Oxlade-Chamberlain
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 8,635
- 2,205
Eti gazeti la uhuru linadai madai ya Dr Slaa yakutaka mdahalo ni kumvunjia heshima Kikwete.
hakika, umenifumbua macho katika swala hili, aaah kuuumbe, asante sana.Wanamaanisha kwamba wananchi wote wanajua uwezo mdogo wa raisi wetu wakuchambua mambo inakuwaje Dr.Slaa anataka mdahalo? yaani wanaona anataka kumdhalilisha raisi mbele ya wananchi wote waone uwezo wake mdogo wa kuongoza na ndio maana wanaona kamvunjia heshima.
Ndio akili ya ccm hio mkuu .
baada ya mgombea urais kupitia chadema dr. Wilbroad slaa kutoa mwito kwa rais kikwete kusimama nae katika mdahala kujadili mustakabala wa taifa hili, rais kikwete ameingia mitini kwa kuhofia kuumbuliwa hadharani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tambwe hiza kwa vyombo vya habari jana, amesema rais hatafanya hivyo kwa kuwa saa 1 haitoshi kuelezea sera za ccm na wanaotaka kujua nini ccm inataka kufanya miaka mitano ijayo yote yameainishwa katika 'election maifesto' yao na rais atapita nchi nzima kuelezea wananchi
hii inadhihirisha tunaongozwa na viongozi wa aina gani. Iwapo bwana kikwete angethubutu kusimama na dr slaa katika mdahalo wanatambua wazi kuwa angeumbuka kwa kuwa hata katika hotuba zake anaandaliwa data muhimu na wakati mwingine sio sahihi.
Hivyo kama ataulizwa maswali ya papo kwa papo wakati mwingine anaweza kukosa majibu. Vile vile wanatambua asingeweza kukabiliana na challenge za dr slaa kuhusu madudu aliyoyafanya miaka mitano iliyopita hasa kushindwa kuwashughulikia mafisadi pamoja na uchumi ambao unaanguka licha ya kuwadanganya wananchi kuwa pato la mtanzania limeongezeka wakati wa utawala wake. (they did not tell the people about inflation rate and how the purchasing power of the common citizen has been affected)
je wanajamii mna maoni gani kuhusu msimamao wa rais wetu?
Mchungaji Slaa kwanini asifanye mdahalo na mkewe atoke CCM na kuamia Chadema? kama kashindwa kum-convince mkewe atamuweza nani?
Huyu mchungaji yuko weak iweje mkewe mpaka leo kabaki CCM? inamaana hamuamini mumewe? Afanye mdahalo chumbani na mkewe kabla hajafanya na wananchi
Mchungaji Slaa kwanini asifanye mdahalo na mkewe atoke CCM na kuamia Chadema? kama kashindwa kum-convince mkewe atamuweza nani?
Huyu mchungaji yuko weak iweje mkewe mpaka leo kabaki CCM? inamaana hamuamini mumewe? Afanye mdahalo chumbani na mkewe kabla hajafanya na wananchi
kikwete amekuwa mzuri kuzungumza kwenye vyombo vya habari kila jumamosi je ni kwa nini asifanye debate na wagombea wengine ili tujue msimamo wake vizuri. Mkapa alifanya debate je ni kwanini raisi wa nchi achaguliwe bila debate!!
Kwa nini raisi kikwete unaogopa mdahalo,be a man,unaonyesha wazi kwamba ujafanya lolote la maana ndiyo sababu unaogopa mdahalo.kama wewe ni mwanaume ingia mdahalo na dr slaa
Kikwete amekuwa mzuri kuzungumza kwenye vyombo vya habari kila jumamosi je ni kwa nini asifanye debate na wagombea wengine ili tujue msimamo wake vizuri. Mkapa alifanya debate je ni kwanini raisi wa nchi achaguliwe bila debate!!