- Mkuu kuendesha TV na Radio station bongo sio kazi ndogo, ni kazi kubwa sana ndio maana hata jamaa yangu imempa taabu kidogo kuianzisha, ni lazima TV iwe a money making machine, Mengi anaiweza kwa sababu anazo biashara nyingi zinaoweza ku-cover hasara kutoka huko TV,
- Siasa haiwezi kuvuta biashara ya Ads, katika bongo kinachoweza kuleta hela za Ads ambazo ndio muhimu kuiendesha station kwa Tanzania ni michezo kwanza halafu mengine baadaye,wa-Tanzania wanapenda maigizo, mpira, comedy, Muziki wa Wa-Congo, wanaipenda siasa only kama kuna kasheshe huko ndani between watawala, au kama kuna chaguzi ndogo kama hiyo ya Biharamulo, lakini ikiisha tu basi huwapati, na otherwise hawana kabisa interest na siasa wala elimu ya siasa kwenye TV.
- Ninataka kuamini kwamba jamaa yako ana biashara nyingine nzito zinazoweza kuibeba hii ya TV mara kwa mara, kwa sababu itakua na misimu ya kuingiza na kutoingiza pia, sasa ni suala la kuwa makini na ku-balance hizi business acts, inahitaji moyo sana ama sivyo ataisia kuwauzia Wahindi kwa bei ndogo sana, mwambie awe makini sana na kuisoma hali ya mazingara kabla hajaifungua rasmi.
Ahsante.
William.