FMES,
Mbona una give up kirahisi namna hii mkuu? Ndio tunajua hatuna watu mahiri katika uongozi, mdahalo utawasaidia Watanzania wengi kuelewa udhaifu huu na hata watafakari kama kuna haja ya kuendelea na mazoea.
Just think pale Mttikila akianza kumbana Kikwete na maswali magumu na kuonyesha wazi ni jinsi gani CCM ilivyo mbofumbofu.
Think about kule kwenye majimbo atakapobanwa Sitta na kuulizwa miaka yote 40 kaleta nini cha maana Urambo na watu wakamkokotoa kwa kutumia yale maswali yangu 22 niliyowahoji Chadema kwa nini hawayatumii kwenye Operesheni Sangara.
Kampeni za Tanzania zinabidi kubadilika sura, ni ahadi zinahutubiwa zikiandamana na pilau, gagulo na hizi hongo sasa hivi mara sijui Ambulance au Msolla kuweka Umeme wa Upepo jimboni mwake ili watu wachaji simu zao bure.
75% ya Wabunge na Wawakilishi ni watu dhaifu. Hawafanyi kazi majimboni, hawatetei wananchi wao hata kuibana Serikali ila wao hukimbilia kwa Wafadhili na kukilinda Chama na serikali na kusahau kuwa wajibu wao mkuu ni kuibana Serikali kuu ili ilete maendeleo kwa Wananchi na si kutegemea misaada.
Tumechoka ahadi, tumechoka kungoja, tumechoka kuburuzwa, tumechoka kudanganywa, tumechoka kuambiwa subirini kesho tumechoka, tumechoka, tumechoka.
Tunataka mapinduzi mapya na sura mpya itakayotupa nuru mpya na pumzi mpya na hata kama mayai 20 katika trei ni mabovu, ni lazima tuwaambie wananchi ubovu wao na mdahalo ni njia moja wapo.
Ikiwa sisi hapa tunawachambua na kujua udhaifu wao, hamuoni kuwa tukianza mchakato wa kuwachambua Wabunge wote na Wawakilishi waliopo madarakani na kuwaambia wananchi wa majimbo kuwa huu ndio uchapakazi wa mbunge na mwakilisho wao na kuonyesha jinsi alivyoshindwa kuleta maendeleo au kuiaamsha serikali ilete maendeleo basi ule ugoigoi utaanza kufutika.
Tena kazi yetu ya kuchambua na kudahalo isiishie kwenye uchaguzi pekee, bali iwe ni kazi ya kudumu ya kila siku?