nikitumai mtalipa uzito.