Mdau ahoji magari ya serikali kuwa katika haraka wakati wote

Mdau ahoji magari ya serikali kuwa katika haraka wakati wote

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
"Magari ya serikali mara zote yanaonekana kuwa na haraka! Hali hiyo ya haraka haionekani popote katika majukumu yao rasmi.

Kwa nini?"
Screenshot_20260328-142030~2.jpg
 
"Magari ya serikali mara zote yanaonekana kuwa na haraka! Hali hiyo ya haraka haionekani popote katika majukumu yao rasmi.
Kwa nini?"
View attachment 3563688
ni mila desturi na utamaduni wa dunia nzima,
hakuaanza juzi, jana au leo.

utaratibu huo ni wa makrne mengi yaliyopita na hakuna namna ya kuubadili tuendako.
 
Kuwahi maendeleo waala,inafikirisha sana maana utendaji mbovu,sio maji,si umeme,sio huduma sa afya mana hata wagonjwa husubirishwa na misafara,sio elimu ,yani kiufupi wanapenda washikilie vitu vidogo vidogo mara uskie choo kimezinguliwa na ving’ora makelele kibao
Mtu mweusi si bure kuna jambo tulimkosea Muumba wetu
 
Speed huwa inaendana na aina ya gari. UNA VX 8 UNATAKA utembee mwendo wa RAV4? Lakini pia speed huashiria uimara na umakini wa dereva barabarani, speed huashiria na huwakilisha namna gani wanatakiwa kufanya na kulekeleza maendeleo kwa speed. nb mengine nimechapia,ila cha muhimu ni kuwa speed hutokana na aina ya gari.
 
Hii kila siku nasema ndio picha halisi ya sisi watanzania weusi. Bado hatijastaarabika tutate tusitake

Hao viongozi, polisi, wanajeshi ndio makundi yanasisitiza ufuatiliaji wa sheria lakini wao ndio namba moja kuvunja sheria. Hii ni kitu inaonesha straight away hatujastaarabika

Unakuta mkuu wa polisi au gari tu ya jeshi/polisi anatoka kazini anaenda nyumbani hana emergency yoyote lakini hataki kukaa foleni anatanua ving'ora vingiiii na kweli matrafiki wanampisha 'wanamvuta' sasa unajiuliza hivi huyu anajua maana ya sheria? So sheria inawahusu baadhi ya watu masikini ila wao wako juu ya sheria?

Unakuta viongozi au chama kwenye uchaguzi wao wanafanya rafu za aina zote ila vyombo vya dola na tume wako kimya wanawa back tu sasa unajiuliza tena hivi are we serious as a nation?
 
Back
Top Bottom