baada ya mgombea urais kupitia chadema dr. Wilbroad slaa kutoa mwito kwa rais kikwete kusimama nae katika mdahala kujadili mustakabala wa taifa hili, rais kikwete ameingia mitini kwa kuhofia kuumbuliwa hadharani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tambwe hiza kwa vyombo vya habari jana, amesema rais hatafanya hivyo kwa kuwa saa 1 haitoshi kuelezea sera za ccm na wanaotaka kujua nini ccm inataka kufanya miaka mitano ijayo yote yameainishwa katika 'election maifesto' yao na rais atapita nchi nzima kuelezea wananchi
hii inadhihirisha tunaongozwa na viongozi wa aina gani. Iwapo bwana kikwete angethubutu kusimama na dr slaa katika mdahalo wanatambua wazi kuwa angeumbuka kwa kuwa hata katika hotuba zake anaandaliwa data muhimu na wakati mwingine sio sahihi.
Hivyo kama ataulizwa maswali ya papo kwa papo wakati mwingine anaweza kukosa majibu. Vile vile wanatambua asingeweza kukabiliana na challenge za dr slaa kuhusu madudu aliyoyafanya miaka mitano iliyopita hasa kushindwa kuwashughulikia mafisadi pamoja na uchumi ambao unaanguka licha ya kuwadanganya wananchi kuwa pato la mtanzania limeongezeka wakati wa utawala wake. (they did not tell the people about inflation rate and how the purchasing power of the common citizen has been affected)
je wanajamii mna maoni gani kuhusu msimamao wa rais wetu?