Kikwete amelewa madaraka, na kuwa anajua iwe isiwe atakuwa raisi. Hiii mentality ya namna hii ni mbaya sana kwa ukuaji wa demokrasia.(Redet tafiti zenu zinabaka Demokrasia, japo zaweza kuwa sahihi, lakini zinapaswa kutafitiwa kila week wakati wa mchakato huu wa uchaguzi. Hillary Clinto alikuwa anaongoza kwenye primaries kwa kura za maoni, lakini siku za kupiga kura zilivyokuwa zinakaribia lead yake ikawa inakuwa eroded pole pole hadi kupitwa na Obama). Kikwete alivyochukua form kuomba kuteuliwa na CCM hakuhangaika kuzunguka kuomba udhamini, mwaka 2005 alizunguka karibu nchi nzima. Hiyo ni dharau, akamtuma kijana wake, hilo lilikuwa ni tusi kwa watanzania na wenye kuipigia magoti CCM. Mdahalo ni jambo zuri, aingie mlingoni ajibu maswali magumu, kutokuonekana kwa vipindi viwili ni kuset precedence mbaya sana kwa mustakabali wa taifa letu. Kama JK hawezi kuielezea CCM manifesto kwa dakini 10 au 20, then hatoweza kuitekeleza kwa miaka mitano ijayo, lets be serious. Mdahalo ni haki ya wananchi, and we have right to demand so, JK acha uwoga, jitokeze, unaweza kuwashawishi wale ambao wameshakusideline na ambao walishaamua kuwa hawatopiga kura mwaka huu lakini wamebadili msimamo baada ya Shujaa na mwenye heri mpakwa mafuta Dr Slaa kuinuliwa.